Sakata la Uteuzi wa Majaji: Bunge lawapiga mkwara wanaolizungumzia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la Uteuzi wa Majaji: Bunge lawapiga mkwara wanaolizungumzia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana Mpotevu, Sep 21, 2012.

 1. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #1
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Sasa ni wazi Bunge limejipa hadhi ya mahakama, Someni habari ifuatayo


  Veronica Kazimoto, MAELEZO

  Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imetoa tamko la kuwataka watendaji wa Serikali, Mahakama, vyombo vya habari na taasisi nyingine zote kuacha kuzungumzia suala la Uteuzi wa Majaji wa mahakama kuu kama lilivyowasilishwa Bungeni wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha 2012/13.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Brigedia Jenerali Mstaafu Hassan Ngwilizi (Mb), amesema suala hilo liko mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ambayo inaendelea na uchunguzi hivyo haitarajiwi taasisi nyingine, nje ya Bunge kulizungumzia suala hili kwa kuwa linajadiliwa.

  “Kamati imeamua kutoa tamko hili kwa madhumuni ya kuhakikisha kuwa uvunjifu wa kanuni na taratibu tulizojiwekea kwa mujibu wa Katiba na Sheria nyingine za nchi kutoendelea kuvunjwa,” amesema Ngwilizi.

  Ngwilizi amenukuu Ibara ya 100 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayosema kuwa kutakuwa na Uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu Katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, au katika mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.

  “Uhuru wa utaratibu unaohifadhiwa na ibara hiyo ya Katiba umelipa Bunge mamlaka ya kujiwekea utaratibu wa kushughulikia masuala yake katika Kanuni za Kudumu za Bunge zilizotungwa chini ya Ibara ya 89 (1) ya Katiba”, amesisitiza Ngwilizi.

  Kutolewa kwa tamko hilo na kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, kunatokana na mwongozo ulioombwa na Gosbert Blandes (Mb) wakati wa Hotuba ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani kwa Wizara ya Katiba na Sheria,Tundu Lissu Mbunge wa Singida Mashariki.

  Katika maelezo yake, Blandes alinukuu ukurasa wa 9 aya ya 2 katika hotuba hiyo iliyosomeka kuwa watu wanateuliwa kuwa majaji wa mahakama Kuu ambao hawajawahi kupendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama.

  Aya hiyo iliendelea kusema kuwa inaelekea watu hao hupewa ujaji kama zawadi ili kuwawezesha kupata mafao ya majaji wastaafu ambayo yameboreshwa na matokeo yake ni kuwa na majaji ambao wamechoka na hawawezi au hawajui namna ya kufanya kazi ya jaji wa mahakama kuu.

  MY TAKE: Ni wazi BUNGE sasa linataka kujifanya ni mahakama kwa kuwafumba watu midomo
   
 2. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #2
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Hizi kanuni za Bunge nadhani wanazitumia vibaya sasa, imekuwa kama nchi ya kiimla
   
 3. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,377
  Likes Received: 8,535
  Trophy Points: 280
  Kamati ya Haki na Maendeleo ya Bunge inetangaza kuwa ni marufuku ama kwa vyombo vya habari, taasisi yoyote ile au mtu mmoja mmoja kuzungumzia au kujadili swala la majaji Makanjanja walio ripotiwa na Mh Mbunge Tundu Lissu kuwa uteuzi wao umevunja sheria na sasa kama taasisi ndio wenye mamlaka ya kushughurikia ukweli wa jambo hilo na si vinginevyo na atakaye kiuka sheria na hatua kali itachukuliwa dhidi yake....

  Hizi marufuku kwanini huwa zinakuja kwa vitu vyenye ukweli na utata hasa kwenye maslai ya watu flani na si taifa?

  Olimboka, Said Kubenea, madaktari, mauwaji ya raia nk jaribu kufikiria kunani hapo?????
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Nimeona live Itv tangazo hilo la kidicteta likitangazwa na mtu mwenye sura ya Hassan Ngwilizi.
  Ni nzuri sana maana wanaweka bold kwenye ukweli...!
   
 5. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #5
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Acha tabia ya kuleta habari nusu nusu.
   
 6. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Too late! Tumeshajadili hadi tumeelewa. Tumeshajua ukweli na tumetosheka. Kilichobaki ni kutumia kura zetu vizuri!
   
 7. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Do we have freedom of experession in TZ?
   
 8. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,377
  Likes Received: 8,535
  Trophy Points: 280
  Una matatizo ya akili
   
 9. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,828
  Trophy Points: 280
  Hopeless, Bunge halina mamlaka ya kumkataza mtu kusema. ni mahakama tu yenye uwezo huo. Hii mijitu imelewa ebunge!
   
 10. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #10
  Sep 21, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Ndo tunajadili hapa
   
 11. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #11
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Hofu yao, aibu ya kwao. Wao kila afanyalo President ni kupiga makofi tu! Makosa ya uteuzi wa majaji yamewekwa wazi, na kumbu kumbu ziko serekalini huko huko! Ya nini kubwabwaja? Waache watz wahoji yanayotendeka nchini kwao.
   
 12. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #12
  Sep 21, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Wafungie mitandao.kila kitu wanaweka vizuizi.Hizi sio zile enzi za zidumu fikra za mwenyekiti.
   
 13. t

  thatha JF-Expert Member

  #13
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Hilo zuio binafsi sina tatizo nalo, maana tukiachwa tuendelee kulijadili bila kikomo kama ambavyo tayari tumefanya hatutafikia hitimisho lolote. Bila chombo/taasisi yenye mamlaka ishughulikie jambo hili ili mwisho mwema na wenye manufaa kwa watanzania uweze kufikiwa. Tumeshaongea na kuandika mengi sana kuhusu jambo hili lakini nani katujibu au japo kutusikiliza hivyo ni vema sasa lishughulikiwe kikamilifu na vyombo husika nasi tusubiri majibu mwafaka.
   
 14. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #14
  Sep 21, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,105
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  Sisi tutaendelea kuzungumza. Hizo kanuni za bunge zinawahusu wao ndo maana hazipo hadharani ili nasi tuzisome. Hili suala lilishazungumzi siku nyingi kabla hata lisu hajawa mbunge. Lisu alipata tu uwanja wa kulizungumzia vizuri na wao kwa ulimbukeni wakaanza kuomba ushahidi kumbe wanamvua nguo bwana wao wanayemtumikia. Bahati mbaya jamaa mwenyewe yuko uchi toka siku nyingi lakini bado anadunda na kengele zake hadharani
   
 15. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #15
  Sep 21, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,105
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  Sisi tutaendelea kuzungumza. Hizo kanuni za bunge zinawahusu wao ndo maana hazipo hadharani ili nasi tuzisome. Hili suala lilishazungumzi siku nyingi kabla hata lisu hajawa mbunge.

  Lissu alipata tu uwanja wa kulizungumzia vizuri na wao kwa ulimbukeni wakaanza kuomba ushahidi kumbe wanamvua nguo bwana wao wanayemtumikia. Bahati mbaya jamaa mwenyewe yuko uchi toka siku nyingi lakini bado anadunda na kengele zake hadharani
  .
   
 16. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #16
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,743
  Likes Received: 1,806
  Trophy Points: 280
  SERIKALI yoyote inayo karibia mwisho wake huwa hivi. kila aliyekabidhiwa jukumu kidogo tu anataka atembee juu ya vichwa vya waajiri wake.hilo tutalipinga milele tena ashindwe kabisaa.
   
 17. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #17
  Sep 21, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Tutaendelea kujadili utumbo wao kila kukicha hata kama wakija kijiweni kwetu maada ni zilezile, kwani freedom of expression uko wapi?
   
 18. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #18
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,743
  Likes Received: 1,806
  Trophy Points: 280
  Huyu Ngwilizi kweli kachoka! ananikumbusha konda aliyekuwa usingizini akakurupuka kumwambia kaka yake anayefungua NET ili alale akamwambia hakuna kuingia wanafunzi wametosha akidhani ile ni daladala.

  Na huyu nae kakurupuka kutukataza waajiri wake tusizungumzie makanjanja wa mahakama kwa sheria ipi? kweli siku ya kufa Nyani miti yote huteleza na hizi ni dalili tosha kuwa 2015 CCM kwtshney.
   
 19. ng'wanankamba

  ng'wanankamba JF-Expert Member

  #19
  Sep 21, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 341
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Tunakoelekea, itafika mahali hakuna tutachokuwa tunakijadili kama taifa, kila utakachogusa utaambiwa hurusiwi kukiongelea kwa amri ya mahakama au bunge, baadaye itakuwa kwa amri ya Ikulu, amri ya polisi, amri ya jeshi n.k. Mungu tunusuru waja wako.
   
 20. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #20
  Sep 21, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  watawala watu wabaya sana,maana wao wakikaa kwenye mamlaka wanakuja na kanuni kedekede za ukandamizaj,lakin wakitaka nyadhifa wanakuja na kanuni nyiiingi na ibara kibao za kuwasaidia wananchi
   
Loading...