Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,279
- 25,854
Naanzia pale panapoelezwa kuwa aliyekuwa Meya wa Jiji, Dr. Didas Masaburi aliuza kihalali hisa za UDA,asilimia 51,kwa kampuni ya Simon Group. Imesemwa kuwa Meya alikuwa na mamlaka yote ya kuuza hisa husika.
Kwanza,hisa za UDA ni moja ya mali za Halmashauri ya jiji. Mali yoyote ya jiji hupatikana au kuondolewa kwa ridhaa ya vikao halali vya Baraza la Madiwani la Jiji. Kununuliwa au kuuzwa kunapaswa kuwa na baraka za Madiwani kutokana na kikao.
Pili,Meya au Naibu Meya anatenda kadiri ya maamuzi ya kikao cha Madiwani. Kinyume chake,halifanywi jambo halali. Kuhusu la hisa za UDA,ushahidi pekee unaotakiwa ni azimio la Baraza la Madiwani wa jiji kuuza hisa zao za UDA. Kama hakuna,Meya hawezi kuwa ameuza kihalali.
Kuondoa mjadala,maazimio yaanikwe.