Sakata la walimu: Mahakama inaweza kuchagua kuheshimiwa na serikali au jamii! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la walimu: Mahakama inaweza kuchagua kuheshimiwa na serikali au jamii!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nsami, Jul 30, 2012.

 1. n

  nsami Senior Member

  #1
  Jul 30, 2012
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa mara nyingine tena mhimili wa Mahakama unajikuta katika mtihani mwingine dhidi ya serikali na wananchi baada ya serikali kukimbilia mahakamani katika sakata la mgomo wa walimu.

  Masikio ya watanzania wengi yana shauku kubwa ya kusikia kauli ya mahakama juu ya mgomo huu. Huku zikisikika kauli mbalimbali kutoka kwa viongozi wa serikali na bunge zikiashiria kuwa viongozi hawa wanajua tamko la mahakama lijalo! Ni manabii hawa! N/Spika amesema leo bungeni kuwa suala la mgomo wa walimu liko mahakamani na tunasubiri tamko la mahakama na kwenda mbali zaidi kuwa mahakama itatoa tamko lake kesho saa nane mchana! Huku NW Elimu Mh. Mlugo akisisitiza kuwa haitapita siku mbili mahakama haijatoa tamko lake?

  Wakati viongozi wa serikali na bunge wakisema hayo naibu katibu mkuu wa CWT Mwl Oluochi anadai mgomo uko palepale kwa kuwa uko umefuata taratibu zote za kisheria na mahakama haitamtaarifu chochote juu ya tamko lake. Hili ni jambo jingine linalohitaji mjadala mpana. Mhimili wa mahakama una options mbili tu kuhusu reputation yake kutokana na kauli yake juu ya hili.

  1. Mahakama isubiri kuheshimiwa na serikali kwa kuiokoa kudhalilishwa na walimu kama ilivyofanya wiki chache zilizopita kwa madaktari. Ikitaka kupongezwa na serikali tamko ni wazi "WALIMU WARUDI KAZINI MGOMO WAO NI BATILI" na hivyo walimu watarudi mashuleni (sio darasani) na kuacha serikali ikichekelea bila kujali kama wataenda kufundisha au la! bila kujali mahakama imetenda haki au la! Hayo hayaihusu serikali yetu kabisaaaaaa!

  2. Mahakama pia inaweza kusubiri kuheshimiwa na wananchi na jamii kwa ujumla kwa kusimamia haki bila kujali kama swahiba wake serikali yuko upande wa kupoteza au wa kupata. Haki mbele.

  Ni maoni yangu tu asije akanisikia Ramadhani Ighondu wa TISS!

  Nawasilisha.
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  wa MAKOLE
   
 3. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwani c tunaambiwa mahakama imeshatoa tamko/uamuzi imetupilia mbali pingamizi la serikali?
   
 4. M

  MASIKITIKO JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 841
  Likes Received: 203
  Trophy Points: 60
  Aah!Kumbe kurudi mashuleni na kurudi darasani ni vitu viwili tofauti
   
 5. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2012
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hizi za kwetu hapa nazo mnaziita mahakama!!!.
   
 6. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #6
  Jul 31, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndiyo hivyo, naweza kuwa shuleni lakini sipo darasani. Si umeona matokeo ya kdato cha nne miaka miwili iliyopita. Division zero na four ndiyo nyingi. Mgomo umeanza zamani. Sasa tumeamua kuwa tugome rasmi.
   
 7. Mpatanishi

  Mpatanishi JF-Expert Member

  #7
  Jul 31, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  dodoma!
   
Loading...