Sakata la Rutabanzibwa vyombo vya habari vimefanya usaliti? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la Rutabanzibwa vyombo vya habari vimefanya usaliti?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WATANABE, Jan 10, 2012.

 1. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  Prudence Karugendo​
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  KWA siku za karibuni zimekuwapo lawama kutoka kwa wananchi na taasisi mbalimbali za kiraia dhidi ya utendaji usioridhisha unaoonyeshwa na watumishi wa umma. Lawama hizo ambazo kwa kiasi kikubwa zinachochewa na tabia ya ukiukaji wa maadili ya utumishi wa umma ambayo imetokea kuzoeleka kwa lugha ya siku hizi kama ufisadi, kwa kiasi kikubwa zimebebwa na vyombo vya habari.

  Vyombo vya habari vimekuwa mstari wa mbele katika kuwanyooshea kidole watumishi wa umma wanaoonekana kuteleza na kutoka nje ya mstari wa maadili ya utumishi wao. Na kwa mwenendo huo vyombo vya habari vimepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa watumishi wa umma walio waadilifu.

  Vimejipatia sifa ya kuufichua na kuufunua uovu uliomo kwenye utumishi wa umma ikiaminika kwamba vyombo hivyo havifanyi hivyo kwa lengo la kumkomoa yoyote bali kuwafanya wahusika wajirudi na kuyazingatia maadili ya utumishi wao kwa manufaa ya jamii nzima ya Watanzania.

  Lakini bahati mbaya kwa sasa kuna minong'ono ya chini chini kuhusu namna vyombo hivyo vya habari vinavyozishughulikia tuhuma za uovu wa watumishi wa umma.

  Inasemekana kwamba kwa sasa tuhuma za uovu zinapotolewa vyombo vya habari vinataka zibaki tu ni tuhuma hata pale zinaposafishwa au kupatiwa ufumbuzi kwa kuonyesha kwamba kilichodhaniwa ni uovu kumbe siyo.

  Papo hapo tuhuma nyingine kuonekana zikifumbiwa macho na vyombo vya habari.
  Minong'ono hiyo imejitokeza kutokana na sakata la Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Patrick Rutabanzibwa, lililokuzwa kwa njia ya kumsakama hadi kufikia kiongozi huyo kuhukumiwa katika Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kulipa faini ya shilingi laki tano au kwenda jela miezi 6 kwa kilichodaiwa kuidharau mahakama, kabla ya Mahakama ya Rufaa kuibatilisha hukumu hiyo.

  Mpaka sasa ni wananchi wachache wanaoelewa kwamba Mahakama ya Rufaa iliibatilisha hukumu iliyokuwa imewatia Rutabanzibwa na wenzake hatiani.

  Wananchi wengi wanaomfahamu vizuri walikuwa bado wanamsikitikia kutokana na hukumu hiyo iliyotolewa na Mahakama ya Ardhi bila kuelewa kuwa ilishatenguliwa kufuatia vyombo vingi vya habari kukaa kimya juu ya jambo hilo.

  Kitendo cha vyombo vya habari kutolipa uzito wa kutosha suala la kubatilishwa kwa hukumu dhidi ya Rutabanzibwa kimeitia dosari sifa iliyokuwa ikitolewa kwa mhimili huo wa nne usio rasmi wa nchi.

  Kwa sasa imeanza kutafsiriwa kwamba kumbe zilizokuwa zinaonekana kama juhudi za kuufichua uovu zilizokuwa zinafanywa na vyombo vya habari ndani yake kuna kukomoana tofauti na ilivyodhaniwa mwanzo. Huu ndio ni wakati mzuri wa vyombo vya habari kuikana tafsiri hiyo.

  Vinginevyo nguvu ya vyombo vya habari inayotumika kuufichua uovu ingebaki endelevu hata pale sehemu husika inapokuwa imetakaswa ili kudhihirisha kwamba vyombo vya habari havilengi kukomoa bali kurekebisha. Pia hiyo inaondoa dhana ya kwamba vyombo vya habari vinatumiwa na baadhi ya watu kwa ajili ya malengo binafsi.

  Kwa ajili hiyo nimeamua kufuatilia sakata hilo la Rutabanzibwa ili nione kilichojiri mpaka kufikia Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kutoa adhabu hiyo ambayo baadaye ilikuja kubatilishwa na Mahakama ya Rufaa. Niliyoyagundua katika kufuatilia kwangu ni ya kushangaza na kusikitisha.

  Kwanza ni kwamba kilichomponza Rutabanzibwa ni msimamo wake wa kuyasimamia maadili ya kazi na kutokubali kuyumbishwa kwa namna yoyote kutoka kwenye maamuzi halali anayoyaamini na kuyasimamia.

  Hayo nimeyagundua baada ya kuisoma barua aliyoandikiwa tarehe 5/7/2011 na taasisi moja ya Kiislamu, barua hiyo iliyojaa matusi na vitisho vya kila aina, iliyonakiliwa kuanzia Ikulu kwa rais, taasisi mbalimbali za serikali na za kidini, hadi kwa ndugu, jamaa na marafiki wa Rutabanzibwa.

  Ilikuwa ikimtaka Rutabanzibwa na wenzake, kama wao na si kwa nafasi zao, kusaini hati za viwanja Na. 1272 na 1273 vilivyopo katika eneo la Msasani Peninsula, jijini Dar es salaam, katika muda wa siku nne tangu alipopata barua hiyo.

  Kama kawaida yake, Rutabanzibwa si mtu wa kutetereshwa na matusi wala kurubuniwa kwa njia yoyote ile. Kawaida yake ni kusimamia usahihi na ukweli. Ndiyo maana hakusaini hati hizo kama alivyotakiwa na barua hiyo. Ni imani yangu kwamba hakufanya hivyo kutokana na kuyazingatia zaidi maadili ya utumishi wake.

  Kadhia hiyo ndiyo iliyosababisha Mahakama ya Ardhi kumuamuru Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutoa hati ya viwanja vile vile Na. 1272 na 1273 Msasani Peninsula, vinavyotajwa kwenye barua hiyo ya vitisho.

  Viwanja ambavyo kimsingi havina uhusiano wowote na taasisi hiyo ya Kiislamu iliyokuwa ikitoa vitisho kwa Rutabanzibwa.

  Inasemekana viwanja hivyo ambavyo katika ramani ya jiji vinapaswa kuwa sehemu ya wazi vilipatikana baada ya serikali kutumia viwanja viwili Na. 1860 na 1861 ambavyo vilionekana kama viko katika umiliki wa Oysterbay Properties LTD kule kule katika maeneo ya Msasani Peninsula na baadaye umiliki wa viwanja hivyo kuhamia kwa Kampuni ya Kahama Mining Corporation LTD.

  Lakini hata hivyo inaaminika kwamba viwanja hivyo viwili, Na. 1860 na 1861 vilivyokuwa vinamilikiwa na Oysterbay Properties na baadaye Kahama Mining Corporation navyo vilikuwa katika eneo la wazi ambalo baadaye lilitumika kujengwa shule ya watoto wadogo ambayo mmiliki wa Oysterbay Properties alikuwa mmoja wa wadhamini kabla ya viwanja hivyo havijageuka kuwa mali ya Oysterbay Properties.

  Kumbukumbu zinaonyesha kwamba kulitokea mvutano kati ya serikali na Oysterbay Properties mwanzoni mwa miaka ya 2000, ambapo serikali ilikuwa inaonyesha kwamba viwanja hivyo viko katika eneo la wazi na kwa upande mwingine Oysterbay Properties ikidai kwamba viwanja hivyo ni mali yake.

  Ni katika kipindi hicho Waziri wa Elimu wa wakati huo, Joseph Mungai, akaagiza pajengwe Shule ya Sekondari ya Bongoyo katika eneo hilo. Miaka sita baadaye, Oysterbay Properties na Kahama Mining Corporation wakafungua shauri Na. 14 la 2008.

  Shauri hilo lilifunguliwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kitengo cha Ardhi dhidi ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Kamishina wa Ardhi, wakidai kwamba viwanja hivyo ni mali ya Kahama Mining Corporation.

  Pia walikuwa wanataka majengo yaliyomo katika viwanja hivyo yabomolewe (Shule ya Sekondari ya Bongoyo) na waliovivamia waondoke.

  Mara baada ya shauri hilo kusajiliwa mahakamani ulitokea uahirishwaji wa mara kwa mara wa shauri hilo wakati pande mbili hizo zikitafuta kumaliza mambo nje ya mahakama, ili kama zingekubaliana zirudi tena mahakamani kuyasajili makubaliano hayo.

  Tarehe 16/10/2009 pande hizo mbili zikafikia muafaka na kuufikisha mahakamani kwa ajili ya kumbukumbu iliyohifadhiwa tarehe 19/10/2009. Tarehe hiyo Jaji Nchimbi akatoa maagizo mbele ya pande zote mbili kwamba kulingana na makubaliano yaliyofikishwa mahakamani hapo shauri hilo lilikuwa limepata muafaka.

  Jaji akaongeza kwamba namna muafaka ulivyokuwa mdaiwa wa kwanza angetoa viwanja mbadala ambavyo ni Na. 1272 na 1273 katika eneo la Msasani Peninsula ambavyo vingegeuzwa katika matumizi ya makazi/biashara na kisha kuamishiwa katika umiliki wa Oysterbay Properties LTD.

  Pamoja na mambo mengine mahakama ikathibitisha kwamba baada ya kusainiwa makubaliano hayo kusingekuwepo na madai mengine.

  Katika kuipitia hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi dhidi ya Rutabanzibwa na wenzake, Mahakama ya Rufaa iliona kwamba makubaliano hayo yaliyofikiwa yalikuwa hayatoi uhalali kamili kwa pande zote mbili kwa vile bado yalikuwa yanategemea hatua zaidi ambazo zilihitajika kuchukuliwa baadaye.

  Kwamba kama hatua hizo zingeshindikana makubaliano hayo yangebaki ni nyaraka tupu zisizoweza kutoa haki yoyote kwa pande zote mbili.

  Mahakama ya Rufaa ikaongeza kwamba iwapo vigezo vya mkataba ni vya mashaka au havijakamilika haiwezi kusemwa kwamba pande mbili zimefikia mkataba (makubaliano) mbele ya sheria. Tafsiri ni ya kwangu.

  "Makubaliano yenye mashaka, au yasiyoweza kutekelezwa bila mashaka, ni batili" Law of Contract Act (CAP 345 R.E. 2002) kifungu 29. Katika kubatilisha hukumu ya Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi dhidi ya Rutabanzibwa na wenzake.

  Mahakama ya Rufaa iliona kwamba wahukumiwa hao wangeweza kuchukuliwa kwa mtazamo wa harakaharaka kuwa nao ni sehemu ya shauri Na. 14 la 2008 kutokana na ukweli kwamba Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ambaye mashauri yote dhidi ya serikali yanapaswa yapitie kwake, alikuwa sehemu ya muafaka uliofikiwa.

  Lakini hata hivyo Mahakama ya Rufaa iliongeza kwamba chini ya kifungu 6(2) Mwanasheria Mkuu wa Serikali anaingia mara tu baada ya idara za serikali na maafisa wake kupokea notisi ya siku 90 za kujiandaa na shauri husika.

  Kwa kuwa Rutabanzibwa na wenzake hawakupewa notisi hiyo, moja kwa moja hawahusiki na shauri la Oysterbay Properties LTD na Kahama Mining Corporation LTD.

  Katika kuhitimisha hoja yake Mahakama ya Rufaa iliona kwamba kwa vile hapakuwepo makubaliano yoyote ambayo yangeweza kutekelezwa bila mashaka masuala yote yaliyofuatia yalikuwa ni batili kwa sababu hayakuwa na miguu ya kusimamia.

  Mpaka hapo tutaona kwamba taasisi ya Kiislamu iliyohusika kutoa vitisho kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ili kumshinikiza atoe hati za viwanja Na. 1272 na 1273, Msasani Peninsula, Dar es Salaam, haihusiki wala kutajwa mahali popote katika mgogoro mzima wa viwanja hivyo.

  Hiyo ndiyo inayoleta hisia kwamba nyuma ya mgogoro huo mzima wa viwanja hivyo walisimama watu waliotaka kutumia kila njia na kila mbinu kuhakikisha haramu inageuzwa kuwa halali hata kwa kutumia jina la Mungu.

  Kwahiyo kitendo cha vyombo vya habari kulipa uzito shauri na hatimaye hukumu ya Mahakama Kuu dhidi ya Rutabanzibwa, lakini vikageuka na kupooza pale shauri hilo lilipopelekwa katika Mahakama ya Rufaa, kimeacha maswali kwa wananchi.

  Wnanchi wanajiuliza kama kweli vyombo hivyo vya habari vimedhamiria kupambana na hatimaye kuitokomeza hali hii tata ya maisha inayotafsiriwa kama ufisadi katika jamii ya Watanzania? Na hapo ndipo linaponijia swali la kwamba katika sakata la Rutabanzibwa vyombo vya habari vimefanya usaliti?

  [​IMG]

  prudencekarugendo@yahoo.com
  0784 989 512
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  My take: Kwa jinsi Mwanasheria Mkuu wa Serikali alivyoshabikia hili suala kumalzimisha Katibu Mkuu kusiani hati za hivyo viwanja, anapaswa kujiuzru kutokana na hii hukumu.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Watanabe:
  Weka comment yako binafsi, vinginevyo utaonekana hujaisoma habari uliyoleta!
  Ni mtazamo tu!
   
Loading...