Sakata la Wamachinga: Suluhisho pekee ni Serikali kuhimiza wananchi kufanya biashara rasmi kwa mujibu wa sheria na kusimamia maslahi ya pande zote

Peter Madukwa

JF-Expert Member
Sep 20, 2012
3,134
2,465
Salaam;

Hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh Amos Makalla ametoa maagizo ya kuwataka wamachinga waliopanga bidhaa zao barabarani kuondoka mara moja katika maeneo hayo.

Maagizo haya yametokana na mgogoro uliopo kati ya wafanyabishara rasmi waliopanga katika maduka dhidi ya wamachinga wanaopanga bidhaa mbele ya maduka na katika barabara kwa kile kinachoelezwa kuwa wafanyabiashara rasmi kukosa soko huku wakilipa kodi lukuki kulinganisha na wamachinga ambao hulipa 20000 tu kwa mwaka.

Aidha agizo hilo linatokana na ukweli kuwa wamachinga wanaopanga bidhaa barabarani wanaleta usumbufu ktk usafiri kwa sababu barabara zinakuwa hazipitiki kutokana na wao kuzibana barabara kwa kupanga bidhaa ktk barabara.

Kimsingi wafanyabiashara waliopanga ktk maduka wanayo haki ya kulalamika kwa sababu

1. Wanafanya biashara rasmi kwa mujibu wa sheria
2. Wanalipa kodi ya mapato
3. Wanalipia leseni ya biashara
4. Wanalipa gharama ya kodi ya jengo na ushuru wa huduma na gharama zingine kedekede
5. Mauzo yao yanaporomoka na hivyo wanakuwa ktk wakati mgumu na hata kupunguza mapato ambayo serikali ingeweza kukusanya.

Kwa mtizamo wangu kutokana na utata wa jambo hili serikali ichukue hatua zifuatazo

1. Wafanyabiashara rasmi walindwe maslahi yao kwa kuwa wao ndiyo hulipa kodi nyingi kwa serikali na kwamba wanafanya biashara kwa mujibu wa sheria.

2. Wamachinga waondolewe mara moja na kama serikali ina nia ya kuwalinda wamachinga basi wawatengee eneo lao katikati ya mji wawajengee vbanda vyao vidogovidogo wawapangishe na walipe kodi

3. Wakati serikali inaendelea kuwabeba wamachinga iwape muda wa kufanya biashara isiyo rasmi na kuwasisitiza kurasimisha biashara zao na umachinga isichukuliwe kama jambo la kudumu kwa kuwa serikali inapoteza mapato mengi kupitia informal business. (Serikali isimamie sheria na ikibidi hata kwa kulazimisha watu kuhama kutoka ktk machinga kwenda ktk mfumo rasmi wa kibishara)
4. Serikali itenge maeneo kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo na miundombinu ijengwe (inaweza kuwa vibanda vidogovidogo ila vya kisasa na siyo mfumo wa ghorofa kama machinga complex). Katika utekelezaji wa jambo hili serikali ni vema ikashirikisha wadau mbalimbali kabla ya utekelezaji ili kukwepa kufeli kama ilivyofeli machinga complex. Serikali ijenge vibanda hivyo katika maeneo yanayozunguka masoko makubwa kama kariakoo, Tegeta, mbagala, gongolamboto, temeke, kimara, mbezi, ubungo, mwenge n.k. aidha wafanyabiashara wadogo ni lazima wawe na leseni ya biashara na walipe kodi lakini gharama ya kupangisha ktk vibanda vyao angalau iwe nafuu. Hili lisiwe jambo la hiyari; kurasimisha biashara iwe jambo la lazima; asiyeweza kufanya biashara rasmj akatafute shughuli ya kufanya.

5. SERIKALI iboreshe mazingira ya kibiashara mikoani na kuimarisha sekta zingine kama kilimo, uvuvi, madini n.k ili kupunguza kasi ya vijana wanaohamia mjini Dsm na ktk majiji mengine.

FAIDA YA KURASIMISHA BIASHARA

1. Itapunguza mgogoro kati ya wafanyabiashara rasmi na machinga
2. Itarahisisha ukusanyaji mapato
3. Itakuwa rahisi kuwa na takwimu halisi za wafanyabiashara kuanzia ngazi ya kitongoji hadi kitaifa
4. Itakuza uchumi wetu na kuboresha miundombinu
5. Itakuwa ni rahisi kwa serikali kuboresha huduma za kijamii
6. Kuokoa muda katika jiji la Dsm unaotokana na msongamano usio wa lazima
7. Majiji yetu yatakuwa safi na katika mpangilio unaovutia
8. Taasisi za kifedha itakuwa rahisi kuwafikia wafanyabiashara ikiwemo katika mikopo

Nasisitiza kuwa; linapokuja suala la serikali kufanya maamuzi iwalinde zaidi wale wanaofanya biashara rasmi kwa kuwa ndiyo wanaolipa kodi na stahili mbalimbali kwa mujibu wa sheria.

Kwa hiyo naunga mkono suala la serikali kuwaondoa wamachinga kwa namna yoyote ile na kwamba umachinga usichukuliwe kama mfumo rasmi na wa kudumu wa kibiashara ni lazima tubadilike ili serikali ikusanye mapato kwa uhakika na kila mwananchi awajibike kwa nafasi yake.

Kwa ujumla maamuzi yasiegamie ktk maslahi ya kisiasa bali yaegamie ktk maslahi ya kiuchumi ya nchi yetu ili tuweze kuwa na taifa linalojiendesha ktk misingi ya haki na sheria, nidhamu na uwajibikaji.

Tukumbuke kuwa kila mwananchi ajue ana wajibu wa kulipa kodi stahili ili tuweze kujenga nchi yetu.
download.jpeg

images.jpeg
 
Salaam;

Hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Amos Makalla ametoa maagizo ya kuwataka wamachinga waliopanga bidhaa zao barabarani kuondoka mara moja katika maeneo hayo.

Maagizo haya yametokana na mgogoro uliopo kati ya wafanyabishara rasmi waliopanga katika maduka dhidi ya wamachinga wanaopanga bidhaa mbele ya maduka na katika barabara kwa kile kinachoelezwa kuwa wafanyabiashara rasmi kukosa soko huku wakilipa kodi lukuki kulinganisha na wamachinga ambao hulipa 20000 tu kwa mwaka.

Aidha agizo hilo linatokana na ukweli kuwa wamachinga wanaopanga bidhaa barabarani wanaleta usumbufu ktk usafiri kwa sababu barabara zinakuwa hazipitiki kutokana na wao kuzibana barabara kwa kupanga bidhaa ktk barabara.

Kimsingi wafanyabiashara waliopanga ktk maduka wanayo haki ya kulalamika kwa sababu

1. Wanafanya biashara rasmi kwa mujibu wa sheria
2. Wanalipa kodi ya mapato
3. Wanalipia leseni ya biashara
4. Wanalipa gharama ya kodi ya jengo na ushuru wa huduma na gharama zingine kedekede
5. Mauzo yao yanaporomoka na hivyo wanakuwa ktk wakati mgumu na hata kupunguza mapato ambayo serikali ingeweza kukusanya.

Kwa mtizamo wangu kutokana na utata wa jambo hili serikali ichukue hatua zifuatazo

1. Wafanyabiashara rasmi walindwe maslahi yao kwa kuwa wao ndiyo hulipa kodi nyingi kwa serikali na kwamba wanafanya biashara kwa mujibu wa sheria.

2. Wamachinga waondolewe mara moja na kama serikali ina nia ya kuwalinda wamachinga basi wawatengee eneo lao katikati ya mji wawajengee vbanda vyao vidogovidogo wawapangishe na walipe kodi

3. Wakati serikali inaendelea kuwabeba wamachinga iwape muda wa kufanya biashara isiyo rasmi na kuwasisitiza kurasimisha biashara zao na umachinga isichukuliwe kama jambo la kudumu kwa kuwa serikali inapoteza mapato mengi kupitia informal business.

Nasisitiza kuwa; linapokuja suala la serikali kufanya maamuzi iwalinde zaidi wale wanaofanya biashara rasmi kwa kuwa ndiyo wanaolipa kodi na stahili mbalimbali kwa mujibu wa sheria.

Kwa hiyo naunga mkono suala la serikali kuwaondoa wamachinga kwa namna yoyote ile na kwamba umachinga usichukuliwe kama mfumo rasmi na wa kudumu wa kibiashara ni lazima tubadilike ili serikali ikusanye mapato kwa uhakika na kila mwananchi awajibike kwa nafasi yake.

Kwa ujumla maamuzi yasiegamie ktk maslahi ya kisiasa bali yaegamie ktk maslahi ya kiuchumi ya nchi yetu ili tuweze kuwa na taifa linalojiendesha ktk misingi ya haki na sheria na uwajibikaji.
Hata kama kuna ulichosahau ila ulichosema ni sawa sana
 
Hakuna LA kujadili hapa ila ikumbukwe kila MTU chochote apatacho lazima atoe fungu kwa ajli ya Kodi ya maendeleo ya taifa lake
 
Kila uwongozi wa serikali unapoanzia mtaa au kijiji mwenyekiti awe na taarifa ya idadi ya wakazi na kati ya hao wafanya biashara ni wangapi.

Katika mipango ya serikali kujenga vituo vya afya, shule, kituo cha polisi pia kuwe na ujenzi wa soko.
 
Option ni mmoja tu, kutengeneza sera madhubuti za kilimo zitakazotengeneza mazingira bora ya masoko.

Kilimo kikipata thamani vijana watatulia vijijini na kulima na sio kuja mjini kutandaza sox kwenye lami.
 
Tatizo kila mtu anataka kuwa mfanyabiashara.
Nafikiri ishu si kila mtu kuwa mfanyabiashara; lakini tuweke utaratibu kuwa anayetaka kufanya biashara basi afanye biashara rasmi, asajiliwe kama mlipa kodi, awe na leseni ya biashara na awe na address ya sehemu ya kufanyia hiyo biashara. Maeneo yatengwe kwa ajili ya biashara. Hii si tu itapunguza migogoro lakini itaongeza ufanisi wa ukusanyaji mapato
naunga mkono hoja.
hakuna haja ya kuangalia wapi tulikosea ila kwa sasa hatuna budi kusahihisha ili tuwe taifa la watu wastaarabu wenye kuzingatia kanuni, taratibu na sheria tulizo jiwekea sisi wenyewe.
Ni kweli mkuu bado tuna nafasi ya kurekebisha tulipojikwaa. La msingi siasa ziwekwe pembeni, tufanye maendeleo na tusimamie utekelezwaji wa sheria ili kuwa na taifa la kistaarabu
naunga mkono hoja.
hakuna haja ya kuangalia wapi tulikosea ila kwa sasa hatuna budi kusahihisha ili tuwe taifa la watu wastaarabu wenye kuzingatia kanuni, taratibu na sheria tulizo jiwekea sisi wenyewe
 
Kila uwongozi wa serikali unapoanzia mtaa au kijiji mwenyekiti awe na taarifa ya idadi ya wakazi na kati ya hao wafanya biashara ni wangapi.

Katika mipango ya serikali kujenga vituo vya afya, shule, kituo cha polisi pia kuwe na ujenzi wa soko.
Hakika takwimu ni muhimu sana; hata maeneo ya chini yatanufaika na mfumo rasmi
 
Hata kama kuna ulichosahau ila ulichosema ni sawa sana
Tuko pamoja kiongozi; shida wanasiasa nao wanatuyumbisha hawasimamii mipango thabiti wanataka kumridhisha kila mtu. Mapato mengi yanapotea. Kama tukisimamia urasimishaji wa biashara naamini tutaokoa hata mapato yanayopotea
 
Mama mama mama! hiyo kauli yako ya jana kwamba wapangwe kistaarabu unataka kuwatwisha zigo wakuu wa mikoa na wilaya. Sasa hivi wanaalikana kutoka vijijini ili wachukue mali kwa wenye duka (walipa kodi) waanze kuzisambaza kwa mguu (wakwepe kodi).

Mama mama mama, naomba kufoka nyuma ya tarakishi. Dawa si kuwapanga ila ni kukomesha kabisa biashara ya wamachinga vijana warudi mashambani wakafuge na kulima tupate mali ghafi, tukuze viwanda. Ukiendekeza umachinga basi sahau ukuaji wa viwanda nchini maana utakuwa unakuza viwanda vya nchi zingine.
 
... wamelipia vitambulisho elfu 20 so wamechangia pakubwa uchumi wa nchi kwa mujibu wa sera za chama tawala.
 
Kila uwongozi wa serikali unapoanzia mtaa au kijiji mwenyekiti awe na taarifa ya idadi ya wakazi na kati ya hao wafanya biashara ni wangapi.

Katika mipango ya serikali kujenga vituo vya afya, shule, kituo cha polisi pia kuwe na ujenzi wa soko.
Hata mimi ningekuwa waziri wa biashara ndo kitu ningemuomba Raisi fungu na eneo Kila mtaa nijenge soko kubwa lenye vigezo vyote vya biashara ndogo ndogo na mapato ya soko yakarudi serikalini, machinga tangu zamani zilikuwa huduma ndogo ndogo walizokuwa wanatoa mama wa nyumbani kwa kuuzia nje ya nyumba kurahisisha kupatikana vitu mitaani na wakati nao wanajipatia kipato huku huduma za muhimu kama usafi na choo zikiwepo maana ni nyumbani na Kama ni mchafu watu hawaji kununua kwako, ila kulingana na hizo huduma kuingiliwa mpaka na vijana wenye nguvu Sasa mabadiliko yalitakiwa yafanyike Ili kuondoa hata watu wabaya kwenye jamii Kila mtaa kutengwe eneo kubwa kujengwe soko la kudumu lenye huduma zote na mjini kubaki kusafi na maduka makubwa yenye kulipa kodi na kufanya usafi, ajenda ya mkuu wa wilaya na mkoa iwe Kila mtaa uwe na soko litabeba chinga, shule za watoto wa msingi na secondary, kituo cha afya, kituo cha polisi, ukumbi wa mikutano na hapo hapo uwanja wa michezo na mikutano ya mtaa hapo kwenye soko kubwa la mtaa litaondoa tatizo la biashara hovyo hovyo tunaloita machinga.
 
Kwanza soko litazalisha ajira, kutakua na mhasibu, meneja na wafanyaji usafi.

Soko linaweza kuwa na floor tatu, chini wauza vyakula, katikati nguo, viatu na bidhaa nyingine tatu na juu migahawa.
 
Option ni mmoja tu, kutengeneza sera madhubuti za kilimo zitakazotengeneza mazingira bora ya masoko.

Kilimo kikipata thamani vijana watatulia vijijini na kulima na sio kuja mjini kutandaza sox kwenye lami.
Kulima kupi huko kwa kulimwa na vijana wote? Kulima kisasa hakuhitaji watu wengi ni tools tu za kisasa unatoa mazao mengi kwa mkupuo, kilicholeta machinga wengi nikuruhusiwa wavunje Sheria kwa kuruhusiwa kuuza popote na ndo hicho kikiondolewa na machinga hawataonekana kwenye hizo sehemu zisizokuwa soko, hata huduma zingine zikiruhusiwa kuvunja Sheria kama kujenga hovyo na kulima hata barabarani pia zitafanyika kwa wingi sana maana machinga ni vijana wanaotoka vijijini na hata elimu ya kutafuta kazi hawana ni chinga tu wanawaza hivyo waliporuhusiwa ndo hivyo wamekuja mjini na wao kuishi mjini kuliko kukaa vijijini na wake zao nao hivyo hivyo wapo nao na watoto wanagawana tu bidhaa na maeneo, kinachotakiwa nikila chinga aambiwe arudi mtaani kwake apewe eneo la kuuzia ndo utashangaa familia yote ni chinga kuanzia baba mpaka wajukuu na wote wanataka Kila mtu eneo lake apewe Bure na asilipe kodi Wala ushuru wowote.
 
Tuko pamoja kiongozi; shida wanasiasa nao wanatuyumbisha hawasimamii mipango thabiti wanataka kumridhisha kila mtu. Mapato mengi yanapotea. Kama tukisimamia urasimishaji wa biashara naamini tutaokoa hata mapato yanayopotea
Uongozi mzuri ni maamuzi magumu bila kusitasita.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom