SAKATA LA VIROBA: Wauzaji wa jumla mawakala wachanganyikiwa

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,059
Wakati kampuni ya Konyagi ikidai kuwa na zaidi ya katoni laki moja za bidha ya konyagi maarufu kama kiroba, wauzaji na mawakala wa bidha hiyo wameiomba serikali ilitizame kwa upya suala hilo kwani linakwenda kuathiri uchumi wa taifa kwani wengi wana mikopo katika mabenki

Na zimelipiwa kodi...tayari vina stika za tra .... Sasa huyu siku akikwepa kodi mtamulaumu kwa unyama unaofanywa na serikali kwa kukirupuka kiasi hiki???
 
Hakuna stica wala nini viondolewe
Akili za kibasheti ndio hizi hizi zinazodumaza uchumi wa nchi....kukurupuka na kutaka sifa.....!!!
Huwezi kuseme viondolewe bila kuwaandaa wauzaji wa jumla na viwanda vyenye stock kubwa ambazo zimelipiwa kodi na kuzalishwa kwa gharama.....
Wakati mwingine muwe mnanyamaza manakoipeleka nchi kwa matamko uchwara mtakuja kujibu mbele za haki....
 
Na zimelipiwa kodi...tayari vina stika za tra .... Sasa huyu siku akikwepa kodi mtamulaumu kwa unyama unaofanywa na serikali kwa kukirupuka kiasi hiki???
Hivi kwa nini tunapenda kutetea uovu, ikiwemo dharau na ukaidi!

Serikali iliagiza kusitisha utengenezaji, uagizaji na utumiaji pombe ya viroba April 2016 na kwamba mwisho uwe Jan 2017, ikaongeza hadi mwishoni mwa Feb 2017. Muda wa kutosha kuacha kutengeneza au kuagiza.

KUTII KWA HIARI, ni ustaarabu
 
Na ilivipa notes viwanda!!?
 
Watanzania hata ukiwapa taarifa uwa hawaamini mpaka jambo litokee...
Hili jambo wazalishaji na wauzaji walikuwa na taarifa sema basi tu walikuwa wanasubiri waje kulalamika
 
Wakati kampuni ya Konyagi ikidai kuwa na zaidi ya katoni laki moja za bidha ya konyagi maarufu kama kiroba, wauzaji na mawakala wa bidha hiyo wameiomba serikali ilitizame kwa upya suala hilo kwani linakwenda kuathiri uchumi wa taifa kwani wengi wana mikopo katika mabenki

viroba vitawatoa hao wenye navyo kwa kiwango cha kutisha watulie tu u

unauza kama vile vipodozi vilivyopigwa marufuku na tfda kwa bei mbaya sana
hii serikali inacheza nikulipe kodi halafu usitishwe jambo ndani ya masaa kwanza inahitajika wawafungulie kesi upuuzi huu haufai
 
Hivi kwa nini tunapenda kutetea uovu, ikiwemo dharau na ukaidi!

Serikali iliagiza kusitisha utengenezaji, uagizaji na utumiaji pombe ya viroba April 2016 na kwamba mwisho uwe Jan 2017, ikaongeza hadi mwishoni mwa Feb 2017. Muda wa kutosha kuacha kutengeneza au kuagiza.

KUTII KWA HIARI, ni ustaarabu
Hivo venye stika vimegongwa na nani? Warudishiwe kodi walizolipia serekalini
 
Ukifuata mtitiriko wa majadiliano, nimekwisha kujibu swali kama lako hilo. Kwa kuwa wanafanya biashara lazima walipe kodi. Kama wameagiza kitu, hata kinyume cha utaratibu, wamelipa ushuru na adhabu zingine kulingana na kosa lako.
 
Katika sakata zina kuna shida mahali, halijakaa kitaalamu
 
Halijakaa kitaalamu vipi!

Wafanya biashara waliambiwa toka Apr, 2016 kwamba ifakapo Jan, 2017, viroba hakuna tena sokoni.

Wakiwa wataalamu wa uzalishaji/uagizaji, ni hakika wanajua soko na mahitaji yake kwa siku, wiki, mwezi hata mwaka.

Na hata mfanyabiashara wa rejareja anajua soko lake linavyoenda.

Kuwa na viroba kwenye maghala yao ni aina moja ya ukaidi au dharau kwa utawala.
 
Back
Top Bottom