Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,670
- 119,302
Wanabodi,
Mjadala wa TBC kusitisha matangazo ya moja kwa moja, live ya vikao vya bunge unaendelea asubuhi hii Star TV.
Miongoni mwa waalikwa ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Zuberi Kabwe, ambaye anatarajiwa kuingia studio muda wowote kuanzia sasa.
Hivyo wale wenye access na Star TV, mnaweza kufuatilia, mimi nitawajulisha Zitto ataongea nini.
Mgeni mwingine ni Mhe. Joseph Kakunda, mbunge wa Sikonge.
Karibu.
Pasco
======= Updates ===========
Zitto ameanza kwa kueleza kuwa mfumo wetu wa Public Broadcasting System bado haujakaa vizuri.
Zito amepangua hoja zote tatu za serikali kama sababu za kusitisha matangazo ya live!.
1.Hoja ya kuwa eti wananchi wanaangalia TV wakati wa kazi haina mashiko!, ameuliza Watanzania wangapi?, kwanza Watanzania wenye umeme ni asilimia 30% tuu!. Asilimia 80% ni wakulima, sasa kuna mkulima ataacha kwenda shambani kwa sababu anaangalia bunge?!. Huu ni ujinga tuu!.
2. Wametoa gharama, Zitto amesema ukilinganisha hizo gharama na haki ya wananchi kupata habari, gharama hizo ni nothing compared!.
3. Mjadala wa bunge ni masaa 5.30, TBC wao watatangaza kipindi cha saa 1 tuu, hii maanayake ni kufanya censorship nini waonyeshe na nini wasionyeshe!. Huu ni udikiteta tuu!.
- Zitto amesema anaamini sababu sio gharama, serikali inatumia gharama kubwa katika mambo mengine ya kupuuzi puuzi tuu bila kujali gharama, lakini kwenye jambo muhimu kama hili ndio kinatolewa kisingizio cha gharama!.
- Zitto amesema demokrasia ni kama jini, ukiishalifungulia kutoka ndani ya jicha, likiishatoka, huwezi tena kulirudisha kwenye chupa!.
Hiki kinachoonekana ni dalili za kwanza za madikiteta kote duniani kulidhibiti Bunge!.
- Huyu jamaa Joseph Kakunda, mbunge wa Sikonge, ni mmoja wa wabunge very smart upstairs na Hadi kwa kuvaa lakini ila anasema lengo la wabunge wa upinzani, ni kutafuta sifa kuonekana na watu wao kwenye majimbo yao!.
Zitto amesema wameanza na kuzuia TBC kutangaza live, kisha TV za binafsi, nazo zitazuiwa!.
- Zitto amesema amependekeza kufanyike mjadala wa kibunge wa jinsi ya kufinance Public Broadcasting Stations.
My Take.
Kwanza huyu mtangazaji wa Star TV aliyeko Dodoma, Joyce Mwakalinga ni mtangazaji mahiri na makini!, yule mbunge kilaza Joseph Kakunda, alipotetea TBC kusitisha matangazo ya live, kwa hoja watarekodi na kurusha usiku, akamuuliza majadiliano ya bunge ni masaa 8, kipindi cha TBC kitakuwa saa 1, kwa nini wananchi wanyimwe haki ya kuona kila kilichoendelea bungeni?!, mbunge kilaza huyu alitetea kuwa muda mwingi bunge linajadili kwa mabishano yasiyo na tija hivyo wananchi hawahitaji kuyaona hayo!.
Kiukweli Zitto ni mmoja wa wabunge makini sana kwa sababu amekuja pale stdio akiwa na facts kichwani, anapangua hoja za seikali with facts na mifano hai kutoka nchi nyingine.
Hongerra sana Zitto, hongera Star TV.
asanteni kufuatilia!.