Sakata la tril 1.5 Dr. Slaa asema ni sababu ya bunge kupitisha vitu hewa. Hapa anakiri tumepigwa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Screenshot_2018-05-14-06-07-13.png
 
Ni wapi amekuri kuwa "mmepigwa". Soma kwanza mahojiano yake yote kabla ya kutoa angalizo kupitia kichwa cha habari.

Sasa unapigwa vipi kwa pesa ambayo hujui ilipo?

Huu mjadala wa 1.5T ni "tango pori" ndio maana wenye uelewa mpana wameachana nao.

Zitto alitaka kuteka kazi za PAC kwa faida ya muda mfupi. Ndio maana alisoma repoti ya CAG kwa haraka na kutoa tamko kabla ya PAC ambao ndio wahusika wakuu bungeni.

Yeye wakati akiwa Mwenyekiti wa PAC alikuwa hatoi nafasi wapinzani kuteka kazi za PAC.

Ninakumbuka kuna kipindi Godbless Lema alimwambia Zitto aache ubinafsi.
 
aipoundiwa zengwe apigwe chini Mungu Mkubwa!
Maana awamu hii...
 
Ni wapi amekuri kuwa "mmepigwa".

Sasa unapigwa vipi kwa pesa ambayo hujui ilipo?

Huu mjadala wa 1.5T ni "tango pori" ndio maana wenye uelewa mpana wameachana nao.

Zitto alitaka kuteka kazi za PAC kwa faida ya muda mfupi. Ndio maana alisoma repoti ya CAG kwa haraka na kutoa tamko kabla ya PAC ambao ndio wahusika wakuu bungeni.

Yeye wakati akiwa Mwenyekiti wa PAC alikuwa hatoi nafasi wapinzani kuteka kazi za PAC.

Ninakumbuka kuna kipindi Godbless Lema alimwambia Zitto aache ubinafsi.
Achana nae zito!
Wewe unajua zilipo?
 
Tunasubiri ripoti ya kazi zake za ubalozi aachane na siasa za kutengeneza read story za magazeti. Huu sio wakati wake
 
Ni wapi amekuri kuwa "mmepigwa". Soma kwanza mahojiano yake yote kabla ya kutoa angalizo kupitia kichwa cha habari.

Sasa unapigwa vipi kwa pesa ambayo hujui ilipo?

Huu mjadala wa 1.5T ni "tango pori" ndio maana wenye uelewa mpana wameachana nao.

Zitto alitaka kuteka kazi za PAC kwa faida ya muda mfupi. Ndio maana alisoma repoti ya CAG kwa haraka na kutoa tamko kabla ya PAC ambao ndio wahusika wakuu bungeni.

Yeye wakati akiwa Mwenyekiti wa PAC alikuwa hatoi nafasi wapinzani kuteka kazi za PAC.

Ninakumbuka kuna kipindi Godbless Lema alimwambia Zitto aache ubinafsi.
mkishakula miugali yenu ya bure behind closed doors Ikulu na Lumumba nakuvimbiana mitumbo yenu at taxpayers expense mnakuwa wajinga na miphd na mimaster yenu yakukariri. Mmeshindwa kudeliver mmebaki kuvunja rekodi ya kuiba matrilioni. PRAY WE DONT GET INTO POWER!
Screenshot_2018-05-14-07-19-00.png
 
Ni wapi amekuri kuwa "mmepigwa". Soma kwanza mahojiano yake yote kabla ya kutoa angalizo kupitia kichwa cha habari.

Sasa unapigwa vipi kwa pesa ambayo hujui ilipo?

Huu mjadala wa 1.5T ni "tango pori" ndio maana wenye uelewa mpana wameachana nao.

Zitto alitaka kuteka kazi za PAC kwa faida ya muda mfupi. Ndio maana alisoma repoti ya CAG kwa haraka na kutoa tamko kabla ya PAC ambao ndio wahusika wakuu bungeni.

Yeye wakati akiwa Mwenyekiti wa PAC alikuwa hatoi nafasi wapinzani kuteka kazi za PAC.

Ninakumbuka kuna kipindi Godbless Lema alimwambia Zitto aache ubinafsi.
Tatizo siyo Zitto bali ripoti ya CAG inaning'inia hewani........imetoa fursa kwa wanasiasa " kusema" wapendavyo!
 
Zipo zilizotumiwa ktk shughuli nyeti zinazohusu usalama wa nchi lkn, at the same time, watu wakatumia mwanya huo kupiga zingine, ndio maana vitabu haviwezi ku-balance.

Serikali makini inayoweza kupambana na ufisadi bado hatujaipata na inaonekana tutasubiri sana kwani hii ya sasa kwenye maswala ya ufisadi ni fix tu hamna lolote.
 
Aliyewahi kuwa Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dkt. Wilbroad Slaa ambaye sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Sweden amesema kuwa mjadala wa kuonekana au kutoonekana kwa sh 1.5 trilioni lililoibuka baada ya kuwasilishwa kwa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) limetokana na udhaifu wa mfumo uliopo wa upitishaji wa bajeti.

Ameeleza kuwa hali hiyo inatokana na mfumo wa Bunge ambao unaruhusu wabunge kupitisha bajeti ambayo fedha zake hazipo tayari.

Dkt. Slaa amefafanua kuwa wabunge wamekuwa wakipitisha bajeti kabla ya fungu halisi kupatikana, ikiwa ni nadharia inayosubiri fungu hilo kupatikana kupitia kwa wafadhili au michakato mingine ya ukusanyaji.

“Kama fedha nyingi zinatumika bila kupitishwa na Bunge kwa sababu ndiyo mfumo wetu, unawezaje kuhoji fedha hizo zilitumikaje?” Dkt. Slaa anakaririwa na Mwananchi waliofanya naye mahojiano maalum.

Aliongeza kuwa kwa kawaida, huwezi kupata takwimu halisi za miradi mikubwa ya Serikali ndani ya kipindi cha mwaka wa fedha husika kwani miradi hiyo huwa katika hatua za utekelezaji.

Balozi Slaa ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Karatu kwa tiketi ya Chadema alisema kuwa kinachofanyika hivi sasa bungeni, wabunge wengi hawajadili hoja na badala yake wamekuwa watu wa kufanya ushabiki na kuhitimisha hoja tu.

Alisema kuwa wakati alipokuwa bungeni, alikuwa anafanya utafiti wa kutosha kuhusu masuala ya ufisadi na kuhakikisha anapata nyaraka zote husika kabla ya kuliwasilisha.

“Ndio maana unaona wakati huo niliweza kuwachachafya Mawaziri kwakuwa nilikuwa sikurupuki,” alisema.

Sakata la sh 1.5 trilioni liliibuliwa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe na baadaye kujibiwa na Serikali pamoja na Chama Cha Mapinduzi.
 
Back
Top Bottom