Sakata la Uteuzi wa Majaji: Bunge lawapiga mkwara wanaolizungumzia

Hivi mbona wakati ule swala la Jairo lilipokuwa chini ya kamati ya bunge
sheria hii haikutumika?After all hakuna tunachojadili kuhusu hili manake
kila kitu kiko wazi.
 
Tutalijadili mpaka watakaposafisha huo uozo kwenye MAHAKAMA zetu tunazozitegemea kutoa haki kwa raia wote...na kuthibitisha hilo waje umu JAMVINI waone tunavyoendelea kulichambua kwa kasi ya ajabu tena wametuchochea tuzame zaidi kutafuta madudu ya mahakama...kwa taarifa yao MAJAJI waadilifu na wanasheria wenye maadili wanafurahia na wanaunga mkono HOJA YA LISSU.
 
"if you don't know where your coming from, you will don't know where your going''

sasa ni wazi bunge limejipa hadhi ya mahakama, someni habari ifuatayo


veronica kazimoto, maelezo

kamati ya haki, maadili na madaraka ya bunge imetoa tamko la kuwataka watendaji wa serikali, mahakama, vyombo vya habari na taasisi nyingine zote kuacha kuzungumzia suala la uteuzi wa majaji wa mahakama kuu kama lilivyowasilishwa bungeni wakati wa mjadala wa bajeti ya wizara ya katiba na sheria kwa mwaka wa fedha 2012/13.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, mwenyekiti wa kamati hiyo, brigedia jenerali mstaafu hassan ngwilizi (mb), amesema suala hilo liko mbele ya kamati ya haki, maadili na madaraka ya bunge ambayo inaendelea na uchunguzi hivyo haitarajiwi taasisi nyingine, nje ya bunge kulizungumzia suala hili kwa kuwa linajadiliwa.

“kamati imeamua kutoa tamko hili kwa madhumuni ya kuhakikisha kuwa uvunjifu wa kanuni na taratibu tulizojiwekea kwa mujibu wa katiba na sheria nyingine za nchi kutoendelea kuvunjwa,” amesema ngwilizi.

Ngwilizi amenukuu ibara ya 100 ya katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania, inayosema kuwa kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika jamhuri ya muungano wa tanzania, au katika mahakama au mahali penginepo nje ya bunge.

“uhuru wa utaratibu unaohifadhiwa na ibara hiyo ya katiba umelipa bunge mamlaka ya kujiwekea utaratibu wa kushughulikia masuala yake katika kanuni za kudumu za bunge zilizotungwa chini ya ibara ya 89 (1) ya katiba”, amesisitiza ngwilizi.

Kutolewa kwa tamko hilo na kamati ya haki, maadili na madaraka ya bunge, kunatokana na mwongozo ulioombwa na gosbert blandes (mb) wakati wa hotuba ya msemaji wa kambi ya upinzani kwa wizara ya katiba na sheria,tundu lissu mbunge wa singida mashariki.

Katika maelezo yake, blandes alinukuu ukurasa wa 9 aya ya 2 katika hotuba hiyo iliyosomeka kuwa watu wanateuliwa kuwa majaji wa mahakama kuu ambao hawajawahi kupendekezwa na tume ya utumishi wa mahakama.

Aya hiyo iliendelea kusema kuwa inaelekea watu hao hupewa ujaji kama zawadi ili kuwawezesha kupata mafao ya majaji wastaafu ambayo yameboreshwa na matokeo yake ni kuwa na majaji ambao wamechoka na hawawezi au hawajui namna ya kufanya kazi ya jaji wa mahakama kuu.

my take: Ni wazi bunge sasa linataka kujifanya ni mahakama kwa kuwafumba watu midomo
 
sina hakika sana kama yuko sahihi kutoa tamko kama hili, kwanza kwa sababu swala la kuteuliwa kwa majaji si la kibunge na ndio maana bunge haliteui majaji.... so sioni mantiki ya kuzuia swala hili kuzungumziwa. hapa mimi ninaona ni katika mchakato wa kuziba mianya ya ukweli kuzungumziwa kwani ninaamini kuwa kamati hii imejikita katika kutaka kuisafisha serikali juu ya uteuzi wa majaji.... viongozi wanaotoa matamko ya namana hii wamejawa na uoga, na wanaogopa hukumu ya ukweli n.k.
 
do we have freedom of experession in tz?

yes...... But..... Not on matters that are either in the court of law or mjengoni. And the list of restrictions is growing! The solution should be the new katiba.
 
Kanuni za bunge kamwe hakiwezi kukinzana na katiba.

Wananchi wana uhuru wa kuwa na maoni na keleza fikra zao.

Mmeyataka wenyewe kwa kutaka kumziba mdono Mh. Tundu Lissu madhara yake ndo hayo yanawarudia.
 
yes...... But..... Not on matters that are either in the court of law or mjengoni. And the list of restrictions is growing! The solution should be the new katiba.

Mosha, can you enlighten us, Where do you get those restrictions
 
Hizi kanuni za Bunge nadhani wanazitumia vibaya sasa, imekuwa kama nchi ya kiimla

Namuona kwa mbali Hassan Ngwilizi akijaribu kufuata nyayo za Eliakim Simpasa. Manake nakumbuka enzi zake(Simpasa) alipokuwa mwenyekiti wa hiyo kamati ya bunge ya maadili, haki na madaraka ya bunge alitaka kuligeuza bunge kuwa juu ya mihimili mingine yote na kutaka kulifanya bunge kichaka cha kuficha madhaifu ya serikali na wabunge wake.

Leo hii hakuna mtu yeyote anayemkumbuka Simpasa pamoja na mbwembwe zake zote, kwahiyo Ngwilizi naye tutamsahau muda si mrefu na hii ngoma anayotaka kuchezesha watu asijekujikuta anaicheza mwenyewe.
 
Hizi ndio aina ya sheria ambazo Tume ya Nyalali ilipendekeza zifutwe/zibadilishwe KABLA hatujaingia ktk mfumo wa vyama vingi. Ziko nyingi tu ila hawa magamba huwa wanachagua na kuzibadili baadhi ya sheria chache mno kati ya hizo.

Lakini hawa watawala hawajui kwamba tunaweza kuamua kwa ujumla wetu KUTOKUTII sheria zilizopo ili kudai mabadiliko na haki zetu
 
Too late. We already know almost everything we need to know about this issue. Na maelezo ya Mh. Lissu nimeshayahifadhi kwa kumbukumbu ya vizazi vijavyo.
 
Hebu tusome vifungu vifuatavyo kwa pamoja.

18 (1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.

18 (2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu ya jamii. (tafsiri yangu - Elimu ya mtu anayetafsiri sheria na kutoa haki ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi)

29 (5) Ili watu wote waweze kufaidi haki na uhuru vilivyotajwa na Katiba hii kila mtu ana wajibu wa kutenda na kuendesha shughuli zake kwa namna ambayo haitangilia haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma. (tafsiri yangu -kujua sifa/uwezo wa jaji lina maslahi kwa umma, hivyo Ngwilizi na kamati yake wanaingilia jambo lenye maslahi ya umma)


Haya, tuje kwenye kifungu alichotumia Ngwilizi.

100 (1) Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika Mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.

My take:

Ngwilizi ameegemea kifungu hichi cha 100(1) ambacho kinahusu 'parlimentary priveleges' (Madaraka na na Haki za Bunge). Hiki kifungu ndicho kinachowapa wabunge kinga dhidi ya jambo lolote wanaloongea bungeni ili wasishtakiwe na ndio maana mbunge anaweza kumjata mtu kama anaamini anavunja sheria. Watanzania 44million sio wabunge, sasa wanahusika vipi na haki za bunge?

Kwa sababu anazojua yeye Ngwilizi amenyofoa kile anachotaka yeye ili kulazimisha watu wakae kimya na hivyo anakuwa amevunja katiba kwa kuondoa uhuru wa raia. (ref 18(1), 18(2) & 29(5))

Lakini jambo ambalo ni very 'new' kwa historia ya Tanzania, ni hatua ya mhimili mmoja (Bunge) kunyamazisha mhimili mwingine (Mahakama). Sijui Ngwilizi ametumia kifungu gani kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano kutoa hilo katazo? Hapa anatakiwa afafanue.
 
Naona Ngwilizi ametutisha na baadhi yetu tumetishika.
Tafsiri ya sheria hiyo inazuia jambo lolote linalojadiliwa na mamlaka moja yenye uwezo wa kutoa maamuzi kisheria ama kikatiba, kujadiliwa pia na mamlaka nyingine yenye/zenye uwezo wa kutoa maamuzi kisheria ama kikatiba. Hii inalenga kuondokana na uwezekano wa jambo moja kupata hukumu mbili.

Sasa kama nyinyi mnajadili katiba mpya kwenye kongamano lililoitishwa na jukwaa la katiba, ambalo halina mamlaka kisheria kuyakusanya NA KUYATUMIA KWENYE UANDIKAJI WA KATIBA MPYA, mnaathiri vipi kazi za Jaji Joseph Sinde.

Au mnataka kuniambia huwa hamuiongelei katiba mpya bila uwepo wa mkuu wa wilaya na tume ya akina Baregu!!!!
 
Mosha, can you enlighten us, Where do you get those restrictions

Every where! If it is not from Mwema then it comes from Ngwilizi or Makinda. Everybody is busy issuing restrictions.At the end of the day we will be allowed to do nothing!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom