MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Nimeshangaa sana kuona suala hili linachukuliwa kinyume kabisa na maagizo ya Mh Rais, watendaji hasa wakuu wa mikoa waliopewa jukumu hilo pamoja na wakurugenzi wote wa taasisi na idara mbali mbali za serikali wanalichukulia suala hili kimzaha na kama mchezo tu!
Inakuaje wafanyakazi hewa wanabainika ndani ya idara flani serikali huku maafisa utumishi wanaendelea na kazi zao,Makatibu tawala wanaendelea na kazi zao, wakurugenzi wanaendelea na kazi zao bila wasi wasi! Wakaguzi wa ndani wa sehasabu wa idara za serikali nao wapo tu!Sasa wakati mishahara hewa ilipokua ikilipwa hizo pesa alikua akipokea nani? Mafaili ya wafanyakazi hao hewa yalikua yakitunzwa na nani?
Nashangaa kuona mkuu wa mkoa au mkuu wa wilaya anafurahia kusoma namba kubwa za watumishi hao hewa eti kwa kazi kubwa aliyofanya, Je, baada ya kazi yake ni hatua gani amechukua? Wanaelewa kua kuna wafanyakazi wanaolipwa na halmashauri kwa mapato yao moja kwa moja? Wanaelewa kua hapo ndipo penye tatizo? Mfano unakuta Mkurugenzi anapewa kibali cha kuajiri walinzi 100 katika halmashauri yake lakini anaajiri 40 tu na hao wengine ni hewa kila mwezi wanalipwa mishahara hewa tu! Wakuu wa mikoa wasielekeze nguvu tu kwa watumishi walioko kwenye mfumo rasmi wa ajira wa serikali bali kule halmashauri kuna majipu makubwa maana baada ya mishahara kuanza kupitia hazina moja kwa moja sasa watendaji wengi wanaandaa taarifa za uongo kuidanganya serikali kujitengea pesa nyingi ndani ya halmashauri kwa madai ya kulipa baadhi ya wafanyazi wanaowalipa wao hasa ambao hawapo katika mfumo rasmi wa ajira.
Hili suala linaonekana kuleta ushindani wa kisiasa tu bila lkuchukuliwa kwa uzito wake pengine kuendana na nia njema ya Mh Rais kupambana na upotevu mkubwa wa pesa katika idara na taasisi mbali mbali za serikali.