Sakata la Umeme: Gharama za IPTL juu Zaidi ya Mara 6 Kulingana na Dowans | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la Umeme: Gharama za IPTL juu Zaidi ya Mara 6 Kulingana na Dowans

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by tk, Oct 24, 2009.

 1. t

  tk JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mambo Yaiva

  • Total waleta shehena ya mafuta tani 7,500
  • Yataumika kufua umeme megawati 100
  • IPTL kutumia Shs milioni 766 kila siku ya Mungu
  Na Isaac Chanzi
  Mtanzania
  Jumamosi Oktoba 24 2009


  Shehena ya kwanza ya mafuta kwa ajili ya mitambo ya kuzalisha umeme ya Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) inawasili kesho nchini.

  Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alisema Dar es Salaam jana kuwa shehena hiyo itakuwa ni ya ujazo wa tani 7,524.

  Mitambo ya IPTL itawashwa Jumapili ya Novemba Mosi mwaka huu huku uendeshaji wake ukiigharimu serikali Sh. Bilioni 23 kwa mwezi, sawa na Sh milioni 766 kwa siku.

  Jumanne wiki hii, Rais Jakaya Kikwete aliagiza kuwashwa mara moja kwa mitambo hiyo inayotumia mafuta baada ya nchi kuingia gizani kutokana na kuharibika kwa mitambo ya Songas na Kihansi.

  Rais aliziagiza Wizara za Fedha na Uchumi , Nishati na Madini, Katiba na Sheria na Shirika la Umeme (Tanseco) kufanya kazi kila moja kwa nafasi yake kuhakikisha mitambo inawashwa.

  "Hadi jana (juzi) mchakato wa kupatikana mafuta ulikuwa umekamilika. Wizara ya Fedha na Uchumi imeshajipanga kwa ajili ya malipo ya mzigo huo ili kusiwe na mgogoro wowote." alisema Ngeleja.

  Alisema kampuni ya Total Tanzania Limited ndiyo iliyopewa dhamana ya kuleta shehena hiyo.

  "Ile mitambo inawashwa kwa kufuata taratibu maalum na sasa wataalamu wanaendelea na kikao kati ya Tanesco, mfilisi (RITA), Wartsila, benki ya Standard Chartered, wakijadili gharama mbalimbali kama mafuta na kujua zitumie siku ngapi kuipasha moto mitambo." alisema.

  Waziri huyo wa Nishati na Madini aliuhakikishia umma kuwa mchakato wa takwimu zote zinazohusu mitambo ya IPTL kuiwezesha inawashwa zimeshwapelekwa tangu jana Wizara ya Fedha na Uchumi kwa ajili ya uhakiki ili fedha iweze kutolewa.

  Mtambo wa Songas wenye kuzalisha megawati 20 ulitarajiwa kuwashwa jana , huku mtambo wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wa Hale – Tanga nao ukiwa umeanza kuzalisha umeme wa megawati kati ya 5 na 6 kutokana na kina cha maji ktotosheleza uwezo wa megawati 8.

  Awali, Kaimu Meneja Uendeshaji wa kampuni ya Wartsila, Gilbert Ndesamburo, aliwaambia waandishi akiwa pamoja na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kuwa mitambo hiyo, amabyo illingizwa miaka miwili iliyopita, ikiwashwa kwa saa 24 hutumia mafuta lita 625,000 huku lita moja ya mafuta hayo ikiuzwa kwa Sh 1,200.

  Ndesamburo alisema kituo hicho kina uwezo wa kuhifadhi mafuta kwa wastani wa tani 15,000 sawa na zaidi ya lita milioni 15.

  Mitambo hiyo, ambayo ipo kumi na yenye uwezo wa kila moja kutoa megawati 10, ilifungwa nchini mwaka 1998 na ikiwashwa hufua megawati 100 za umeme.

  Serikali ilikuwa imeagiza mitambo hiyo ibadilishwe iwe inatumia gesi asilia kuiendesha , ili kupunguza gharama za uzalishaji, lakini Wizara ya Nishati na Madini ikasimamisha mchakato huo kusubiri kumalizika kwa kesi ya msingi inayoendelea mahakamani.

  Katikati ya mwaka huu Rais Kikwete aliagiza mchakato huo wa kubadili mitambo uendelee badala ya kusubiri kesi hiyo kumalizika.

  Uendeshaji wa mitambo ya IPTL kwa sasa unasimamiwa na kuendeshwa na kampuni kandarasi ya Wartsila,ambayo iliingia mkataba wa miaka miwili na serikali, kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme.

  Mwaka 2006 nchi illingia gizani wakati kulipotokea ukame mkubwa na kusababisha serikali kutafuta suluhisho la haraka ambalo lilisababisha ijikute ikiangukia kwenye kashfa ya Richmond.

  Kiwango kinachotumiwa na IPTL kufua umeme, kinaanza kufungua sura mpya yenye kuonyesha kuwa kazi ya kuzalisha umeme si lelemama inahitaji fedha nyingi ajabu.

  Itakumbukwa kuwa Kamati ya Bunge ya Kuchunguza Mkataba Tata wa Richmond, ilisema kuwa serikali ilikuwa inaingia gharama kubwa kulipa Sh. Milioni 152 kwa siku kwa ajili ya kuzalisha megawati 125 kupitia Kampuni ya Dowans.

  Kwa sasa IPTL watalipwa Sh milioni 766 kila siku ya Mungu kama gharama za uendeshaji na watazalisha megawati 100, ikilinganishwa na 125 za Dowans ambazo zingezalishwa kwa h milioni 152 kwa siku.

  Kampuni ya Songas ambayo inazalisha umeme megawati 180 hupokea Sh milioni 284 kila siku iendayo kwa Mungu tangu ilipoingia mkataba na serikali.

  Hii inathibitisha kuwa gharama za kuzalisha umeme ziko juu sehemu zote duniani.

  Tangu Septemba, mwaka huu, nchi iliingia gizani baada ya kuwepo upungufu wa megawati 180 kwenye gridi ya taifa kutokana na kuharibika kwa mitambo ya Hale na Kidatu. Kwa sasa imeelezwa imetengamaa.


  Article ya Mtanzania inaishia hapo. Yafuatayo ni mchango wangu.

  Tangu gharama za kuzalisha umeme kutumia mitambo ya IPTL zilipotangazwa, nimejaribu sana kuwauliza wataalamu wa JF wanielimishe kuhusu gharama za kuzalisha umeme kwa kutumia gesi kwa mitambo ya Dowans. Bahati mbaya sikupata jibu la suala hilo mpaka leo nilipoona article yenye mchanganuo huo katika Mtanzania.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo nimejaribu kulinganisha gharama hizo kwa makampuni matatu
  Yanayojitokeza:

  1. Gharama za kuzalisha megawati moja kwa mitambo ya IPTL ziko juu kwa Tshs. 4.9 milioni kulinganisha na gharama za Songas na ziko juu kwa Tshs. 6.3 milioni kwa megawati ukilinganisha na Dowans.

  2. Gharama za kuzalisha megawati moja ni juu mara 4.9 ukilinganisha na Songas na mara 6.3 ukilinganisha na Dowans.

  3. Gharama za IPTL ziko juu kwa 385.5 % ukilinganisha na zile za Songas na 529.9 % ukilinganisha za Dowans.

  4. Gharama zinazookelewa kwa siku kwa kuzalisha megawati moja kwa mtambo wa Songas ni Tshs. 6.1 milioni na ukilinganisha na Dowans ni Tshs. 6.4.

  5. Ikiwa matumizi ya mitambo ya IPTL yataendelea kwa muda wa miezi sita, gharama ambazo zingeweza kuokolewa kwa kutumia mitambo ya Dowans zitafikia Tshs 145.0 Bilioni.

  Sasa Najiuliza:

  1. Serikali ilikuwa na options mbili. Aidha kuwasha mitambo ya IPTL au ile ya Dowans. Sasa huu uamuzi wa kuwasha mitambo ambayo gharama zake ni kubwa kiasi hicho ulifikiwa kwa vigezo gani?

  2. Mitambo ya IPTL inatumia mafuta ambayo yanakuwa imported. Kwanini nchi itumie fedha za kigeni kuagiza mafuta nje wakati gesi asilia ipo hapahapa nchini kama mitambo ya Dowans ingetumika.

  3. Tuanelezwa kila siku kuwa Tanseco ina matatizo ya kifedha. Jee hii ndio njia bora ya kuiondoa katika matatizo hayo.

  4. Ugumu wa Logistics nzima ya kuendesha mitambo ya IPTL haikuonekana? Kwanza kila wakati kutegemea meli na kampuni za kuagiza hayo mafuta. Yakichelewa tu hali inarudi palepale. Pili muda uanotumiwa na Mawaziri na maofisa wa Wizara na Idara mbalimbali
  kuhakikisha kuwa mambo yanaenda sawa wakati kwa Dowans ni straight forward operation ambayo ingeweza kusimamiwa na Dowans na Tanesco pekee.

  5. Kila siku tunaambiwa kuwa serikali haina fedha. Jee hii inajitokeza vipi katika maamuzi haya. Hizo fedha za ziada ambazo zingeweza kununua mitambo mingine kweli zinatupwa tu hivi kwa sababu za visasi? Tena tunapopeleka bakuli nje kuomba fedha kwa wahisani,
  hivi wanatuelewa vipi?

  6. Hii Kamati ya Nishati na Madini, haikuona madhara ya mambo yote haya wakati ilipopendekeza mkataba na Dowans uvunjwe? Na mess yote hii waliyoifanya katika kadhia nzima ya kuingilia maamuzi ya serikali na Tanesco mpaka wakatufikisha hapa, jee wajumbe wa Kamati hii kweli wanastahili kuchaguliwa tena kurudi Bungeni 2010?
   
 2. S

  SpinDoctor Member

  #2
  Oct 25, 2009
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dowans...Dowans...! Kwanini usiseme serikali inunue mitambo mipya!
   
 3. Insurgent

  Insurgent JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2009
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 469
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Siasa kwenye kila kitu ndio imetufikisha hapa.
  Jibu: Kaimu Meneja Uendeshaji wa kampuni ya Wartsila, Gilbert Ndesamburo
   
 4. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Jk hakuweza wala hawezi kuamuru mitambo ya Dowans iwashwe tu hivihivi, ikitaifishwa na kuwashwa wanaomiliki hiyo mitambo watapataje faida??
   
 5. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2009
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Sifuatiliagi haya masuala , sababu ni kuumiza kichwa ,so sijui IPTL ni nini na Songaz ni nini, ingawa najua DOwhans ni nini.

  Tatizo na shindwa kuelewa kwanini , pale walipo sema kuna janga la mgao linakuja , hatua zozote kufuatiliwa au hazikufutwa kuwezehsa hali hiyo isitokee, kwa kununua mitambo mipya au kununua spare za hiyo mitambo itakapo haribika ili tatizo kama hili likitoke liweze dhibitiwa mara moja.

  Nadhani viongozi wetu wanaoendekeza siasa zaidi, hawajui umuhimu wa nishati ya umeme na haswa ukizingatia hawajali hasara inayotokana na kukosekana na matumizi ya umeme, na dhani kwangu umeme ni uhai, na nadhani siwezi subiri kuhatarisha uhai ndio niweze fanya kitu ku nuusuru uhai .

  Utakuta vitu vingine mfano network ya LUKU au hata za ATM unaambiwa server iko down au inafanyiwa upgrading wakati hawawezi hata kua na backup yeyote , matokeo yake watu wanakaa bila umeme na kushindwa hata kutoa pesa kwenye ATM. jiulize ni hasara kiasi gani hapo?


  Tatizo haswa ni nini ?, mitambo ni ghali sana au je hizo spare zinakuja na Meli ambayo labda kuna Pirrates huko somalia wamechelewesha au ni nini haswa? ( sorry kuuliza hivyo labda majibu mmesha toa teari) , ila ina shangaza kwa nchi kusema hatuna pesa za kunua mitambo wakati vyanzo vya umeme vipo vingi na na ushahidi kuna company nyingi zimekuja hapa TZ kutaka kuanzisha vyanzo na wame pigwa chini bila sababu.Je hatuwezi hta kukopa pesa kunusuru janga hili kwakunua mitambo mipya?

  Labda hapa kuna dili lilikua linapikwa na halija pikika , la kunusuru Dohans na sasa itanusurika kwa kupitia IPTL? (swali tuu)

  HaYa mambo yanaumiza kichwa kufuatilia sababu haya make sence kabisa , pesa zipo ,kukopa kuna wezekana kama hakuna pesa , sioni sababu gani tuwe na tatizo hili ambalo halisababishwi na ukame bali ni hali ya kuharibika kwa mitambo .

  God Bless TAnzania.


  I hate Tanzania ,I hate being an African from Africa.
   
 6. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  sawa wana solve problem, lakini najiuliza hivi ni kwa nini wale ambao wamesabisha tufike hapa hawajatiwa mbaroni tuu? wale wenye mamlaka ya kufanya maamuzi ambao walijua kwamba mitambo ya Dowans sio suluhu kwa sababu ni ya kitapeli na iko kwenye kesi lakini wakaendelea kutetea kwamba inunuliwe badala ya kununua mitambo mipya mara moja.

  Walijua kwamba kiangazi huwa kinakuja kila mwaka katika miezi hii lakini hawakufanya juhudi yoyote ya kununua mitambo mipya kana kwamba mitambo pekee hapa duniani iendeshwayo kwa gesi ni ya Dowans tu.

  Kama JK ameweza kuamuru mitambo ya IPTL iwashwe mara moja anashindwa nini kuamuru watu wanaosabisha hasara yote hii na usumbufu wote huu wasikamatwe mara moja na kufunguliwa mashtaka?
   
 7. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  I love my motherland Tanzania, I hate everything that takes it into deep porverty and make it a difficult place to live...
   
 8. t

  tk JF-Expert Member

  #8
  Oct 25, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Si mmekwisha ambiwa kuwa mitambo mipya imekwisha agizwa lakini itachukua miezi 12?
   
 9. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #9
  Oct 25, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0

  Pengine tuangalia uwezekano wa kutumia nuklia salama, inatisha kuiongelea kutokana na gharama na utaalamu, it is about time yale mapesa tuliyofisadiwa na Richmond, EPA, Mkapa, Anna Mkapa, Kigoda, Chenge, Rostam Aziz, Sumaye na wengine yarudishwe, tupate nguvu ya kukaa mezani na wafadhili na watakia mema nchi yetu ili tutafute vyanzo vya umeme mbadala.
   
 10. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #10
  Oct 25, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Watanzania mna-bore na mko negative sana na ndio maana hamuendelei. JK alipoamuru kuwashwa kwa mitambo, mnalalamika kuwa mawazo yalikuwa ya Zitto Kabwe.

  Gharama za IPTL zinaanza kuonekana, mnalalamika kuwa gharama ni kubwa sana.

  Hakuna modernity inayoshuka kutoka mbinguni kama chakula cha wana w Israel. Acheni kulalamalalama.
   
 11. t

  tk JF-Expert Member

  #11
  Oct 25, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hapa issue sio kulalamika. Issue hapa ni kuwa jee ni sawa kuopt kwa option ya gharama kubwa wakati ya gharama ndogo ambayo itatoa mafanikio yale yale ipo?

  Sasa ukipoint out hilo kosa liko wapi?
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  Oct 25, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Vita dhidi ya ufisadi
   
 13. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #13
  Oct 25, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Siasa kwa kawaida inatakiwa always iwaletee wananchi maendeleo, sina uhakika na hizi politics za kwetu goal yao ni nini...........!
   
 14. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #14
  Oct 25, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,402
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  kwa hali ya mambo ilivyo sasa hivi siwezi hata kulaumu walalamikaji. Serikali za CCM in series, zilivyo-boronga; na hata wakifanya lipi nafuu halitakuwa la maana, kwa kuwa the bad have overwhelmed their good. CCM in case wanataka ku-exist lazima wafanya sweeping policy changes, in all departments; from Good Governance, judiciary, police force, education, patriotism and charisma! Kwa Tanzania kuwa politician ni sawa na kuwa MWONGO. Na hata kama serikali itafanya kitu chochote kitachukuliwa kuwa ni uongo au hata kuwa ni utapeli.
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Oct 25, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu wewe ni msomi mzuri sana na bila shaka unaelewa vizuri maana haswa ya msemo Usipoziba Ufa utajenga ukuta...
  Kwa maana kwamba muda na gharama za kuziba ufa ni ndogo sana ukilinganisha na ujenzi wa Ukuta mzima.. Lakini inapotokea kwamba gharama kuziba huo Ufa zinazidi zile za ujenzi wa Ukuta kwa nini wananchi wasithubutu kuuliza?..
  Nitarudia kusema kuwepo kwa IPTL na Dowans ni ktk kuziba ufa ulotokea katika mahitaji ya Umeme wetu, wala sii moja ya mikakati ya kuendeleza Umeme nchini, tunaziba pale palipobomoka..
   
 16. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2009
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Ningependa tena wana JF kuuliza, TANESCO wanapata wastani wa shilingi ngapi kwa siku kutokana na mauzo ya umeme?NCHI HII IMEOZA NI WAKATI SASA WA KUBADILISHA MFUMO WA MAJINA AU MARAFIKI WALIOMSAIDIA AU WALIOKUA KARIBU NA NYERERE na SASA wanarithishana utawala wa nchi yetu.Utashanga watoto wadogo wanakosa TIBA kwa kukosa pesa kiasi kidogo mpaka waende kwenye ma tv kuomba wasamaria wema,lakini mabilioni ya kuwapa mabepari kununua mafuta wanazipata kwa dharura waliojua kwani mtaalam Dr Idrisa Rashid alishataadharisha juu ya ukosefu wa umeme.
   
 17. t

  tk JF-Expert Member

  #17
  Oct 25, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ufisadi upi? Wa IPTL au wa Dowans. Maana makamnpuni yote mawili ya harufu ya ufisadi ndani yake.
   
 18. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #18
  Oct 25, 2009
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mliwachagua wenyewe huku mkiwa na akili timamu, mkadai ni "chaguo la Mungu" sasa mnalia kilio cha mbwa mdomo juu!
   
 19. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #19
  Oct 25, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ustaadh,
  Wewe hukuwepo?
   
 20. Insurgent

  Insurgent JF-Expert Member

  #20
  Oct 25, 2009
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 469
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Memory za watanzania ni fupi kama zile za kuku...
  IPTL...Brian Cooksey report on the whole saga, does it ring any bell?
  You can also search for IPTL in here.
   
Loading...