Sakata la Umeme Nchini: Dr. Rashid Alikuwa Sahihi na kamati ya Bunge Ilikosea

Naona swala la kwanza la Tanesco wamechukua hatua gani limeshajibiwa. Sasa swali langu la pili la serikali imechukua hatua gani linahitaji kujibiwa maana niliuliza maswali matatu huko siku za nyuma.

Jibu la swali lako ni kuwa kamati ya Bunge iliridhika na namna serikali ilivyotumia fedha katika kufuatilia suala hilo.
 
Tatizo la watz na serikali yenu, hamfikiri kwa vichwa vyenu, wachache wanaofanya hivyo wanaonekana hawajuwi kitu, hawajasoma au vp. Kama tatizo lilionekana mapema kwa nini busara isingelitumika na mitambo ile ya Dowans ikafanya kazi kunusuru hali. Wakati shirika likijuwa nini kitatokea watz wengi wamebaki kufata kelele za wanasiasa wenye maslahi yao binafsi pembeni, sasa hao wapiga zogo waliotaka mitambo ile isinunuliwe wao wanakaa gizani kama akina "pangupakavu?" au huo waliotaka mitambo ile isinunuliwe kwa visingizio visivyokidhi maslahi ya wananchi kwa tatizo lililotarajiwa kutokea, wapo wapi na huo umeme wao wa "upepo" kuwaokoa watz na giza?
Yupo wapi spika Sitta na wenzake walioona kasoro za kununuliwa mitambo ile bila ya wao kutoa pendekezo la maana la kutatuwa hali ya dharura iliyopo, je wao wanakaa gizani kama akina "fanyakukuche kitanda kinaumiza?"
Watanzania, wakati unakupiteni kutegemea viongozi wabovu wa CCM wakuamulieni kila kitu bila ya ridhaa yenu, mlipaswa hata mufanye kura ya maoni kuamua kama mkubali mitambo ya Dowans isinunuliwe na kuwa tayari kukaa gizani...hata mwaka mzima au masharti ya sheria yalegezwe na mitambo inunuliwe kukidhi hali ya dharura kama ilivyopendekezwa na wataalamu. Badala yake mumewaachia wanasisa "maslahi" kuamua kwa faida ya matumbo yao na hasara kwenu. poleni sana kwa giza.


Te he he! Waambie!
 
Ngekewa,
Mkuu kazi yote hii tunayoifanya hapa ni kuunyesha Umma kwamba tuna viongozi wabovu.. bahati mbaya wapo watu wanaofikiria tofauti na kibaya zaidi ni pale baadhi ya wajumbe wetu kwa upande wa Upinzani tuna kina Zitto na Lipumba wanaafiki upumbavu huu ati kwa maslahi ya Taifa.. sijui kama wanaelewa haswa maana ya maslahi!
 
Hii ni lawama ya Serikali na Rashid full stop. Yaani wamekuja bungeni na plan A peke yake na walipoambiwa STOP basi wakazila ili waje waseme "Si tulisema?". Kaulizwa swali na waandishi wa habari, Dr. Mzima kashindwa kajibu.

Kama kununua mitambo mipya mchakato unachukua mwaka mmoja, kwa nini hawakuliomba BUNGE libadili sheria hata kwa muda ama ruhusa ya Special case kununua mitambo moja kwa moja kutoka kwa watengenezaji na watengenezaji watoe Bima ya mitambo hiyo? Hivi Rais kweli alishindwa kusaidia kutangaza kuwa "inabidi avunje sheria kwa sababu hili swala ni kama vita na ni kwa ajili ya usalama wa Taifa". Ujenzi wa majengo ungelifanywa within 3-4 months na wakati huo, Wahandisi wangelikuwa USA/German kusomea na baadaye kuileta hiyo mitambo mipya. Tungeliazima dege la Mrusi na kwa kipindi cha mwezi mmoja, mitambo ingelikuwa inafanya kazi.

Walipoona Azimio la Arusha linawakera na kuwazibia, walilipiga panga siku moja na wakalizika. Walipotaka pesa BoT kwa ajili ya uchaguzi, walitengeneza EPA na kuchota. Wakaja tena kuzibeba kwa kutumia Deepgreen, Meremeta etc. Walipotaka kuanzisha kampuni ya Richmond, walipindisha kila sheria hadi ikawepo. Hawa watu kama kweli wangelikuwa na NIA ya kuleta mitambo mipya na si kununua mitambo ya Dowans, basi amini usiamini, ingelikuwa sasa hivi inafanya kazi.

Inabidi mwakani tuchague Rais atakayeahidi kumaliza shida ya umeme na maji Tanzania. Kama akishindwa basi mnamuweka pembeni. Akimaliza mnamchagua kwa ngwe ya pili. Akiahidi mambo kibao, mhhhhh. Nawapenda USA ambao waliahidiwa na mgombea kuwa "wakimchagua basi kila chungu jikoni kitakuwa na kuku......... na kweli aliwajaza mikuku..."

Wakulaumiwa ni wanasiasa "maslahi" kina Sitta na kundi lake.
Hivyo vitisho vyote vilivyotolewa na wababe hao hukuvishuhudia hata kuwapaka lawama Serikali na Tanesco?
Hivyo kwa akili yako hiyo mitambo iliyokwishakula fedha za Watanzania ni haki ya nani kama si Watanzania waliotowa Fedha zao?
Tulikuwa na haki ya kuitumia mitambo hiyo hata kama kwa kuitaifisha, sasa wapi hao wababe wwako walitowa ushauri utakaowezesha Watanzania wafaidi kile ambacho walitapeliwa? Au hadi sasa wanasemaje ? Tunachotaka ni umeme na wala sio siasa kwani hata wao tuliwachaguwa ili watuletee maendeleo na sio kuturudisha nyuma kiasi hiki. Wababe hawa wanastahilki kuwajibishwa kama walivyofanywa walwe wa Richmond.
 
Ha ha ha ha! wewe naona sasa umeshakuwa ni kichekesho. Unajitahidi kadri ya uwezo wako kutaka kumtetea huyu fisadi Idrissa Rashid ambaye alistahili kufukuzwa kazi siku nyingi zlizopita kwa kushindwa kazi pale TANESCO na pia kustahili kuchunguzwa kwa kuhusika kwake na ufisadi wa rada, lakini badi umekazana tu na juhudi zako sijui umeahidiwa nini na papa fisadi Rostam ikiwa mitambo yake ya kifisadi ya Richmond itanunuliwa na TANESCO. Juhudi zako haziwezi kufika mahali popote huyu fisadi Idissa Rashid na yeyote yule anayetetea ununuzi wa mitambo ya kifisadi ya RA wamechemsha sana na Watanzania tumeshaamka kutoruhusu manununuzi yoyote yale ambayo yana harufu kali ya kifisadi. Endelea na juhudi zako za kumtetea fisadi Idrissa Rashid, lakini ujue kamwe hazitafanikiwa.

Hivi kweli Babu unataka kunieleza kuwa huoni seriousness ys hili tatizo kwa nchi na mawazo yako yote yameishia kwa Rostam? Huyu Rostam atawalipa watu wangapi? Loo kazi bado ipo kwa wa TZ na Iddi Simba yuko right.
 
Wakulaumiwa ni wanasiasa "maslahi" kina Sitta na kundi lake.
Hivyo vitisho vyote vilivyotolewa na wababe hao hukuvishuhudia hata kuwapaka lawama Serikali na Tanesco?
Hivyo kwa akili yako hiyo mitambo iliyokwishakula fedha za Watanzania ni haki ya nani kama si Watanzania waliotowa Fedha zao?
Tulikuwa na haki ya kuitumia mitambo hiyo hata kama kwa kuitaifisha, sasa wapi hao wababe wwako walitowa ushauri utakaowezesha Watanzania wafaidi kile ambacho walitapeliwa? Au hadi sasa wanasemaje ? Tunachotaka ni umeme na wala sio siasa kwani hata wao tuliwachaguwa ili watuletee maendeleo na sio kuturudisha nyuma kiasi hiki. Wababe hawa wanastahilki kuwajibishwa kama walivyofanywa walwe wa Richmond.
Wanacho taka mafisadi ni kuinunua hiyo mitambo na sio kuitaifisha kama wewe unavyosema, ukitaka suala la kutaifisha, huna budi ufuate mchachato wa akina Sitta yaani wafuate maazimio ya Bunge waliofanya makosa wadhibiwe, watoe report ya kweli ya kiasi nchi ilizopoteza kwenye huu mkataba, aliyekuwa anachukua pesa tanesco ajulikane, ndio litafuata suala la kutaifisha kinyume cha hapo itakuwa hadithi za abunuwasi.
 
Totally nonsense, rubbish... wewe unawatetea mafisadi tu,,, huna lolote

Labda mwenzangu huelewi maana ya extract. Hayo maneno si yangu ni ya wale waliyoyasema wakiwemo hao hao unao watetea. Lete hoja ndugu.
 
Junius,
Mkuu wangu usimsome Kasheshe kufikia maamuzi pasipo wewe kufikiria kwa kichwa chako undani wa tatizo hili la Umeme.
Kwanza kabisa hapa nanukuu maneno ya Malima alivyosema.
Hata hivyo, baada ya shellukindo kusema kwamba sakata la Dowans limekwisha zikwa, Naibu waziri wa Nishati na Madini, Adama Malima aliyekuwepo katika mkutano huo aliongeza kuwa, serikali haina mpango tena wa kununua mitambo hiyo ya kufufua umeme ya Dowans, lakini endapo mtu binafsi atainunua na kuiuzia Tanesco umeme kwa sheria ya sasa itakubali.

Hapo ujuu katika maandishi menkundu inaonyesha wazi kwamba serikali yetu imeshapania kuuza mitambo hiyo kwa Tanesco. Wanaposema endapo mtu binafsi akinunua mitambo hiyo anaweza kuiuzia Tanesco Umemem ina maana gani?.. Dowans ni shrika binafsi ikiwa na maana kuna mtu binafsi aliyeinunua hiyo mitambo toka Richmond na wote hawa walitakiwa kuiuzia Tanesco Umeme..Sasa kilichoshindikana ni kipi toka mwanzo! - kwa sababu ya Ufisadi... na pili Dowans ingechukua tender kinyumwe cha sheria pasipo kutangazwa tender huru kwa wawekezaji..Leo tunapitisha sheria ya kununua mitambo hiyo hiyo chini ya maamuzi ambayo ni pinzani na sheria yetu ya manunuzi...Licha ya yote hayo tumeona shirika kama Songos wakiuponda mtambo huo kuwa ni mtumba, haifai ni chavu...leo nchi nzima tunashindwa ktk maamuzi na shirika moja dogo ambalo tumeliajiri sisi wenyewe!

Mkuu hakuna asiyejua kwamba mitambo hiyo ni mali ya MTANDAO, hii ndio fact! hao kina Lowassa na Rostam kwa hiyo jina la mtu binafsi yoyote linaweza kuwekwa kama mnunuzi na tukarudi ktk makosa yale yaliyofanyika toka mwanzo..Rostam akinunua mtambo huo wa Dowans hawezi kuandika jina lake ila atazua jina jingine la kampuni. Je, mmeshasahau kwamba ni serikali hiyo hiyo hadi leo imekataa katakata kututajia nani mwenye kumiliki shirika hilo tena walidiriki hata kusema HAWAJUI mwenye kumiliki shirika hilo, iweje leo tukanunue mitambo toka shirika ambalo viongozi wetu hawafahamu mwenyewe..Hii inaingia akilini kweli?

Pili, nakumbuka vizuri kuwa kamati ya madini na Nishati kwa maneno yake Zitto mwenyewe alisema malengo ya Tanesco kununua mitambo ile ni kuiwezesha Tanesco kuwa na mitambo yake yeynyewe badala ya kukodisha jambo ambalo limetugharimu sana kwa kipiundi kifupi toka mashirika binafsi, leo hii tunarudi ktk janga lile lile. Hivi kweli mtu unaweza pindisha sheria tukanunua mali ya wizi kwa sababu mwizi ni binadamu sio mali iliyoibiwa!

Mkuu wangu ikiwa mitambo hii ina mashaka ya Ufisadi na wahusika wake ni Rostam na Lowassa basi seriikali wala shirika haliwezi kununua mitambo hiyo hadi janga la Richmond limepatiwa ufumbuzi. Mitambo ya Dowans ni ushahidi wa kesi ya Richmond ambayo kisheria inatakiwa kuwa confiscated na mashtaka kufunguliwa mahakamani lakini tunapouza ushahidi huu ni mbinu mojawapo ya kupoteza ushahidi.

Tatu,
tatizo la Umeme kwa maelezo ya Shelukindo ni tatizo ambalo LIPO toka Kikwete anaingia madarakani yalikuwepo na ktk kiwango hicho hicho.. Tuliambiwa maelezo yote alozungumza Shelukindo, hakuna jipya na wanachi tulivaa vibwebwe pamoja na ahadi ya mvua za kisayansi na kufua umeme wa makaa ya mawe, kuboresha mabwawa yetu na mengine mengi ambayo rais mwenyewe aliwaahidi wananchi kabla hata hajakaa Ikulu..Loe hii ni miaka MINNE hakuna jipya!

Na sote tunaelewa kwamba Tender ya Richmond, Watsila na mashirika mengine zilikubaliwa kama ni tatizo lka dharura ambalo lilitakiwa haraka iwezekanavyo kwa wakati ule...Ilichukua mwaka mzima kwa Richmond kufikisha mitambo yao na haraka sana tuligundua Ubabaishaji wao na tukawasimamisha.. Toka Richmond wasimamishwe ni miaka MITATU mingine imepita wakati Tanesco na serikali wakijua kwamba hizo MW 100 ni muhimu sana iweje walishindwa muda wote huo kufidia hjizo Mw 100, ila wakazanie kununua mitambo hiyo tu kwa miaka yote mitatu?.. Hivi kweli tulishindwa kuagiza mitambo mingine au hata kuwapa hiyo Tender Watsila au shirika jingine ambalo linawauzia umeme Tanesco kwa uhalali isipokuwa Dowans pekee!..

Mkuu it's been FOUR Yrs toka tuna matatizo ya umeme kwa jiji la Dar pekee na miaka zaidi ya 20 kwa mikoa ambayo imetajwa kuwa na shida ya umeme wa dharura. Ni miaka 40 kwa nchi nzima tukiondoa wakati wa mkoloni iweje leo somo kubwa la ununuzi wa mitambo ya Dowans tena Mw100 iwe makosa makubwa ya serikali ambayo imehsindwa kuanzisha vyanzo vipya vya umeme toka mwalimu Nyerere atoke madarakani.

Hadi leo hii tunategemea vyanzo vya mwalimu Nyerere ambaye alivijenga ktk wakati mgumu sana, wakati ambao serikali iligharamia kila matumizi ya huduma za wizara na taasisi zake, leo tunashindwa kabisa kujenga vyanzo vipya wakati serikali inavuta kodi pasipo matumizi makubwa lakini wepesi kuzungumzia Dowans ambayo inaingia kinyume cha sheria.


Sawa iwapo unataka lazima tukubali kuwa Kikwete mwenyewe anahusika na hili tatizo la umeme lakini ningeomba nizungumzie mambo machache ambayo hukuyatilia maanani wakati ukilenga hizo lawama zako.
Kwanza hili tatizo la umeme kwa Tanzania halikuanza katika kipindi cha Kikwete bali limekuwepo kwa muda mrefu lakini kwa wakati huo hatukuwa na uhuru wa kusema kama wakati huu wa Kikwete. Msingi wa umeme wa Tanzania ni maji ambayo ni matokeo ya maumbile yaliyo nje ya Kikwete au mwengine yeyote. Ni miaka minne tu tangu Kikwete achukuwe madaraka na ilichukua chini ya mwaka mmoja kukabiliwa na tatizo la umeme, suala jee ni mchakato gani endelevu uliowekwa na hao waliomtangulia Kikwete?
Pili, si tulikwishajuwa kuwa mitambo ya Dowans ililetwa kitapeli, sasa wasiwasi wwetu ulikuwa wapi iwapo tulikwishadanganywa huko nyuma lakini sasa tungeingia katika mchakato wa kuangalia faida ya mitambo hiyo huku tukijiepusha na kudanganywa tena? Labda lengo letu lilikuwa kuona kuwa ile mitambo haitunufaishi sisi na badala yake kumtia adamu mmiliki wake? Nafikiri wakati wa kujitowa muhanga kijingajinga kama huku umeshapitwa kwani ile mitambo tulikwishaigharamia na ingekuwa jambo la busara kuitumia baada ya kuhakikisha kuwa hakuna udanganyifu mwengine.
Tatu nafikiri umeshafika wakati kwa Watanzania kupokea maonyo na ushauri kutoka kwa anaeonya kwani Wabunge wetu walikuwaq wakali kuonya lakini wakakaidi hata shauri za wataalamu na wala hawakutoa mapendekezo ya kuepusha hali hii na badala yake sasa ni kutafutana uchawi.
 
Tutajadili sana hapa JF, lakini source ya matatizo yote haya ni ufisadi, kundi la mafisadi wamemweka Idrisa hapa Tanesco ili kulinda na kutetea ufisadi wao naye kwa kutokuwa na uzalendo na kulewa hela chafu alichokuwa anafikiria ni deal lake la Dowans tu. Baada ya kupigwa chini ndio anashangashangaa tu hapo Tanesco na hakuna la maana alilofanya.


Waswahili husema 'mnyoge mnyongeni na haki yake mpeni' Hivyo Bunge tukufu lina watu wangapi? wanapi maprofesa? na wangapi wataalamu wa fani mbali mbali? Hivyo huyu Rashidi mmoja baada ya Watanzania kungamuwa kuwa kawekwa na mafisadi ameweza kuwashinda akili wabunge wote kwa kutowa pendekezo ambalo kutotekelezwa kwake kumetokea yale aliyoyatabiri?
Ni ufinyu wa akili zetu zilizolemazwa na masilaha ya kisiasa uliotufikisha hapa na kumlaumu Rashid ni kupungukiwa na hoja. Kwani si alikwishatuonya iwapo ni fisadi au ni shujaa si issue, issue ni jitihada na mawazo gani yalifanywa kucounter huo ufisadi wa Rashid.

Nionavyo mimi kilichokuwa muhimu kwa Wakubwa wetu wakiwemo wabunge walikichukulia hatuwa muafaka kukipata, si hatuoni maboresho ya maslahi yao?
 
Ana makosa mengi tu.

Kwanza unaanzia pesa alizozipata kwenye manunuzi ya RADA.

Sasa tuje kwenye hili la umeme: Siku moja nikibadili chanel, nikapita MTV na kukuta Rusell Simons akimtukana kijana aliyedesign nguo na kuzipa mpangilio mbaya. Sijui yalianzia wapi ila niliona Rusell akimtukana, na baadaye akazirukia hizo nguo zilizokuwa chini na kuzikanyagakanyaga na baada ya kurusha matusi kadhaa, akaTEMEA mate na kuondoka.

Amini usiamini kama Kikwete angelikuwa ni Putin, basi Rashid angelipewa maneno yake LIVE mbele za watu na kutukanwa. Kinachofuata ni kuwa au UKIMBIE kazi au uje na kitu kinachoeleweka. Baada ya Rashid kukataliwa kununua mitambo mibovu na mchakato wa kununua mitambo mipya ni mrefu, je alikuja na plan yoyote ya KUWALAZIMISHA wabunge wabadili sheria au hata kuomba kibali MAALUMU kwa BUNGE na RAIS ili kununua mitambo "moja kwa moja" kwa watengenezaji? Hivi Tanesco si waliambiwa na akina Lukindo wanunue mitambo mipya? Sasa walikuwa wanatangaza tena tender ya nini? Wangelipeleka Wahandisi USA/German na kwenda kuchukua offer za makampuni na wakaja nazo. Au hata Mabalozi wangelienda na kuchukua offer na kuzituma Tz. Kwa kipindi kifupi, Wahandisi wa Tanesco, serikali, Bunge na washauri wa Rais wangelikutana na kuchagua wapi inunuliwe. Wanaita Waandishi wa habari wa Upinzani na kusema "inabidi tufanye hivi ili kuokoa nchi kwenye giza". Amini usiamini, wangelishangiliwa kama mashujaa.

Rashid na U-dr wake alipokataliwa Dowans, akaona "niliwaambia, sasa ngoja muone cha mtema kuni....." Ingelikuwa nchi za wakorofi, si tu kuwa anafukuzwa kazi ila anahukumiwa kama Mhujumu uchumi.

Nafikiri una bifu hapo! Kwanini hatuzungumzii giza tulilonalo na tunarukia mengine? Kila jambo kina wakati wake la tutatengeneza mseto usoeleweka.
 
No mkuu wangu,Viongozi ni reflection yetu kwa sababu viongozi wanataka kununua mitambo ya Dowans by all means necessary na wewe na wengine wengi wenu mnataka pia kununua mitambo chakavu kwa sababu zisizokuwa na maana kabisa!..MNAFANANA kimawazo!

Hivi kweli tukinunua mitambo ya Dowans tatizo litakwisha?.. HAPANA! mbona nawe unafikiri kama viongozi wetu mkuu wangu!..

Hatujanunua hiyo mitambo kama unavyoshauri wewe mwenye akili timilifu, jee huo mgao haupo?
Pengine ungenunuliwa huo mgao usingekuwepo.
Halafu siasi tulionafikira unazozibeza hizo ndio fikira zetu sasa zenu na kina shelukindo ni zipi ilikututowa kwenye tatizo?
 
Bob,
Yaani inashangaza sana mkuu.............watu hawaoni wala hawakumbuki............. Hii kitu Dowans naona watu wamelogwa nayo.................tulishasema hapa Mafisadi walifanya na wataendelea kushirikiana kwa makusudi ili tuingie gizani................

.........kuna mtu eti kasema Richmond ni ilikuja kwa sababu ya ubovu wa procurement procedures zetu............sijui huyu mtu kama alisoma maelezo ya kamati ya Bunge kuhusu mchakato ulivyokuwa..........yaani watu wankumbatia ufisadi hivi hivi unaona...............inaudhi sana kwa kweli
 
Nyie wote mnaofikiri kununua mitambo ya DOWANS ni kumaliza tatizo la umeme Tanzania, nasema hivi:

"Nyie ni sawa na Mwanamke/Gigolo au SHOGA anayefuatwa na mteja ili atoe huduma ya mapenzi bila Condom huku akijua kabisa jamaa ana UKIMWI".
Ukiulizwa unasema "heri nife kesho kutwa na ukimwi, kuliko kufa kesho na njaa".

Kibaya zaidi ni kuwa, ulifahamu kuwa pesa na unga ndani vinaisha na wewe ukakaa bwerere kwa kisingizio kuwa "ilikuwa uende kwa jirani kumtoa mwali" na hivyo ukawa umechoka kwenda kazini.......

Wewe unaefikiria kuwa utapata umeme kwa maneno matupu ni sawa sawa na mwanamume goigoi usieamuwa kuowa ati utatekegemea kutoka kwa wa wenzako utakufa na haja zako. Ujanadume ni kujitowa muhanga na kukabili vikwazo.

Eti tusinunue mitambo na huku hatuna uwezo wala utaalamu wa kupata mitambo mengine na bado tunawategemea wale wale tukiowakatalia ushauri wao ni kichekesho cha mwaka. Tanesco na Rashid kama tuliwaona kuwa wanatupeleka siko basi tunge kuwa agressive katika ktutowa ushauri na mapendekezo na sio kupogozwa shuka na kungojea mke wa jirani apite.
 
Ha ha ha ha! wewe naona sasa umeshakuwa ni kichekesho. Unajitahidi kadri ya uwezo wako kutaka kumtetea huyu fisadi Idrissa Rashid ambaye alistahili kufukuzwa kazi siku nyingi zlizopita kwa kushindwa kazi pale TANESCO na pia kustahili kuchunguzwa kwa kuhusika kwake na ufisadi wa rada, lakini badi umekazana tu na juhudi zako sijui umeahidiwa nini na papa fisadi Rostam ikiwa mitambo yake ya kifisadi ya Richmond itanunuliwa na TANESCO. Juhudi zako haziwezi kufika mahali popote huyu fisadi Idissa Rashid na yeyote yule anayetetea ununuzi wa mitambo ya kifisadi ya RA wamechemsha sana na Watanzania tumeshaamka kutoruhusu manununuzi yoyote yale ambayo yana harufu kali ya kifisadi. Endelea na juhudi zako za kumtetea fisadi Idrissa Rashid, lakini ujue kamwe hazitafanikiwa.

Mkuu mbona unashuka hadhi kiasi hiki? Hivyo hoja hapa ni Rashid peke yake? Kwa hadhi yako sikutegemea kuwa utakuwa rahisi hivi. Kama Rashidi alikuwa ana tuhuma au la haitusaidii sana kwa hili tatizo kwani Rashidi ni mtu mmoja na kutowa nguvu zako zote kumlega yeye bila kutupa ushauri wa kutoka katika janga hili utakuwa hutusaidii kitu.
Unataka tuamini kuwa hili suala ni la one man show/ Mkuu tunategemea busara zako katika kututowa katika kiza na sio chuki binafsi.
 
.....wewe bado unaishi kwenye ujima,nenda kawadanganye wale mnaowahonga pilau na madebe ya pombe na usisahau kwa sababu zisizozuilika na kwa usalama wa Taifa!

Haya tumeyazowea! Pasipo hoja basi huko ndiko mnakotupeleka. Aibu lakini.
 
Kwa nini emergency plan isiwe kwenye kununua mitambo HARAKA kwa kuruka hizo sheria za PRRA? Si wangeliambiwa Wabunge, Rais na PM kuwa inabidi TUVUNJE sheria kwa serikali YENYEWE kwenda kununua mitambo na wenye mitambo kutoa guarantee na si kusubiri TENDA? Tenda ingelikuwa ni kwa wenye mitambo moja kwa moja na kazi ifanywe na watengeneza mitambo na wahandisi wa Tanesco. Kuna mtu angelalamika kuvunja sheria? Kama wangelitaka, amini sasa hivi mitambo mipya ingelikuwepo.

Haya ni matokeo ya LAITI!
 
Habari ndiyo hiyo. Dowans ni kama bwana/bibi mwenye ukimwi. Halafu mtu anakuja anasema nenda kampakate/kapakatwe na huyo jamaa mwenye ukimwi na tena pekupeku. Hii Raha ya siku moja, itatupa matatizo mengine mengi zaidi mbele. Mwanakijiji alishatuandikia hapa kuwa hiyo mitambo ilinunua na pesa za Bank. Sasa wenye bank wakija kudai mitambo yao na wakati huo sisi tumenunua, MTASEMA nini?

Naona sababu zinapunguwa kutoka ufisadi na kuwa ukimwi na mali ya Benki , sijui hiyo Benki ni ya Obama?
 
Hata watu wale majani, ndege ya rais itanunuliwa!

Hata watu wale mchanga, rada mpya itanunuliwa!

Leo inakuaje watu wanakubali kuwasha vibatari ili mitambo mipya inunuliwe lakini serikali haiko tayari kununua mitambo mipya ila ya DOWANS ndio ya kununua?

Nani ni mtendaji mkuu wa Tanesco? Naona kila mtu anashauri tu!

Dr. Iddrissa anashauri, Kamati ya bunge wanashauri, sasa nani ni mtendaji hapa Tanesco? Kuna haja gani ya kuwa na DG kama hawezi kuwajibika?

Kama wizara ndio wanawajibika, Ondoa cheo cha DG acha wataalamu wamshauri waziri na katibu mkuu.

Kuwa gizani sio sababu ya kununua Dowans. NO WAY!

Angalau una msimamo iwapo si mtumiaji wa koroboi kama mimi.
 
Ngekewa,
Mkuu kazi yote hii tunayoifanya hapa ni kuunyesha Umma kwamba tuna viongozi wabovu.. bahati mbaya wapo watu wanaofikiria tofauti na kibaya zaidi ni pale baadhi ya wajumbe wetu kwa upande wa Upinzani tuna kina Zitto na Lipumba wanaafiki upumbavu huu ati kwa maslahi ya Taifa.. sijui kama wanaelewa haswa maana ya maslahi!

Sasa iwapo nyie mnachukuwa wajibu wa kuelimisha wananchi waingie kizani na mnahisi mna haki kwanini mnawaona kina Zitto hawana haki ya kuwatakia wananchi umeme? Lengo langu ni kuwa tuwe na hoja katika mawanzo yetu na sio kushabikia eti jambo limefanywa na watu fulani tunaowapenda au kuwachukia.
 
Wanacho taka mafisadi ni kuinunua hiyo mitambo na sio kuitaifisha kama wewe unavyosema, ukitaka suala la kutaifisha, huna budi ufuate mchachato wa akina Sitta yaani wafuate maazimio ya Bunge waliofanya makosa wadhibiwe, watoe report ya kweli ya kiasi nchi ilizopoteza kwenye huu mkataba, aliyekuwa anachukua pesa tanesco ajulikane, ndio litafuata suala la kutaifisha kinyume cha hapo itakuwa hadithi za abunuwasi.

Na hilo linashindikana vipi wakati"mna" ushahidi wa hayo mnayoyaeleza?
Iko wapi hiyo good will ya kina Sitta iwapo wana ushahidi lakini wananyamaza na kuipeleka nchi kwenye kiza?
Uambiwapo lazima nawe ujiambie au utawala bora uko wapi?
 
Back
Top Bottom