BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,009
Si mmekwisha ambiwa kuwa mitambo mipya imekwisha agizwa lakini itachukua miezi 12?
Naona hiyo mitambo mipya inaanza kusukwa toka A ndiyo maana inachukua miezi 12
Si mmekwisha ambiwa kuwa mitambo mipya imekwisha agizwa lakini itachukua miezi 12?
Mkuu wangu wewe ni msomi mzuri sana na bila shaka unaelewa vizuri maana haswa ya msemo Usipoziba Ufa utajenga ukuta...
Kwa maana kwamba muda na gharama za kuziba ufa ni ndogo sana ukilinganisha na ujenzi wa Ukuta mzima.. Lakini inapotokea kwamba gharama kuziba huo Ufa zinazidi zile za ujenzi wa Ukuta kwa nini wananchi wasithubutu kuuliza?..
Nitarudia kusema kuwepo kwa IPTL na Dowans ni ktk kuziba ufa ulotokea katika mahitaji ya Umeme wetu, wala sii moja ya mikakati ya kuendeleza Umeme nchini, tunaziba pale palipobomoka..
Watanzania mna-bore na mko negative sana na ndio maana hamuendelei. JK alipoamuru kuwashwa kwa mitambo, mnalalamika kuwa mawazo yalikuwa ya Zitto Kabwe.
Gharama za IPTL zinaanza kuonekana, mnalalamika kuwa gharama ni kubwa sana.
Hakuna modernity inayoshuka kutoka mbinguni kama chakula cha wana w Israel. Acheni kulalamalalama.
sawa wana solve problem, lakini najiuliza hivi ni kwa nini wale ambao wamesabisha tufike hapa hawajatiwa mbaroni tuu? wale wenye mamlaka ya kufanya maamuzi ambao walijua kwamba mitambo ya Dowans sio suluhu kwa sababu ni ya kitapeli na iko kwenye kesi lakini wakaendelea kutetea kwamba inunuliwe badala ya kununua mitambo mipya mara moja.
Walijua kwamba kiangazi huwa kinakuja kila mwaka katika miezi hii lakini hawakufanya juhudi yoyote ya kununua mitambo mipya kana kwamba mitambo pekee hapa duniani iendeshwayo kwa gesi ni ya Dowans tu.
Kama JK ameweza kuamuru mitambo ya IPTL iwashwe mara moja anashindwa nini kuamuru watu wanaosabisha hasara yote hii na usumbufu wote huu wasikamatwe mara moja na kufunguliwa mashtaka?
The presenter of this thread (TK) made a min Cost - Benefit analysis which is really sensible and gives a guidance for any decision maker. Tanzania needs power, and during this period emergence power is crucial but not at unjustifiable costs.
Hii Tanesco ipo kibiashara au inatoa huduma? Kama kweli wanafanya biashara tangia kuanzishwa kwake hivi sasa tungetegemea wanamiliki mitambo ya gas ya kuzalisha MW 500 ambazo zingekidhi mahitaji. Na hayo makampuni ya kijanja yasingekuwepo na wanasiasa wasingesogeza pua zao Tanesco na umeme ungekuwa bei poa.
Hapa ndio nachanganyikiwa! Umepanda kwa 40%!Waziri kasema kuwa umeme hautapanda bei