SAKATA LA WALIOGANDA NA TEMEKE CHANZO CHA UVUMI NI Mchungaji John Mzule

R.B

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Messages
6,294
Points
2,000
R.B

R.B

JF-Expert Member
Joined May 10, 2012
6,294 2,000
SAKATA la watu wanaodaiwa ni wanandoa wasaliti kugandana, Temeke, Dar es Salaam limechukua sura mpya baada ya kubainika kuwa, Mchungaji John Mzule wa Kanisa la Gospel Revival Assemblies of God, Mbagala, Dar naye alichangia kuenea kwa uvumi ule, hivyo polisi wanamfuatilia.

Mchungaji John Mzule wa Kanisa la Gospel Revival Assemblies of God, Mbagala.

Mchungaji Mzule ameingia matatani baada ya kudaiwa kuwa, siku ya tukio aliushawishi umma uamini kwamba kuna watu waligandana wakifanya zinaa kwa vile alithibitisha kuwa, aliwaona wazinzi hao wakishushwa kutoka kwenye gari aina ya Canter hospitalini Temeke.
Mchungaji huyo alikuwa akithibitisha hayo katika eneo la hospitali hiyo pale alipohojiwa na mapaparazi hali iliyowafanya watu waliokuwa wakimsikiliza kuamini hivyo na wao wakawapigia simu wenzao kutoka pande mbalimbali za Jiji la Dar es Salaam ambao walifika kwa lengo la kushuhudia.
Katika eneo la tukio, mwandishi wetu alimkuta Mchungaji Mzule akimlaumu mtu aliyesababisha ‘wazinzi’ hao kugandana kwamba, alifanya kosa kubwa sana na anastahili adhabu ya pekee atakapobainika
Kijana aliyetaka kuvuruga amani eneo la hospitali ya Temeke akiwa mikononi mwa polisi.

TUNAMNUKUU: “Kitendo hiki ni cha kinyama sana na aliyesababisha hapaswi kuvumiliwa kwa sababu ni udhalilishaji wa kijinsia.”
Uwazi lililokuwepo hospitalini hapo siku ya tukio, lilishuhudia wananchi wakiwa wamefurika wakitaka kushuhudia watu hao waliogandana licha ya kuambiwa na uongozi wa hospitali kwamba hakukuwa na tukio hilo.
Baadhi ya maafande wa Jeshi la Polisi waliozungumza na waandishi wetu Novemba 9, 2012 walisema mtu aliyevumisha habari hiyo kama akijulikana atachukuliwa hatua za kisheria kwa kosa la kuuadaa umma.

Wananchi wakiwa eneo la hospitali ya Temeke kutaka kuwashuhudia wapenzi wanaodaiwa kugandana wakati wakifanya mapenzi.

“Ni kwamba kama tutampata mchungaji huyo au mtu mwingine anayechangia kueneza uvumi huu ni lazima tutamhoji atueleze kwa nini amezusha,” alisema afisa mmoja wa cheo cha juu wa polisi ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwa kuwa siyo msemaji.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, ACP Angelbert Kiondo alipopigiwa simu siku ya Jumapili ili kusikia kauli yake juu ya tukio hilo, iliita bila kupokelewa.​

Attachments:

Tiba

Tiba

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2008
Messages
4,556
Points
1,250
Tiba

Tiba

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2008
4,556 1,250
Mchungaji alikuwa anaota au?

Tiba
 
J

JF2050

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2010
Messages
2,085
Points
0
Age
108
J

JF2050

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2010
2,085 0
Inasemekana tukio hili lilikuwa ni kweli hata kama polisi wakane.
 
Obe

Obe

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2007
Messages
8,688
Points
2,000
Obe

Obe

JF-Expert Member
Joined Dec 31, 2007
8,688 2,000
Inasemekana tukio hili lilikuwa ni kweli hata kama polisi wakane.
....................., bado hujathibitisha. Hii habari kusambaa kwake kunaonesha namna gani hatuvipi vichwa vyetu kazi yake, kufikiri.
 
J

JF2050

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2010
Messages
2,085
Points
0
Age
108
J

JF2050

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2010
2,085 0
....................., bado hujathibitisha. Hii habari kusambaa kwake kunaonesha namna gani hatuvipi vichwa vyetu kazi yake, kufikiri.
Mkuu sijaandika ili kuthibitisha au kushindana na wewe. Kama watu wengi walikuwa wakihojiwa na wanadai wameona kwa macho yao, sasa unataka wathibitishe vipi? Kama unaamini sio kweli unatakiwa uthibitishe kama vile ukiamini ni kweli.
 
J

JF2050

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2010
Messages
2,085
Points
0
Age
108
J

JF2050

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2010
2,085 0
Obe wewe unataka kuamini ni uzushi kwa sababu polisi kasema, au kwa sababu gani?
 
Obe

Obe

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2007
Messages
8,688
Points
2,000
Obe

Obe

JF-Expert Member
Joined Dec 31, 2007
8,688 2,000
Mkuu Classics! Naelewa kabisa mazingira yanayoshawishi habari ya kugandana kuonekana ya kweli! Binafsi nilitegemea kuwa na habari kamili zaidi ya uzushi tu huku kila mmoja mwenye habari ya TEMEKE akija na maneno yake.

Kwa jinsi ya tukio lenyewe naamini wahusika wangejulikana wanaishi wapi, na majina yao, hii kwangu ingeclick ubongo wangu.
hata hivyo, tupo pamoja sana mdau( na kwa hapa sishabikii kitendo cha kucheat)
 
Mzito Kabwela

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2009
Messages
17,855
Points
2,000
Age
36
Mzito Kabwela

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2009
17,855 2,000
Morinyo kutua Man city
 
Erythrocyte

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Messages
60,027
Points
2,000
Erythrocyte

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2012
60,027 2,000
Tunaomba wanaomfahamu huyo mchungaji watupatie CV yake , iende deep kidogo kujua pia kama ana akili timamu au la , na mtu yoyote humu JF aliyeamini ujinga ule , bila kumung'unya maneno elimu yake ni ndogo sana , hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuamini upumbavu wa aina ile , Naomba kuuliza swali , kuna yeyote humu aliwahi kumuona POPOBAWA ? Rejea utafiti wa CCN ! Shame !
 
Father of All

Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Messages
3,090
Points
1,225
Father of All

Father of All

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2012
3,090 1,225
Hakuna kitu kama hicho bali akili ndogo na imani za kijingaa za kishirikina. Mara hii mmesahau uvumi kuwa mtu aligeuka chatu Buguruni na ukweli ukadhihiri kuwa ulikuwa ujingaa wa kawaida unaoenezwa na wapumbavuuu wanaotaka kuuza magazeti yao ya udaku? Shigongo hawezi kula bila upuuuuuzi kama huu.Ni aibu kuwa na taifa la mataaahira na washirikina kama letu.
 
A

Africa_Spring

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2012
Messages
428
Points
0
A

Africa_Spring

JF-Expert Member
Joined Jun 16, 2012
428 0
Bila ya kudanganya atapataje sadaka
 
M

Magano

Member
Joined
Nov 19, 2012
Messages
18
Points
0
M

Magano

Member
Joined Nov 19, 2012
18 0
Bado hajajitokeza sangoma yeyote?, maana sanaa za namna hii mwisho wake utyakuta kumbe kuna sangoma anatengeneza promo!
 
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Messages
48,074
Points
2,000
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2010
48,074 2,000
Heheheh eti atashtakiwa kwa kuuhadaa umma, makosa mengine bhanaaa....mbona wao walikua ndio walinzi wa amani kule Samunge kwa dokta uchwara!!! wamkamate na Magufuli, Lukuvi na wengineo waliokuwa wakipamba kurasa za mbele za magazeti ili kuhadaa umma kuwa kikombe kinatibu magonjwa sugu
 
nyabhingi

nyabhingi

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Messages
13,658
Points
2,000
nyabhingi

nyabhingi

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2010
13,658 2,000
yani watu wameganda,mmoja kafa lakini hatujui jina wal mahali anapoishi..go tell that to the marines
 
Wile GAMBA

Wile GAMBA

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2011
Messages
1,809
Points
0
Wile GAMBA

Wile GAMBA

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2011
1,809 0
kajua kama ni ukweli au ni uongo haisaidii kitu, kitu cha kujifunza hapa ni mke wa ntu ni sumu, usimfanyie mtu kitu usichotaka kufanyiwa!
 
Wiyelelee

Wiyelelee

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2012
Messages
1,072
Points
1,170
Wiyelelee

Wiyelelee

JF-Expert Member
Joined Nov 9, 2012
1,072 1,170
SAKATA la watu wanaodaiwa ni wanandoa wasaliti kugandana, Temeke, Dar es Salaam limechukua sura mpya baada ya kubainika kuwa, Mchungaji John Mzule wa Kanisa la Gospel Revival Assemblies of God, Mbagala, Dar naye alichangia kuenea kwa uvumi ule, hivyo polisi wanamfuatilia.
Mchungaji John Mzule wa Kanisa la Gospel Revival Assemblies of God, Mbagala.
Mchungaji Mzule ameingia matatani baada ya kudaiwa kuwa, siku ya tukio aliushawishi umma uamini kwamba kuna watu waligandana wakifanya zinaa kwa vile alithibitisha kuwa, aliwaona wazinzi hao wakishushwa kutoka kwenye gari aina ya Canter hospitalini Temeke.
Mchungaji huyo alikuwa akithibitisha hayo katika eneo la hospitali hiyo pale alipohojiwa na mapaparazi hali iliyowafanya watu waliokuwa wakimsikiliza kuamini hivyo na wao wakawapigia simu wenzao kutoka pande mbalimbali za Jiji la Dar es Salaam ambao walifika kwa lengo la kushuhudia.
Katika eneo la tukio, mwandishi wetu alimkuta Mchungaji Mzule akimlaumu mtu aliyesababisha ‘wazinzi' hao kugandana kwamba, alifanya kosa kubwa sana na anastahili adhabu ya pekee atakapobainika

Kijana aliyetaka kuvuruga amani eneo la hospitali ya Temeke akiwa mikononi mwa polisi.

TUNAMNUKUU: "Kitendo hiki ni cha kinyama sana na aliyesababisha hapaswi kuvumiliwa kwa sababu ni udhalilishaji wa kijinsia."
Uwazi lililokuwepo hospitalini hapo siku ya tukio, lilishuhudia wananchi wakiwa wamefurika wakitaka kushuhudia watu hao waliogandana licha ya kuambiwa na uongozi wa hospitali kwamba hakukuwa na tukio hilo.
Baadhi ya maafande wa Jeshi la Polisi waliozungumza na waandishi wetu Novemba 9, 2012 walisema mtu aliyevumisha habari hiyo kama akijulikana atachukuliwa hatua za kisheria kwa kosa la kuuadaa umma.

Wananchi wakiwa eneo la hospitali ya Temeke kutaka kuwashuhudia wapenzi wanaodaiwa kugandana wakati wakifanya mapenzi.

"Ni kwamba kama tutampata mchungaji huyo au mtu mwingine anayechangia kueneza uvumi huu ni lazima tutamhoji atueleze kwa nini amezusha," alisema afisa mmoja wa cheo cha juu wa polisi ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwa kuwa siyo msemaji.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, ACP Angelbert Kiondo alipopigiwa simu siku ya Jumapili ili kusikia kauli yake juu ya tukio hilo, iliita bila kupokelewa.​

Kwenye hiyo nyekundu: Mi naomba mumhukumu mtu huyo kwa jina lake na si kwa jina la Mchungaji kwa vile wakati anaongea hakuvaa nguo zenye kola ambazo ni alama ya kiuchungaji.
 
Forum statistics

Threads 1,295,991
Members 498,495
Posts 31,230,032
Top