Sakata la watumishi hewa: RC Makonda awaapisha wakuu wa Idara wote jijini Dar

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
Screen-Shot-2016-05-02-at-3.51.43-PM.png

Wakuu wa Idara zote za jiji la dsm pamoja na maafisa Utumishi wa halmashauri za jiji wamesaini kiapo cha kazi mbele ya Mkuu wa mkoa na wakuu wa wilaya baada ya kubainika kutoa taarifa zisizo za kweli dhidi ya kuwepo kwa watumishi hewa katika idara zao baada ya kubainika watumishi hewa wengine 209 katika Uchunguzi wa Siku chache zilizopita.

Miongoni mwa masharti yaliokuwapo katika kiapo hicho ni kwamba iwapo ikigundulika kuwapo kwa watumishi hewa katika idara husika baada wiki moja ijayo,Afisa utumishi au mkuu wa idara hiyo atalipa gharama za mishahara iliyopotea,kushitakiwa kwa uhujumu uchumi,kuachishwa kazi lakini pia kufikishwa mahakamani.

Hatua ya kusaini na kula kiapo inatokana na baadhi ya wakuu wa idara pamoja na maafisa Utumishi katika jiji la DSM kudaiwa kutoa taarifa za uongo kwa Mkuu wa mkoa Paul Makonda na wakuu wa wilaya za jiji hilo baada ya kutoa idadi ndogo ya watumishi hewa kwa mkoa wa dsm ambao walikuwa 74 tu, huku uhakiki wa sasa uliofanywa na tume maalum ukibaini watumishi hewa 209 ambao wametafuna kiasi cha takribani shilingi bilion 2.7

Kiapo hicho cha kazi kiliionekana kuwa mwiba kwa watumishi hao wa mkoa wa DSM kutokana na wengi wao kushindwa kujaza,huku wakileta hoja ambazo zilionekana kutokuwa na nguvu kwa mkuu wa mkoa kwa kuogopa kujifunga mpaka pale Bwana Makonda alipotoa dakika 5 kujaza na kuwasilisha.

Baadhi ya wakuu wa idara pamoja na maafisa utumishi wamesema kiapo hicho ni kizuri kwa ajili ya Utendaji kazi lakini ni mwiba kwa wakuu wa idara hasa kutokana na wengi wao kufanya kazi kwa mazoea, huku Katibu tawala wa mkoa wa Dsm THERESIA MBANDO akikiri kuwepo kwa taarifa zenye utata juu ya idadi ya watumishi hewa.

Source: Channel Ten
 
Na bado tutaona mengi, umasikini mbaya people could otherwise pack up and go!
 
Ni kweli mkuu, bado lakini natafakari madhara ya hivi viapo.

Strategy hii inaweza kufanya vizuri sana kama itafanikiwa hata kwa mikoa mingine, maana wengi wa hawa watumishi hewa wanapikwa na hawa wakurugenzi wa idara za halmashauri.
 
Huu ndiyo ubunifu tunaoutaka, hongera mkuu wa mkoa, na ikibidi kila nusu mwaka uwe unapata ripoti ya idadi ya watumishi ambayo itakuwa imesainiwa na wakuu wote wa idara, na kwenye kazi za internal auditors kiongezwe kipengele cha watumishi hewa kwenye kazi zao.
Hata mimi nimeona huu ubunifu murua sana.

Wakuu wote wa mikoa na wilaya inabidi kuiga huu mkakati, utapunguza sana hii kadhia ya utumishi hewa.
 
HUU NI USHENZI NA UDHARIRISHAJI KWA WAFANYAKAZI.! IWEJE MAOVU YA CCM WATUPIWE WAFANYAKAZI?! WAMEKUBALI KWA UOGA TU! CCM ACHENI KU"HARASS" WAFANYAKAZI!
Mkuu wa idara unawajibika kwa watumishi walio chini yako. Sio kwa CCM. Siku nyingi nimekuwa nasema Makonda anafanya mambo kwa kupenda kujionyesha lakini hili alilofanya namuunga mkono kwa asilimia zote. Sasa kama wewe ni mkuu wa idara kuna shida gani ya kujua watu walio chini yako? Kama huwezi basi bora ukae nyumbani! Tukiendelea namna hii tutapata maendeleo na watu watafanya kazi kwa bidii!
 
Huyu Mama Mbando ndio yule alikuja na zuio "fake" la Uchaguzi wa Mayor wa Jiji?
Akala kashikashi akajidai kazimia na kuibiwa mkoba,kuulizwa ndani ya mkoba kulikuwa na nini!?Akasema simu na taulo ya kike
Kuulizwa aina ya simu,akataja Sumsung....Watu kuibeep simu ikaanza kulilia toka kwenye manyonyo yake
Watu wakampa nakozi mbili tatu....Hii kesi akabambikiwa Halima Mdee,hata sijui imeishia wapi?

Haya sasa,na yeye kaapishwa leo...Wakibainika hewa hata wawili akajiandae kunyea debe,Maana "Uhujumu uchumi" (kama kweli ni kosa kwa kutotambua watumishi hewa) ni kosa lisilo na dhamana

CCM ni kama yale Mauchawi ya Kibena na Kihehe,Pembe linakaa chini ya uvungu linalishwa damu,Wanayaita "Ndilye-Kiki"....Ukililisha damu halina nongwa,Likikosa damu hata yako linakunywa!!Utauwa woooote wa ukoo wako,wakiisha linakugeukia wewe na kukunyonya

Mama Mbando umewasaidia sana CCM kwenye umeya mpaka "ukanyonya" damu za watu,Sasa zimeisha wanakunyonya mwenyewe
 
Makonda katika ubora wake! good....... wengine muige namna hii ya ubunifu wa makonda. Pongezi nyingi sanamheshimiwa. Hii ishu ya ghost wek inahangaisha serikali nyingi sana wala siyo hapa tu. Naamini kw spidi hii y JPM atatoa somo kwa inchi zote.
 
Makonda ni mtu anayefanyia Kazi maagizo yote toka ngazi za juu. Mtakumbuka wakati Mawaziri na manaibu wao wanakula Kiapo Waziri mkuu na Katibu mkuu wslisema kiapo kitafika mpaka kwa wakuu wa Idara wakuu wengine hawapendi kwenda na wakati.
Makonda katimiza wajibu.
 
Watumish wa serikalin wamegeuzwa kuwa punching bag za wanasiasa, hii yote ni sababu ya umasikin uliokithiri pamoja na ukosefu wa maarifa wa wanasiasa wetu. Tulisha discuss sana hili swala, watumish hewa wanatokana na, information asymetry, na kila baada ya muda watabadilika na watakuwepo tu, lakin watu hawaelewi, mnawafeed viongoz taarifa zisizo sahihi sababu ya woga. Tulishafanya kazi council tunalijua hili. Halafu hawa viongoz wa ccm wanawadhalilisha sana wafanyakazi, sheria za utumishi wa umma ziko wazi, na zimeelekeza kila hatua ya kuchukua, na viapo watu wanavifanya mwanzo, mm ningekuwa serikalin nisingeapa bora kuacha kazi, kuliko kudhalilishwa.
 
Rafiki njaa utafanya nini?
 
Back
Top Bottom