Akilinjema
JF-Expert Member
- Aug 9, 2016
- 11,433
- 11,747
Amani ya Mwenyezi Mungu aliyeumba Wanadamu wote iwe juu ya kila asomae na kuchangia Mada hii!
Kufuatia sakata la Wachimba visima kutakiwa wajisalimishe na kwenda kulipia tozo husika hali ambayo imeleta taharuki kubwa miongoni mwa jamii kiasi cha Watu kueleza kwa vipi Serikali yenye jukumu la msingi kushindwa kuwapatia huduma muhimu sana ya maji ambayo ndiyo uhai wa mwanadamu Kwa zaidi ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanganyika badala Yake inataka kuwasakama wananchi ambao baada ya kupata shida Kwa miaka mingi ya Kukosa Maji hali iliyopelekea kujiongeza Kwa kuchimba visima vya Maji Kwa matumizi mbalimbali ikiwemo ya majumbani au viwandani n.k?
Taharuki hiyo imepelekea KM Mkumbo kuelezea yafuatayo ;
1. Wenye visima vyenye urefu usiozidi mita 15 hawahusika na malipo
2. Wenye visima visivyozidi urefu mita 15 na visivyokuwa na miundombinu yoyote Kama vile kufungwa pump hawata husika na malipo pia
3; wenye visima vyenye kuzidi zaidi ya mita 15 na walifunga pump hao Ndiyo walosemekana kutakiwa kulipa !
Hoja binafsi :
Kwa kuwa kiwango cha meza ya Maji (water table ) hutofautiana kati ya maeneo flani na mengine je kigezo cha kina cha urefu wa kisima chaweza kuwa na mashiko?
Mwingine akichimba mita 15 hatapata hata tone la Maji hadi achimbe mita 100 ndo atapata Maji Walau kidogo na Kwa urefu huo swala la kufunga pump huwa haliepukiki je alipishwe sababu ya kuishi maeneo ambayo water table iko Chini zaidi ukilinganisha na maeneo mengine?
Ushauri ;
1. Mtu aliyechimba kisima chake Kwa matumizi ya nyumbani/familia alilipishwe kabisa maana Mtu huyu Maji ya Dawasco yangekuwa yapo kwake asingechimba kisima kabisa!
2. Mwenye kisima ambacho hutumika Kwa matumizi ya viwanda/biashara hawa nao wasilipishwe maana wanalipa kodi ya mapato na bila Maji wataweza kufunga kiwanda au biashara husika!
Wanaopaswa kufikiriwa kulipa:
1. Wale walichimba visima exclusively kwaajili ya kuuza Maji Kibiashara na mauzo yao yawe yanazidi shilingi milioni 4 Kwa mwaka hao Walau wanaweza kuchangia kiasi kidogo!
Karibu Kwa majadiliano na michango yenye Tija kwa maendeleo ya Taifa letu!
Alamsiki!