Sakata la richmond;tuliowaadhibu wanatosha;marmo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la richmond;tuliowaadhibu wanatosha;marmo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jan 23, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,442
  Likes Received: 5,695
  Trophy Points: 280
  Serikali yatunishia misuli wabunge
  HAKIKA JK KAZI UNAYO ULIWACHAGUA WENYEWE  [​IMG]
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Philip Marmo.  [FONT=ArialMT, sans-serif]Serikali imeshikilia masimamo wake wa kutokuchukua hatua zaidi dhidi ya watumishi wake waliohusika katika kashfa ya mkataba tata wa Richmond kama ilivyotakuwa na Bunge, na badala yake imesema yaliyotekelezwa yanatiosha.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Ukweli huo umedhihirika jana baada ya Serikali kuwasilisha kwa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini taarifa ya utekelezaji wa maazimio 23 ya Bunge kuhusu kashfa ya mkataba wa Kampuni ya Richmond.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mbali na taarifa ya utekelezaji wa maazimo hayo, pia iliwasilisha inayohusu hatma ya wamiliki wa mgodi wa makaa ya mawe Kiwira.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo walizungumza na Nipashe jana kwa sharti la kutotajwa majina walisema kuwa ripoti hiyo haina maelezo ya kuridhisha kujibu hoja za wabunge.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Habari zinaeleza kuwa taarifa ya serikali iliyowasilishwa jana haielezi chochote kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Habari kutoka ndani ya kikao cha kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge, jijini Dar es Salaam jana, zinaeleza kuwa taarifa hizo ziliwasilishwa kwa kamati hiyo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Philip Marmo.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Baada ya wajumbe wa kamati hiyo kuzisoma, baadhi waliamua kuondoka kimya kimya bila kusubiri kuzijadili [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]kwa kueleza kuwa Serikali imeonyesha jeuri na dharau kwa Bunge kwa kitendo chake cha kutofanyia kazi mapendekezo ya Bunge.[/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Wapo baadhi ya watu wanaodhani maagizo ya Bunge ni lazima yatekelezwe na Serikali, kazi ya Bunge ni kuishauri Serikali kwa hiyo Serikali imeridhishwa na hatua ambazo imekwishachukua kwa watumishi wake waliohusika kwenye sakata la Richmond,” mjumbe mmoja wa Kamati ya Nishati na Madini alinukuu taarifa ya Serikali kwa wabunge.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema taarifa ya Serikali imeeleza kuridhika na maelezo ya awali ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na pia adhabu ya onyo aliyopewa Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Dk. Edward Hoseah, baada ya kubainika kufumbia macho madudu ya Richmond.[/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Majibu haya yamewakera sana wabunge, tutajadiliana na kuwasilisha mapendekezo yetu kwenye mkutano wa Bunge Dodoma, lakini tumepanga kuishtaki Serikali kwa wananchi ambao ndiye mwajiri wa Bunge na Serikali,” alisema mbunge mmoja.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Vigogo waliotuhumiwa katika kashfa ya Richmond pamoja na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, Arthur Mwakapugi ambao tayari wamekwisha kustaafu utumishi serikalini.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Ripoti ya Richmond inatarajiwa kuwasilishwa bungeni baada ya makundi katika jamii, wakiongozwa na wabunge kutoridhishwa na hatua zilizochukuliwa na serikali katika kutekeleza maazimio hayo.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Taarifa ya jana inaonyesha kuwasafisha Mwanyika Dk. Hoseah.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo, Dk. Hoseah, alionywa kwa kutokuwa makini wakati akifanya uchunguzi wa mchakato uliofanikisha kuipa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura Kampuni ya Richmond Development (LLC).[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mbali na Dk. Hoseah, mwingine aliyeonywa, ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya majadiliano ya wataalamu, Singi Madata.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Taarifa ya jana inaeleza kuwa Serikali imeridhishwa na hatua iliyozichukua dhidi ya vigogo hao.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli, William Shellukindo (CCM), alithibitisha jana kamati yake kupokea taarifa hizo kutoka serikalini.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo, habari zilizopatikana baadaye zimeeleza kuwa wajumbe hao walifikia uamuzi huo kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kutoridhishwa na yaliyomo ndani ya taarifa hizo za serikali.[/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Baada ya kuondoka kikaoni, sijui wenzetu tuliowaacha walifikia maamuzi gani. Lakini hakuna cha kuridhisha katika taarifa hizo na zitazua malumbano makubwa bungeni. Suala hili CCM wanajimaliza wenyewe. Kwa ufupi ni matatizo matupu,” alisema mjumbe mwingine ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema katika maazimio 23 ya Bunge Serikali imeeleza kuridhishwa na hatua zilizochukuliwa na kamati za nidhamu kwa kuwaonya baadhi ya vigogo waliofumbia macho mkataba huo tata ambao uliliingizia taifa hasara ya mabilioni ya fedha.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya mapumziko ya kikao cha kamati yake jana, Shellukindo alisema taarifa kuhusu kashfa ya Richmond, waliipokea na jana asubuhi walianza kuipitia na kuijadili kazi hiyo walitarajia kuifanya hadi usiku.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema mara baada ya kuijadili na kutafakari, wataiwasilisha sambamba na maoni ya kamati katika Mkutano wa 18 wa Bunge, unaotarajiwa kuanza mjini Dodoma, wiki ijayo.[/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Tumepokea taarifa ya serikali kuhusu hoja ya Kampuni ya Richmond Development LLC. Tunaendelea na kikao nadhani hadi usiku. Tunajadili na kutafakari ili baadaye tukatoe taarifa bungeni, huko ndiko mtapata taarifa,” alisema Shellukindo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Bunge, jijini Dar es Salaam.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kuhusu taarifa ya Kiwira, Shellukindo alisema waliipokea na wamekwisha kuishughulikia na kusema: “Serikali imechukua hatua nzuri kuurejesha mgodi huo na kuwalipa waliokuwa wafanyakazi wake”.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Sakata la Richmond na Kiwira ni masuala, ambayo yamezua msuguano baina ya serikali na Bunge kutokana na serikali kusuasua katika kuwasilisha taarifa ya kuridhisha wabunge juu ya utekelezaji wa maazimio 23 ya Bunge kuhusu kampuni hiyo.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Pia, wabunge walitaka kujua kama waliokuwa wamiliki wa Kiwira, akiwamo Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa na aliyekuwa Waziri wake wa Nishati na Madini, Daniel Yona, baada ya serikali kutangaza kuurejesha mgodi huo kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Shirika la Madini la Taifa (Stamico), watalipwa fidia au serikali ndiyo italipwa.[/FONT]
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2010
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hamna kitu kipya kitoka serikali ya JK. Wanalindana. Huyu is one of us so lets protect him. Hii inaonyesha hawaheshimu umma ulio wachagua. I pity (maskini wenzangu) those who wasted their time kumpigia kura 2005. Leo hii wanaumia. Tusubiri binge lijalo
   
 3. O

  Omumura JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sipendi na sitaki kusikia sarakasi za Richmond mie,nasikia kichefu chefu, jamani mwenye Chui anipe moja bariidiiiiii ninywe then nilale niote dunia imeisha!
   
 4. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Haaaaaa haaaaaaaaaaaaa
   
 5. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,009
  Trophy Points: 280
  Waliomwambia JK ni mwoga wa maamuzi magumu hawakukosea wala kukurupuka. Ni kweli, wanamfahamu ndani nje. Rais wetu JK kwa watu wenye kuifahamu saikoloji anatoka katika kundi la watu wa haiba ya sanguishi. Kundi hili ni la watu maarufu sana hata kama hakuna kinachoweza kuthibitisha umaarufu wao. Kundi hili halifai kiuongozi. Watu pasipokuelewa hujichanganya kwa umaarufu wa watu hawa na kuwachagua viongozi. Hapo ndipo hulia na kusaga meno. Ni kundi la watu wenye haiba ya kumpendeza kila mtu, na hapo ndipo huharibu zaidi ya kawaida.
   
 6. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Bila shaka kikao cha CC jumapili kitatumika kulizima Bunge kabisa,wenyewe mtasikia jinsi kina Mwakyembe & Co watakavyonyea.
   
Loading...