Sakata la vigogo kupora viwanja Burka lachukua sura nyingine!

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
199,959
2,000
Mkurugenzi akanusha vigogo kupewa viwanja Arusha

Imeandikwa na John Mhala, Arusha;
Tarehe: 3rd December 2010


MKURUGENZI wa Halmashauri ya Arusha, Wilayani Arumeru, Halifa Hida, ametoa ufafanuzi juu ya malalamiko ya ugawaji wa viwanja vilivyoko eneo la Burk, na kusema kuwa hakuna kigogo yeyote aliyepata kiwanja zaidi ya kimoja kama uvumi ulivyozagaa nje na ndani ya halimashauri hiyo.

Hida aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari, ofisini kwake, kuhusiana na malalamiko hayo yanayoendelea kutolewa juu ya ugawaji wa viwanja hivyo unaodaiwa kuuziwa vigogo wa serikali huku majina ya wakazi wa wilaya hiyo yakikatwa.


Alisema viwanja hivyo vimetolewa kwa mujibu wa sheria na kila aliyepatiwa fomu ya maombi alifuata sheria kama walivyotangaza katika vyombo mbalimbali vya habari.


Aidha aliongeza kuwa malalamiko mengi yanayotolewa na baadhi ya wananchi yamekuwa hayana tija, kwani majina ya watu wanaodaiwa ni vigogo waliomba viwanja hivyo kwa kufuata taratibu zote zinazohitajika.


Aliongeza kuwa uuzwaji wa viwanja hivyo haukuwa na siri ama masharti yoyote

yaliyoonesha kuzuia mtu yoyote asiye mkazi wa eneo hilo kutouziwa kiwanja.

Alisema, katika ugawaji huo hakuna ufisadi uliotumika wala kashfa kama inavyodaiwa na baadhi ya watu kuwa ugawaji wa viwanja hivyo umetawaliwa na ufisadi na kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) inachunguza suala hilo.


Akijibu hoja kwa nini tangazo la viwanja hilo lilitolewa kwa wiki mbili na

lisikatizwe kwa wiki moja mara baada ya kutimia idadi ya watu walioomba kulingana
na idadi ya viwanja hivyo 700, alisema kuwa, sheria hairuhusu.

"Kama umetangaza siku 14 lazima upokee maombi siku 14 hata kama yatakuwa yamevuka malengo, kama jinsi ilivyotokea kwa kupokea maombi ya watu zaidi ya 20,000. "


Alisema hata hivyo watu waliokosa wasikate tamaa, kwani wote watapatiwa viwanja kwa mujibu wa taratibu zitakapokamilikaa za upimaji wa maeneo ya wazi ya Lakilaki na Gomba Estate wilayani humo.


Hida alisema lengo kubwa linalofanya na halmashauri hiyo ni kuhakikisha wanapunguza ujenzi holela kwa kuzungumza na wenye mashamba makubwa ili kuyanunua na kuyagawa kwa wananchi wenye shida ya ardhi.


Malalamiko hayo yamekuja kufuatia wananchi wengi waliomba viwanja hivyo kwa kulipia Sh. 10,000 kwa fomu ya maombi, kukatwa majina yao na majina yaliyorudi kuwa ni ya vigogo wa serikali na wafanyabiashara kutoka mikoa mbalimbali nchini.
 

Jibaba Bonge

JF-Expert Member
May 6, 2008
1,239
1,500
Huyo mkurugenzi ni kibaraka tu wa wakubwa asijifanye kujitetea kwamba walifuata sheria. Ni sheria gani inayafuatwa kwa mfano watu 500 wajaze fomu za kuomba viwanja na let say viwanja viko 50 halafu by chance viwanja vyote 50 viwe vimegawiwa kwa vigogo. asilete za kuleta hapa.

Nina mfano hai kabisa wa hizi halmashauri kufanya madudu pengine kwa kujikomba kwa vigogo. Pale halmashauri ya mji wa Kibaha kuliwahi kutangazwa viwanja mwaka ambapo viwanja vilipimwa kule Mwanalugali na sehemu nyingine za Tumbi. Nilikuwa mmoja wa waliomba Super Low Density. Nadhani vya ukubwa huo vilikuwa kama 17-30 hivi na ninawafahamu wengi 'wasio na majina' (wasio vigogo) walioomba viwanja hawakupata lakini cha ajabu waliopata plots zote walikuwa ni ma-DC, wakuu wa mikoa, ma-RPC, Wabunge, mawaziri, makatibu wakuu wa wizara na wengine wa aina hiyo viwanja vikawa vimeisha!!! Pale kwenye mbao za matangazo kila aliyekuwa anasoma yale majina aliishia kucheka kwa kusikitika! Sheria gani ilifuatwa hapa iliyokuwa inachagua vigogo tu wakati ambapo wote tulifuata utaratibu uliowekwa wa kuomba viwanja?
Sisemi hivi kwa sababu mimi nilikosa lakini hata ninaowafahamu walioomba viwanja hivyo hawakupata kwa sababu hawakuwa vigogo na isitoshe majina ya waliopata yanafahamika. kama harimashauri wanaona siyo kweli hii habari wabandike hapa majina ya waliopata zile super low density wakati ule.
 

Mo-TOWN

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,727
1,250
Huyo mkurugenzi aache unafiki. sio tu kusema hao wakubwa wameomba kwa njia ya kawaida. Natumaini hamaanishi pia kuwa hao vigogo ndio walikuwa wa kwanza kujua habari ya viwanja na kuviomba. Namshauri wakati unaamua kuongea na media asipende kufikiria kuwa yeye ndiye muelewa zaidi ya wengine. Labda nimuulize ni vigezo gani viliwekwa kwa mtu kupata kiwanja? Hao vigogo anaodai wamepata kiwanja kimoja kimoja anaweza kuwataja? Iweje vigogo walio dar ndio wawe na chance kubwa zaidi kupata kuliko wengi ya watu wa kawaida walio Arusha?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom