Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,550
- 6,062
Akina Zitto waliyaona haya tukawaita majina sijui fisadi kijana nk. Leo watu tunakosa uthubutu walau wa kusema samahani tulisokea na wenzetu walikuwa sahihi. Na kwa mjadala unavyokwenda hapa nakumbuka maneno ya FMES " Viongozi wetu ni reflection ya sisi wenyewe" ndio maana bado tunadai "mkosaji" ni Idris na Tanesco yake! hivi hili nalo ni
Mkuu Masatu,
Mpaka wanaleta ombi la kununua mitambo ya Dowans, hakuna aliyekosa. Hayo yalikuwa maoni yao. Ila ilipokataliwa wakabweteka. Hapa WAKOSAJI ni wote. Idis kwa kutokutafuta PLAN B. Wabunge kwa kutokutafuta jinsi ya kurahisisha ununuzi wa mitambo mipya, Rais kwa kutoinglia kati swala linaloweza kuharibu uchumi wa taifa, Waziri kwa kutokumshauri Rais ........ Tanesco kama Tanesco hawana ubavu. Wamebanwa kama mjusi kwenye mlango na macho yamewatoka. Wanaangalia tu jinsi Mafahali wawili wanavyogombania KULA na mmoja akitaka kuzuia na mwisho inakuja kukomoana. Kama ingelikuwa wakati wa uchaguzi, ingelikuwa safi sana. Mwendo huu huu hadi mwakani..... watu waje wabebe misalaba yao wenyewe.