Sakata la wabunge na mawaziri wenye matatizo...mbona hizi wizara hazimo?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la wabunge na mawaziri wenye matatizo...mbona hizi wizara hazimo?!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nderingosha, Apr 21, 2012.

 1. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,546
  Likes Received: 1,327
  Trophy Points: 280
  Nimefatilia mijadala/kelele za wabunge zinazodai baadhi ya mawaziri wenye matatizo watimuliwe upesi kazi……baadhi ya mawaziri hawa ni:waziri wa fedha, waziri wa biashara na naibu wake,waziri wa tamisemi na waziri wa afya. ..Kinachonishangaza ni kutosikia kelele dhidi ya mawaziri wengine wa wizara ambazo zimekuwa zikipigiwa kelele kwa muda mrefu sasa……mfano: wizara ya ulinzi,wizara ya nishati na madini, wizara ya mambo ya ndani na wizara ya mali asili na utalii na hata wizara ya elimu…….Nasema hivi nikikumbuka kuwa wizara ya ulinzi imekumbwa na uzembe mkubwa…..rejea mauaji ya mabomu mbagala na gongo la mboto….na hata ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma…rejea malipo hewa ya askari nje etc etc..lakini leo waziri bado yuko kibaruani na mambo yameshasahaulika….Tukija wizara ya nishati na madini ni hivi majuzi tu iliundiwa tume na kudhihirika kuwa na ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma….refer sakata la Jairo…..na pia wizara hii imekuwa na ubadhirifu mkubwa kwenye TANESCO….IPTL…ununuzi wa mafuta…..umeme wa dharura …dowans saga……etc etc…….nashangaa leo mawaziri wa wizara hii…akina Ngeleja na Malima hawapigiwi kelele……Tukija wizara ya mambo ya ndani……..rejea mauaji ya raia wasio na hatia songea….kauli tata za waziri dhidi ya madai ya Dr.Mwakyembe na hatma ya uchunguzi wa suala lake……mauaji ya Arusha……etc etc…..leo sisikii kelele dhidi ya waziri wa wizara hii……Tukija wizara ya malia asili na utalii……..rejea sakata la vitalu…..wizi wa wanyama pori kule KIA..na hata mtuhumiwa mkuu kutoroka nchini etc etc…..nashangaa leo waziri wa wizara hii hapigiwi kelele…….na mwisho wizara ya elimu….rejea wizi wa hela za mikopo vyuo vikuu…hiki ni kilio cha kila siku lakini waziri anapeta tu……Ukifatilia kwa makini utakuta baraza zima la mawaziri limeoza…….na mbadala hapa ni kuvunja baraza zima tu……kwa kuanza na kumwondoa PM..
  My take: Kwa kuikumbushia mifano hii….bado nabaki kusema kuwa kelele za wabunge…haswa wa CCM ni danganya toto tuliyozoea……yenye lengo la kupoza vilio vya wananchi dhidi ya udhalimu wa serikali…..Itakumbukwa pia kuwa waziri mkuu alionyesha udhaifu mkubwa katika sakata la madaktari…pale alipowadanganya madaktari na umma kuwa atalipeleka swala la madai yao ….ikiwamo mawaziri wa wizara ya afya kwa rais……lakini kilichotokea baadae wote twakijua…………pale huyu huyu PM alipojitokeza hadharani akipinga madai ya madaktari na haswa lile la kutimuliwa mawaziri husika….Kwa maana hii nashangaa eti wabunge wamemtuma Pinda aende kumweleza JK madai yao!!!!!!!!........yaaani Pinda tunayemjua akamwambie nini JK???????......nasikitika kwamba kwa Pinda huyu…haya yatakuwa ni business as usual…..we have had a very painful experience with him already ….so don’t expect anything from him………

  Angalizo
  : Huu ni utawala wa kulindana….utawala wenye kuwalinda wezi na kuwaadhibu wasema ukweli……only time will tell…
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,231
  Trophy Points: 280
  .umesahau wizara ya ardhi.....
   
 3. w

  wikolo JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kwangu mimi wizara ya elimu ni kituko kikubwa. Hili tatizo la watoto kufeli mitihani naliona kama ni zito kuliko hata huo wizi kwani maisha ya baadaye ya watoto hawa yanaharibika. Waziri wa elimu anatakiwa naye aondoke kwa tatizo hili kwani badala ya kupungua linazidi kukua. Hii ina maana limemshinda na sidhani kama ni busara kusubiri hadi pale itakapofikia kwamba watoto zaidi ya 90% wanafeli. Na kwa hili la 90% ya watoto kufeli wala haliko mbali!!
   
Loading...