Sakata la ununuzi wa S-400: Uturuki kuwekewa vikwazo

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
May 27, 2016
5,416
7,828
Habari!

Mpango uliofikiriwa muda mrefu wa kuiwekea vikwazo nchi ya Uturuki juu ya hatua ya nchi hiyo kununua mfumo wa ulinzi wa anga wa S-400 kutoka nchini Urusi umeripotiwa kukamilika.

Kulingana na vyanzo mbalimbali wakiwemo maafisa kutoka nchini Marekani wameweka bayana kukamilika kwa mpango huo na muda wowote kuanzia sasa utatekelezwa ambapo Rais wa Marekani Donald Trump ametilia saini mapendekezo ya hatua zilizopendekezwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Ndugu Mike Pompeo.

Sakata hili limechukua sura mpya huku Uturuki ikiendelea kusisitiza msimamo wake kuhusu ununuzi wa mfumo huo. Moja ya madai ya Ankara ni kushindwa kwa nchi washirika ikiwemo Marekani kuipatia nchi hiyo mfumo mbadala wa ulinzi wa anga kuendana na masharti yanayokubalika na Uturuki ambaye ni mwanachama wa muda mrefu wa ushirika wa NATO.

Uamuzi wa Ankara kununua mfumo wa S-400 kutoka Urusi unamaanisha kuwa, nchi hiyo imewekwa kando katika mpango wa F-35 wa Marekani na nchi washirika, uamuzi ambao unaikosesha Uturuki ndege za mashambulizi za kizazi cha tano za F-35 zipatazo 100 ambazo Uturuki ilipanga kuzinunua kupitia kampuni inayozalisha ndege hizo, Lockheed Martin ya nchini Marekani.

Sababu kuu ya kuondolewa kwa Uturuki katika mpango wa F-35 ni kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni hatari za kiusalama endapo mfumo huo wa S-400 utatumika kukusanya taarifa za kiintelijensia zihusuzo ndege za F-35 zikiwemo mbinu mbalimbali zinazowezesha ndege hizo kutotambulika na rada, kwa lugha nyingine, stealth capabilities.

Nini kitajiri na ni kina nani kulengwa na vikwazo hivyo? Yote hayo tutapata kuyafahamu kadri muda utakavyoturuhusu kuyafahamu!

Pia pitia mada hii:
 
Uturuki atasanda, hapo bado Biden hajaapishwa. Yaani watajua kua hawajui.
Biden ata activate CAATSA, Yaani huyo sultan uchwara ataelewa Shoo maamae
 
Uturuki atasanda, hapo bado Biden hajaapishwa. Yaani watajua kua hawajui.
Biden ata activate CAATSA, Yaani huyo sultan uchwara ataelewa Shoo maamae
Sababu ya kuwawekea vikwazo ni ipi?
1: usalama(S-400 ina athiri vipi usalama wa USA na NATO kwa ujumla).
2: biashara(protectionism)
 
Uturuki atasanda, hapo bado Biden hajaapishwa. Yaani watajua kua hawajui.
Biden ata activate CAATSA, Yaani huyo sultan uchwara ataelewa Shoo maamae
Wabongo mnapenda ushabiki kweli,mmarekani hawezi kuanzisha vita na turkey.Geography ya Turkey inaipa advantage ya kipekee(angalia ramani ya dunia).Mashariki kapakana na nchi za kiarabu,Magharibi ulaya mashariki,kusini kisiwa cha cyprus(cyprus wana share na Turkey) na ugiriki.Kaskazini kuna black sea na Russia,sasa kwa akili yako unafikili m russia anaweza ku ruhusu mmarekani aanzishe vita mlangoni kweka!?. Unakumbuka nini kilitokea Crimea!?.
 
Back
Top Bottom