Sakata la Wamachinga: Suluhisho pekee ni Serikali kuhimiza wananchi kufanya biashara rasmi kwa mujibu wa sheria na kusimamia maslahi ya pande zote

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
7,707
2,000
Tatizo la uwepo wa wamachinga sio kukosa maeneo rasmi ya kuuzia bidhaa zao, tatizo ni asili ya biashara ya umachinga.

Biashara ya umachinga inataka kuzurula, kusongamana, holela na kufanyika maeneo ya njia kuu zenye kupitiwa na watu wengi.

Kuna sehemu nyingi kuna masoko mazuri lakini utashangaa wafanyabiashara wengi (wamachinga!) wamejazana nje ya soko na ndani hakuna wauzaji.

Mmachinga ni sawa sawa na kuku wa kienyeji, anaishi vizuri kwa kuachiwa azurure.
 

Mr. MTUI

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
8,136
2,000
Wakuu wa mikoa na wilaya wanaambiwa wawapanhe wamachinga..hv kwa hii Dar wamachinga wapo Zaidi ya milioni mbili watawapanga wapi?
 

Madukwa Peter

JF-Expert Member
Sep 20, 2012
2,524
2,000
Uongozi mzuri ni maamuzi magumu bila kusitasita.
Ni kweli kabisa mkuu; kiongozi mzuri ni yule anayefanya maamuzi magumu yenye tija kwa taifa la kesho. Kuendelea kuwabembeleza machinga kwa sababu za kisiasa ni mwanzo wa kuendelea kudidimkza uchumi. Ni vema yakafanyika maamuzi yatakayoleta tija ya kudumu. Umachinga ni kirusi.
 

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
4,476
2,000
IMG_0536.jpg
 

Madukwa Peter

JF-Expert Member
Sep 20, 2012
2,524
2,000
Vitambulisho vya wamachinga vilishazikwa .
Kitambulisho siyo suluhu ya kudumu; ni suluhu ya muda mfupi.

Haikuwa mbaya lakini bado inaonekana haina tija ya kudumu


Suluhu ya kudumu ni kufanya b8ashara rasmi kwa kuzingatia sheria za kufanya biashara
 

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
1,562
2,000
Salaam;

Hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh Amos Makalla ametoa maagizo ya kuwataka wamachinga waliopanga bidhaa zao barabarani kuondoka mara moja katika maeneo hayo.

Maagizo haya yametokana na mgogoro uliopo kati ya wafanyabishara rasmi waliopanga katika maduka dhidi ya wamachinga wanaopanga bidhaa mbele ya maduka na katika barabara kwa kile kinachoelezwa kuwa wafanyabiashara rasmi kukosa soko huku wakilipa kodi lukuki kulinganisha na wamachinga ambao hulipa 20000 tu kwa mwaka.

Aidha agizo hilo linatokana na ukweli kuwa wamachinga wanaopanga bidhaa barabarani wanaleta usumbufu ktk usafiri kwa sababu barabara zinakuwa hazipitiki kutokana na wao kuzibana barabara kwa kupanga bidhaa ktk barabara.

Kimsingi wafanyabiashara waliopanga ktk maduka wanayo haki ya kulalamika kwa sababu

1. Wanafanya biashara rasmi kwa mujibu wa sheria
2. Wanalipa kodi ya mapato
3. Wanalipia leseni ya biashara
4. Wanalipa gharama ya kodi ya jengo na ushuru wa huduma na gharama zingine kedekede
5. Mauzo yao yanaporomoka na hivyo wanakuwa ktk wakati mgumu na hata kupunguza mapato ambayo serikali ingeweza kukusanya.

Kwa mtizamo wangu kutokana na utata wa jambo hili serikali ichukue hatua zifuatazo

1. Wafanyabiashara rasmi walindwe maslahi yao kwa kuwa wao ndiyo hulipa kodi nyingi kwa serikali na kwamba wanafanya biashara kwa mujibu wa sheria.

2. Wamachinga waondolewe mara moja na kama serikali ina nia ya kuwalinda wamachinga basi wawatengee eneo lao katikati ya mji wawajengee vbanda vyao vidogovidogo wawapangishe na walipe kodi

3. Wakati serikali inaendelea kuwabeba wamachinga iwape muda wa kufanya biashara isiyo rasmi na kuwasisitiza kurasimisha biashara zao na umachinga isichukuliwe kama jambo la kudumu kwa kuwa serikali inapoteza mapato mengi kupitia informal business. (Serikali isimamie sheria na ikibidi hata kwa kulazimisha watu kuhama kutoka ktk machinga kwenda ktk mfumo rasmi wa kibishara)
4. Serikali itenge maeneo kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo na miundombinu ijengwe (inaweza kuwa vibanda vidogovidogo ila vya kisasa na siyo mfumo wa ghorofa kama machinga complex). Katika utekelezaji wa jambo hili serikali ni vema ikashirikisha wadau mbalimbali kabla ya utekelezaji ili kukwepa kufeli kama ilivyofeli machinga complex. Serikali ijenge vibanda hivyo katika maeneo yanayozunguka masoko makubwa kama kariakoo, Tegeta, mbagala, gongolamboto, temeke, kimara, mbezi, ubungo, mwenge n.k. aidha wafanyabiashara wadogo ni lazima wawe na leseni ya biashara na walipe kodi lakini gharama ya kupangisha ktk vibanda vyao angalau iwe nafuu. Hili lisiwe jambo la hiyari; kurasimisha biashara iwe jambo la lazima; asiyeweza kufanya biashara rasmj akatafute shughuli ya kufanya.

5. SERIKALI iboreshe mazingira ya kibiashara mikoani na kuimarisha sekta zingine kama kilimo, uvuvi, madini n.k ili kupunguza kasi ya vijana wanaohamia mjini Dsm na ktk majiji mengine.

FAIDA YA KURASIMISHA BIASHARA

1. Itapunguza mgogoro kati ya wafanyabiashara rasmi na machinga
2. Itarahisisha ukusanyaji mapato
3. Itakuwa rahisi kuwa na takwimu halisi za wafanyabiashara kuanzia ngazi ya kitongoji hadi kitaifa
4. Itakuza uchumi wetu na kuboresha miundombinu
5. Itakuwa ni rahisi kwa serikali kuboresha huduma za kijamii
6. Kuokoa muda katika jiji la Dsm unaotokana na msongamano usio wa lazima
7. Majiji yetu yatakuwa safi na katika mpangilio unaovutia
8. Taasisi za kifedha itakuwa rahisi kuwafikia wafanyabiashara ikiwemo katika mikopo

Nasisitiza kuwa; linapokuja suala la serikali kufanya maamuzi iwalinde zaidi wale wanaofanya biashara rasmi kwa kuwa ndiyo wanaolipa kodi na stahili mbalimbali kwa mujibu wa sheria.

Kwa hiyo naunga mkono suala la serikali kuwaondoa wamachinga kwa namna yoyote ile na kwamba umachinga usichukuliwe kama mfumo rasmi na wa kudumu wa kibiashara ni lazima tubadilike ili serikali ikusanye mapato kwa uhakika na kila mwananchi awajibike kwa nafasi yake.

Kwa ujumla maamuzi yasiegamie ktk maslahi ya kisiasa bali yaegamie ktk maslahi ya kiuchumi ya nchi yetu ili tuweze kuwa na taifa linalojiendesha ktk misingi ya haki na sheria, nidhamu na uwajibikaji.

Tukumbuke kuwa kila mwananchi ajue ana wajibu wa kulipa kodi stahili ili tuweze kujenga nchi yetu.
View attachment 1938702
View attachment 1938703
Kitendo cha wakuu wa mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza kuwavunjia miundo mbinu ya biashara ndogo ndogo na kusababisha baadhi bidhaa zao kuporwa. Serikali imevunja sheria ndogo za wafanyabiashara wadogo ya mwaka 2018 sura 288 na waliohusika kuna siku watawajibika kusababisha hasara hizo.

Mtindo wa kuthamini kupendezesha vitu na kutweza utu na haki za wafanyabiashara wadogo haukubaliki kisheria, kikanuni, kiutaratibu, kiutamaduni, kijamii, kiusalama na kimantiki hivyo wasababishaji wa hasara, usumbufu na uonevu ni sharti wawajibishwe
 

Attachments

 • File size
  454.7 KB
  Views
  2
 • File size
  2.4 MB
  Views
  2

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom