Sakata la Umeme Nchini: Dr. Rashid Alikuwa Sahihi na kamati ya Bunge Ilikosea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la Umeme Nchini: Dr. Rashid Alikuwa Sahihi na kamati ya Bunge Ilikosea

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by tk, Oct 13, 2009.

 1. t

  tk JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Katika hali isiyokuwa ya kawaida Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, ambayo huko nyuma ilikuwa mbogo katika masuala ya utendaji wa Tanesco, jana ilikuwa kama kondoo wakati ikipokea taarifa za Serikali kuhusu hali halisi ya uzalishaji wa umeme nchini.

  Extracts kutoka gazeti la Tanzania Daima la jumanne Tarehe 13 Oktoba 2009 "Siri Yafichuka Umeme Tatizo Sugu :

  Extract 1

  "Kikao cha pamoja kati ya Serikali, Shirika la Ugavi (Tanesco), na Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, kimebaini kwamba ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la mgawo wa umeme nchini utapatikana baada ya muda mrefu.

  Ukweli huo mchungu kuhusu mgawo wa nishati hiyo unaoweza kuendelea kulikabili taifa mara kwa mara ulibainishwa jana wakati pande hizo tatu zilipozungumza na wanahabari muda mfupi baada ya kikao chao."

  Extract 2

  "Akizungumza katika mkutano huo wa pamoja, Mwenyekiti wa Kamati ya nishati na Madini ya Bunge, William Shellukindo (CCM) alikiri kwamba, uchunguzi uliofanywa na wajumbe watatu wa kamati hiyo waliotembelea mabwawa ya kuzalisha umeme ya Kihansi, Hale na Pangani umebainisha kwamba, mgao huo haujasababishwa kwa namna yeyote na vitendo vya hujuma."

  Extract 3

  "Pamoja na kukiri kwamba, kikao chao kilibaini kuwa, tatizo la umeme litaendelea kulisumbua taifa kwa kipindi kirefu zaidi, Shellukindo alisema suala la kuitaka serikali kununua mitambo ya Dowans halikuwa sehemu za ajenda walizozijadili.

  Hata hivyo, baada ya shellukindo kusema kwamba sakata la Dowans limekwisha zikwa, Naibu waziri wa Nishati na Madini, Adama Malima aliyekuwepo katika mkutano huo aliongeza kuwa, serikali haina mpango tena wa kununua mitambo hiyo ya kufufua umeme ya Dowans, lakini endapo mtu binafsi atainunua na kuiuzia Tanesco umeme kwa sheria ya sasa itakubali.

  Katika hilo, Malima alisema kwa sheria ya sasa, Tanesco ina uwezo wa kununua umeme kutoka katika makampuni na taasisi binafsi ili iweze kukidhi mahitaji yake ya kuhakikisha kuwa nishati hiyo inakuwepo wakati wote nchini."

  Extract 4

  "Kwa upande wake, akizungumzia sababu sababu zilizolifikisha taifa hapa lilipo sasa, Shellukindo alibainisha kuwa, mgawo wa sasa unatokana na upungufu wa megawati 72 ambao kamati yake iliridhika na sababu za kitaalamu kutoka serikalini na Tanesco."

  Extract 5

  "(Shellukindo) aliishauri serikali kupitia Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2004, kuona namna ya kuondoa urasimu uliopo ili usiathiri manunuzi ya mitambo miwili itakayozalisha umeme wa jumla ya megawati 160, katika miji ya Dar es Salaam na Mwanza.

  Wakati Shellukindo akitoa rai hiyo, kumbukumbu zinaonyesha kuwa, miongoni mwa sababu ambazo zilisababisha Bunge kuitia msukosuko serikali, wakati wa sakata la Richmond mwaka jana ni uamuzi wake wa kuamua kutumia utaratibu uliokuwa ukijaribu kukwepa ukiritimba wa sheria ya manunuzi."

  Extract 6

  "Katika hali ambayo haikutarajiwa katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk idris Rashid, alishindwa kujibu maswali ya waandishi wa habari waliomtaka kutoa ufafanuzi wa kauli zake alozitowa machi mwaka huu kuwa serikali isiponunua mitambo ya Dowans, nchi nitaingia gizanimwishoni mwa mwaka na wananchi wasimlaumu kwa hilo.

  Baada ya kuulizwa swali hilo, Dk. rashid alisita kujibu na kunyamaza kimya, hatua aliyowafanyawaandishi kumshinikiza kuelezea suala hilo.

  Hata hivyo, Naibu Waziri Malima aliingilia kati kwa kujibu kuwa alifanya utabiri wa nyota ulioegemea katika utaalamu wa kisayansi na ambao matokeo yake yamethibitisha kwamba alikuwa sahihi.

  "Mkurugenzi alituandikia mwezi Februari mwaka huu akitoa mapendekezo ya kitaalamu kuwa serikalini tusipochukua hatua za haraka, nchi inaweza kuingia gizani mwishoni mwa mwaka kutokana na uwezekano wa kutokea ukame na tumeona" alisema Malima."

  Alisema wazi kuwa wataalamu wa masual ya umemewaliliona tatizo hili mapemana kutoa ushauri wao wa kitaalamu, hivyo serikali ilipaswa kuzingatia.


  Extract 7

  "Mapema mwaka huu, dhamira ya serikali kupitia Tanesco kutaka kununua mitambo ya Dowans, iliibua mjadala mkali miongoni mwa watanzania, huku wakionyesha shaka kuhusu ununuzi huo."
   
 2. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kila kitu kipo hapo!!!
   
 3. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hivi Waziri wa nisahti (Bw Ngeleja) hilii si moja ya jukumu lake muhimu? Mbona haonekani kutoa ufafunuzi wa tatizoo hili sugu???

  Je bado anastahili kuwa waziri kamili katika wizara hiii??

  Je Bw Malima ameonyesha kuwa na uajsiri wa kufafanua jambo hili toka mapema na kwa kujiamini kama ilivyoonyeshwaa hapoo juu akimsaidia Dr Idrisa maelezo yake, si wakati wa serikali ya Jk kumkabidhii jukumu kamili la wizara hiyoooo??

  Nawakilishaaa
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,795
  Trophy Points: 280
  Nahisi kama watu walioko katika wizara hii na Tamesco hawana uwezo wa kumudu kasi ya mahitaji ya nishati ndani ya nchi.Hatuhitaji semina zisizo isha juu ya kukosa umeme. Tunataka solutions za kuongeza utengenezaji wa umeme ambazo zitakuwa implemented haraka iwezekanavyo
   
 5. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2009
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kamati ya Bunge haiwezi kulaumiwa; yenyewe ilichokataa ni kununuliwa na serikali mitambo ya dowans ambayo tayari ni mizee kwani sheria ya manunuzi itaka serikali inunue mitambo mipya.
  Naweza kuwalaumu tanesco kwani sheria ya manunuzi wanaijua, na kama walishaona kuwapo kwa ukame, walitakiwa kuagiza mitambo mipya kabisa siyo kung'ang'ania mizee ya dowans.
  Kama waliona kuwepo kwa ukame, na wanajua sheria haiwaruhusu kununua mitambo ya zamani, na bado wakaacha kufanya mipango ya kununua mipya mapema, kwanini tusihisi kuwapo kwa uhujumu? Rashid alishasemwa mengi juu ya ufisadi, alipaswa aondoke/aondolewe pale tanesco awekwe mwingine ambaye baada ya kuhisi ukame angeleta mpango wa kununua mitambo mipya; huyu Radhid amekaa tu pale akisuburi aseme - niliyoyasema mmeyaona?
  Yabidi nasi tumuulize - ulichukua hatua gani ambazo hazivunji sheria?
   
 6. O

  Ogah JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  hebu mtueleze mna maana gani hapo..............
   
 7. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Naona mambo yanaanza kuwa wazi sasa
   
 8. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Je huyu Malima tangu alivyoambiwa na Rashidi tangu February, ni uamuzi gani aliochukua kuzuia nchi isiingie gizani? Kwani February mpaka sasa ni miezi kadhaa imekwisha pita na nchi ndio iko gizani.
   
 9. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Naona swala la kwanza la Tanesco wamechukua hatua gani limeshajibiwa. Sasa swali langu la pili la serikali imechukua hatua gani linahitaji kujibiwa maana niliuliza maswali matatu huko siku za nyuma.
   
 10. c

  care4all Senior Member

  #10
  Oct 13, 2009
  Joined: Feb 25, 2007
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanini hao waandishi wa habari hawakwenda muuliza Mh . Mwakyembe aliyesema hatutaki ile mitambo hata nchi ikiingia kwenye giza? Kwa sasa Mh. huyu anahoja gani au kuna mipya inakuja? Nchi inataendelea vipi DS kila kona...Kama hukuimarisha umeme maendeleo ni ndoto.
   
 11. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu hapo ndo pa kustaajabu, yaani wamefanya kusudi ili nchi iingie gizani ili tupigike na kuruhusu wanunue mitambo chakavu ya Dowans, tena kwa bei ya kurusha, kwakweli binafsi niko radhi niwashe kibatari but I stand for NO kwa RICHMOND!!
   
 12. t

  tk JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kutokana na maelezo yaliyopatikana katika kikao hicho ni kuwa, kwa mujibu wa taratibu zilizopo, inachukua miezi 12 tangu zabuni zitangazwe mpaka mitambo inunuliwe na kufika Tanzania. Kwa mantiki hiyo, tangu April 2009 wakati maamuzi ya kutonunuwa mitambo ya Dowans yalipochukuliwa mpaka sasa ni miezi 6 tu. Kwa hiyo serikali bado imo katika muda wa mchakato huo..
   
 13. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,471
  Likes Received: 1,427
  Trophy Points: 280
  tatizo hapo issue ni kwa nini iwe mitambo ya DOWANS, kama kweli Tanesco walikuwa na nia ya kweli kukabiliana na upungufu wa umeme wangetoa mapendekezo serikalini ya kuhitaji mitambo sio kuhitaji dowans, kama muda tulikuwa nao wa kutosh ahata wa kuagiza mitambo mingine lkn cha kushangaza wao tanzesco ikafikia kipindi wakasusa, na inashangaza mtu kama Idrissa hadi leo bado yupo pale wakati yeye alitakiwa asiwepo kwa kushindwa kuishawishi serikali kutafuta mitambo ya kuzalisha umeme
   
 14. t

  tk JF-Expert Member

  #14
  Oct 13, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Naona usifikirie binafsi. Hebu wafikirie wawekezaji wenye viwanda, wafanyakazi viwandani, wafanyabiashara, wagonjwa hospitalini, wanafunzi shuleni, confidence na competitiveness ya nchi kwa wawekezaji.. Jee wote hao wawashe vibatari?
   
 15. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #15
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Nakumbuka mwaka jana watu walikuwa wanasema kuwa another disaster like that of 2007 can be avoided, lakini kutokana na ujinga wetu we are in it again. Na ajabu watu watapigwa siasa tu na hakutakuwa na solution yoyote. Wanachoongea wahusika ni kama blame game ambayuo haitasaidia kuleta suluhu ya tatizo
   
 16. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #16
  Oct 13, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wanasiasa wameingiliia wataalamu na sasa itabidi wawajibishwe na wananchi kama hali itakuwa mbaya.
   
 17. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #17
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Huyo Radhid (Rashid) alishafanya hivyo unavyotaka na usifikiri kuwa binaadamu sote tunafikiri sawa. Kwa yeye aliona kuwa suala la kununua mitambo ya Dowans ingekuwa suluhisho la muda na baadae kufuatiwa na ununuzi wa mitambo mengine.
  Nionavyo mimi nim kuwa Watanzania hatuna misimamo katika maamuzi yetu kwani hata baada ya ushauri wa kitaalamu tuliamua kwa wingi wetu kukubali kuwa tuko tayari kukaa giza kuliko kununua Dowans lakini sasa tunatafuta wachawi wakati tunachopaswa kufanya ni kukubali matokeo ya uamuzi wetu TAKATIFU.
  Nasema takatifu kwani tulikuwa na bado tuko vichwa ngumu kubadili uamuzi Eti Sheria itakiukwa. Sawa sheria uitakiukwa lakini sheria si zimewekwa kuleta unafuu wa mambo? sasa Sheria inapokuwa kikwazo na sote tushajua kwaninmi hatuifanyii marekebisho hiyo sheria kwa maslaha ya Taifa?
  Tatizo Tanzania haiongozwi na busara na uzoefu wa viongozi bali inaongozwa na unazi sawa wa ule wa Yanga na Simba ambao hakuna anaekubali mwenziwe ana hoja ya kujenga. Hivi sasa tunaongozwa na Ufisadi v/s upambanaji na kila mmoja akili yake iko huko tu. Nafikiri tuwe na moyo wa kukabili matokeo ya maamuzi yetu na kuacha kutafutana uchawi. Mgao wa umeme ni matokeo ya ukaidi wetu na tukubali matokeo ,basi!
   
 18. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #18
  Oct 13, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,721
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  Punguza hamasa mkuu...

  Tanesco wanachoweza kufanya ni kushauri...na walifanya hivyo kwa ushahidi wa maneno ya waziri malima....kwamba walishauri nchi iwe na back up ya umeme na ready made solution ilikuwa ni kununua dowans...kilichotokea ni historia...lakini tunachojua kwa hakika ni kuwa dowans ilikataliwa na wizara ilishindwa kuanzisha mchakato wa kutafuta mitambo mipya...na hilo ndio limetufikisha hapa.....je lawama iende kwa tanesco au wizara...jazba itatuongoza kuinyooshea kidole tanesco lakini busara ni wizara kwani mwisho wa siku si tanesco ambayo ingekuwa na ultimate responsibility ya kununua dowans....si tuliona richmond...au ndio tumeshasahau maana lowasa alikuwa kipenzi chetu...mwanamtandao mwenzetu?????
   
 19. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #19
  Oct 13, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Tanesco haina lawama.Serikali kupitia wizara ingetafuta mbadala wa Dowans.Full stop!
   
 20. c

  chabeby Member

  #20
  Oct 13, 2009
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  penye ukweli uongio hujificha hata kama utachukuwa muda nrefu kiasi gani? kwa haya ya mgao tunayoyashuhudia leo kama yamesababishwa na mvutano wa kisiasa kuliko kitaalauma kama ulivyoonywa basi wabunge wetu ni wenda wazimu na ni wasema hovyo bila kuangalia matokeo ya kile wakisemacho.

  Nani alaumiwe?
  Nawakilisha......
   
Loading...