Sakata la UwT: Mwenyekiti ang'ang'ania 10% mradi wa kuku wa asili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la UwT: Mwenyekiti ang'ang'ania 10% mradi wa kuku wa asili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Nov 28, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,693
  Trophy Points: 280
  Habarini za jioni wana jf;kuna habari za kusikitsha hapa
  lile sakata tulilokuwa tunalijadili kuhusu kutoelewana
  kati ya mwenyekiti wa uwt..mama sopha simba na katibu wake limepata ufumbuzi.....kwa habari zaidi nunua nipashe kesho
  kwa ufupi ni kwamba kuna mradi ulibuniwa na katibu wa uwt.
  Wa kuku wa asili kutoka ubelgiji ulipofika mikononi mwa mwenyekiti wa uwt waziri wetu sophia simba akakataa kusaini toka mwezi february akitaka ten percent....baada ya kuona amekalia plan ya mradi huu inasemekana copy imepelekwa kwa mh rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania kwa msaada zaidi...hivi haya mambo ya ten per yataisha lini.......kwa zaidi soma nipashe.......,
   
 2. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #2
  Nov 28, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,068
  Likes Received: 3,999
  Trophy Points: 280
  ndo bongo hiyo kaka
   
 3. M

  Masatu JF-Expert Member

  #3
  Nov 28, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Dah! hii ni bonge la "breaking news" na hilo gazeti la kesho hapo juu... it goes without saying
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  Nov 28, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Mwenyekiti uozo anakomaa ten percent za akili za wenzake kweli asubiri kisutu tu namuhesabia dakika......
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Nov 28, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,693
  Trophy Points: 280
  Kwa wachaga ningemuita "litondo kabsa"""
  siku hizi wajanja wanakula 25% nini 10% enzi za mkapa na walishasahau
  yeye anangangania 10% kweli anaitaji mirembe ya haraka as soon as possible
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  Nov 28, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  njaa itamuua huyu mama dah ten percent kaona dili kweli hatuna serikali uozo mtupu
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  Nov 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,693
  Trophy Points: 280

  • [*]Ni wa kuku wa asili
   [*] Alikataa kusaini kisa ten per cent
   [*] Ungewakomboa wanawake
   [*] JK apelekewa mchanganuo wake
   [*] Simba: Katibu Mkuu ananichimbachimba

  Na Mwandishi wetu
  29th November 2009  Lile sakata la mvutano kati ya Mwenyekiti wa Taifa wa UWT, Sophia Simba na Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo, Husna Mwilima linazidi kuchipua mambo, ambapo safari hii kinachogombaniwa ni mradi wa kuku wa asili uliopangwa kuanzishwa.

  Habari za uhakika ambazo Nipashe Jumapili imezibaini wiki hii zinadai kuwa zipo tuhuma kuwa Simba, amezuia mradi mkubwa wa ufugaji kuku wa asili kutoka nchini Ubelgiji kwa kuukalia mkataba bila kuusaini.

  Imedaiwa kuwa juhudi za kuletwa kwa mradi huo zimefanywa na Katibu Mkuu wa UWT, Husna Mwilima, kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Liege cha nchini Ubelgiji.

  Maudhui makubwa ya mradi huo endapo utekelezaji wake utaanza, utasaidia kuwapunguzia umaskini wanawake katika umoja huo hasa wenye kipato cha chini na pia kutunisha mfuko wa UWT.

  Katika hali ambayo bado haijafahamika, Simba anadaiwa kuukalia mkataba wa mradi huo tangu Aprili, mwaka huu na hivyo kuukwamisha.

  Habari za uhakika kutoka kwa wadau wa mradi huo ambazo zimelifikia gazeti hili zinadai kuwa, kufuatia kukwama kwa mradi huo, wameamua kumwandikia Rais Jakaya Kikwete, huku wakiambatanisha vielelezo vyote vya na kumweleza jinsi baadhi ya viongozi wake wanavyokwamisha maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.

  "Mwenyekiti wa UWT ameukalia mkataba huo na kukwamisha juhudi zote za kuanzisha mradi huu. Je, ni nini kilichofanya ukaliwe. Ni “ ten per cent” haipo, au kuna jingine," kilihoji chanzo hicho .

  Kiliongeza kuwa "kwa imani kubwa ya mafanikio ya mradi huu wa kujikomboa kwa wanawake wengi wenye kipato cha chini, mimi na wakereketwa wengine wa CCM na Mtanzania mmoja aishiye Ubelgiji tulijitolea muda pamoja na gharama ili kuweza kuona kuwa mradi huu unafanikiwa, lakini hatma yake juhudi hizi zimegonga mwamba."

  "Mradi ulilenga kufuta umaskini kwa kufuata wanawake vijijini, walio tayari kufuga kuku wa asili na kunufaika na mradi huo wa kipekee," kilisema chanzo hicho.

  Alipoulizwa jana kuhusu madai hayo, Simba alisema yeye ni msomi na hawezi kuweka sahihi yake kwenye vitu visivyoeleweka kwani waliotoa wazo la mradi huo hawakuweza kuuelezea mradi huo kwa undani ili ukubalike.

  Alisema mtu aliyewasilisha wazo la mradi huo alipaswa kulishawishi Baraza Kuu la umoja huo ili liukubali mradi lakini alipoitwa alishindwa kufanya hivyo.

  "Mradi ni mzuri sana lakini lazima mhusika ambaye ndiye aliyekutuma kuliuliza swali hili awashawishi wajumbe wa Baraza Kuu kabla ya kuupitisha, halafu yeye ndiye Katibu na masuala ya kusaini mikataba yanamhusu yeye mimi kama mwenyekiti hayo si yangu," alisema.

  "Hayo ni majungu yaani anaanza kunichimba hata kwenye mradi wa kuku jamani? Alihoji kwa huruma, Anasema na kuongeza, “tumeukataa wakati tulimwambia auelezee kwenye Baraza Kuu hakufanya hivyo ina maana alitaka watu wakubaliane naye kwa kitu ambacho hawakijui au...Mimi niliposikia wazo hilo nililiunga mkono maana ni zuri sana litasaidia wanawake kuondokana na umaskini nikashauri watafutwe wanawake wa kuutekeleza sasa niliukataa lini jamani, mimi ninachosema wauelezee watu waujue sio wasaini vitu visivyoeleweka," alisema.

  Wakati huo huo, Simba alimshutumu Katibu Mkuu wake, kuwa anaendeleza malumbano ya kijinga ambayo hayatamsaidia na badala yake yanambomoa.

  Alisema yeye (Sofia Simba) alimwamini sana Mwilima kiasi cha kupendekeza jina lake kwa Rais Jakaya Kikwete ili ateuliwe kushika wadhifa huo lakini amemgeuka na amekuwa akimchimba kila siku.

  "Kabla ya kupeleka jina lake kwa Rais Kikwete nilimwuliza Mwilima nataka kupendekeza jina lako. Are you ready (uko tayari), akasema Ok (sawa) na mimi nikapendekeza akateuliwa, sasa anafanya kazi ya kunichimba chimba hata katika mradi wa kuku? alihoji Simba.

  Alisema kuna mradi mwingine mkubwa wa kuku ambao unatekelezwa na UWT na kwamba utakapoanza huu mwingine utasaidia kuwakwamua wanawake wengi kwenye lindi la umaskini.

  Hata hivyo, juhudi za kumpata Mwilima kupitia simu yake ya mkononi ziligonga mwamba kutokana na kutoipokea licha ya kupigiwa kwa siku mbili mfululizo

  CHANZO;NIPASHE JUMAPILI
   
 8. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,693
  Trophy Points: 280
  HIVI AKIAMBIWA AWAHI MIREMBE ATAKAATAA EMBU SOMA HAPO CHINI
  HAYO NI MAJIBU YA MTU MMOJA

  Alipoulizwa jana kuhusu madai hayo, Simba alisema yeye ni msomi na hawezi kuweka sahihi yake kwenye vitu visivyoeleweka

  HALAFU
  Mradi ni mzuri sana lakini lazima mhusika ambaye ndiye aliyekutuma kuliuliza swali hili awashawishi wajumbe wa Baraza Kuu kabla ya kuupitisha, halafu yeye ndiye Katibu na masuala ya kusaini mikataba yanamhusu yeye mimi kama mwenyekiti hayo si yangu," alisema
   
 9. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #9
  Nov 29, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hii miradi hii!
  IMENIKUMBUSHA MIAKA ILEEEE ya mradi wa VIMAMI ambapo mama zetu walitapeliwa na hawa vigogo wa UWT... ati kuku/vifaranga wanaletwa kutoka ITaly in exchange for mifupa na matunda!( Vifaranga- Matunda- Mifupa!)
  UWT hebu panukeni mawazo...... hakuna miradi zaidi ya kuku?

  HILI SAKATA.... ngoja tusikie zaidi...
   
 10. b

  bnhai JF-Expert Member

  #10
  Nov 29, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Hili gazeti nalo huandika udaku
   
 11. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #11
  Nov 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,693
  Trophy Points: 280
  mkuu mbona waziri simba kakiri upo na ni mradi mzuri ama kiswahili ushakisahaau kabisa .....huo udaku ni upi labda tujulishe udaku nini??yawezekana yupo pamoja
   
 12. b

  bnhai JF-Expert Member

  #12
  Nov 29, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Kwanza angalia wewe ulichoandika na kilichomo kwenye gazeti. Kuna authentic source ya hiyo 10%?
  Angalia title inavyosemeka na ukimsoma Simba anakwambia alihitaji ajiridhishe. Hivi kuwa Mwenyekiti ni kusign kila kilichopo mbele yako?
   
 13. Shakazulu

  Shakazulu JF-Expert Member

  #13
  Nov 29, 2009
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 940
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Hivi kwa akili zako ulitegemea Mwanyekiti Simba aseme kuwa hajaupitisha kwasababu ya 10%?
   
 14. G

  GEOMO Senior Member

  #14
  Nov 29, 2009
  Joined: Jul 11, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Huyu ni mkaidi tu. Mzee John alimshauri kipindi kile akiwa dodoma atumie mda huo pia kupitia milembe ili afanyiwe check up ya kichwa,na akamtaadhalisha sana kuwa atakuwa amefanya kosa kubwa sana asipofanya hivyo lakini wapi mama wala hakujali sasa matokeo yake ndo hayo anajikana kwa kauli zake mwenyewe.
   
 15. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #15
  Nov 29, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hao kuku wa asili watatoka ubelgiji? Kuku wa kibelgiji watakuwaje wa asili bongo? Au ndiyo yale yale ya ule mradi wa shujaa wetu wa kuleta farasi?
  Inawezekana Mwenyekiti ana sababu tosha kuustukia na si hiyo 10% anayoshutumiwa. Pengine hiyo 10% imeahidiwa kwa hao wanaotaka mradi upitishwe bila kufanyiwa SWOT!

  Amandla.......
   
 16. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #16
  Nov 29, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Kuku wa Ubelgiji ataishi kwenye joto la bongo kweli? Something is wrong here. Au mabanda ya kuku yana viyoyozi siku hizi!
   
Loading...