Sakata la Richmond: Lowassa amjibu Mwakyembe, asema asitafte mtaji wa kisiasa

Haki hupatikana mahakani. Nakumbuka kuna kipindi flani Mwakembe alisema mahakama ya mafisadi imekosa Kesi kwa hiyo iliaminike akafungue Kesi. Kwa vyombo vyote vipo chini ya ccm kwa nini aongelee ktk majukwaa ukweli haupatikani ktk majukwaa
 
Polonium ndio inamsumbuwa Mwakyembe ubongo umeshaoza umejaa fungus.

Mwakyembe na marehemu Samuel Sitta ni watu wa ajabu sana kuwahi kutokea hapa duniani.
Lowassa angemlaumu Nassari aliyeianzisha hiyo maada Bungeni, Mwakyembe hakukurupuka tu kujibu alichokozwa . na kwa maana hiyo mlitaka akubali tu ndiyo, ndiyo ndiyo kwa alichosema Nassari?
 
Lowassa angemlaumu Nassari aliyeianzisha hiyo maada Bungeni, Mwakyembe hakukurupuka tu kujibu alichokozwa . na kwa maana hiyo mlitaka akubali tu ndiyo, ndiyo ndiyo kwa alichosema Nassari?
Mwakyembs ni maiti inayotembea, na wewe kama unaamini Mwskyembe ana akili timamu basi nawe ni maiti pia.
 
Kama ni mwizi wa mali ya umma, na Watanzania tunauchungu na majizi, kamavile ambavyo wezi wa kuku wanachomwa moto, KWA NINI SRIKALI YA CCM INAOGOPA KUMPELEKA MAHAKAMANI HUYU MTU ILI HAKI KWA TAIFA ITENDEKE? UJUE SERIKALI INATUMIA FEDHA ZETU NA MOJA YA MAJUKUMU YAKE KIKATIBA NDIYO HAYA.

KUPIGA KELELE MAKUKWAANI NA KUTAKA KUENDESHA MAMBO KWA MALUMBANO YASIYOKUWA NA MWELEKEO WALA HATIMA NI DALILI KWAMBA SERIKALI HAIJUI WAJIBU WAKE;, HAINA NIA NJEMA NA TAIFA, HAINA UJASIRI WA KUSIMAMIA MASLAHI YA UMMA, HAINA MWELEKEO WOWOTE SAHIHI BORA LIENDE, INAAAAASIMAMIA MASLAHI YA WATU BINAFSI NA KULINDA WAHARIFU, NA HIVYO HAIFAI NA HAINA SIFA YA KUWEPO!.

KAMA NDIVYO SERIKALI HII IONDOLEWE TUANZE UPYA. TUMECHOKA NA UPUUZI WA KINA MWAKYEMBE.
Serikali haiogopi kumpeleka mahakamani yule mwizi, ila inafanya busara za kumvumilia kwasababu anaimpact kubwa kwa siasa za Tanzania, kumkamata na kumzuilia mtu kama yule nyuma yake watakufa wapumbavu wengi watakaojifanya kuandamana na serikali haitawavumilia wapumbavu hao, lazima itawatia adabu na mtakufa hovyo hovyo!!!
Kuepusha hayo yote ndio inamvumilia kidogo ila muda ukifika atafikishwa tu mahakamani na atapata anachostahili...
 
Serikali haiogopi kumpeleka mahakamani yule mwizi, ila inafanya busara za kumvumilia kwasababu anaimpact kubwa kwa siasa za Tanzania, kumkamata na kumzuilia mtu kama yule nyuma yake watakufa wapumbavu wengi watakaojifanya kuandamana na serikali haitawavumilia wapumbavu hao, lazima itawatia adabu na mtakufa hovyo hovyo!!!
Kuepusha hayo yote ndio inamvumilia kidogo ila muda ukifika atafikishwa tu mahakamani na atapata anachostahili...


Acha upumbavu wewe.

Kumvumilia mtu mwizi kwa kuogopa impacts zake kisiasa siyo kuzidi kumjengea uwezo? Pumbaveu kweli wekli nyinyi majitu.

Pelekeni majizi mahakamani ili atakapohukumiwa na impact yake kisiasa inaisha.

Mnafanya mambo kipumbavue utafikiri taifa lote la majuha.

Wewe ni menzako wote wenye akili kama zako ni mapumbavue kweli. Hakuan mtu wenye kichwa chake atareason kama wewe hapa. Pumbavue kweliwlei.
 
...Hivi ule wimbo wa mahakama ya mafisadi uliishia Wapi?
Ukitaka chombo kama Mahakama kiendeshwe kwa mihemko kama yako wengi hamtasalimika, mtalia na kusaga meno zaidi ya mnavyolia sasa, saa ingine mjitahidi kushirikisha ubongo ktk tafakuri zenu kabla hamjadhihirisha uvundo ulio vifuani mwenu..
 
View attachment 499376

Ikiwa siku chache baada ya dr Mwakyembe kudai Lowasa ni muhusika mkuu wa Richmond na hachomoki waziri mkuu huyo wa zamani amjibu.

Lowasa amedai kama ana udhibitisho inatakiwa aende mahakamani sio bungeni na kwenye majukwaa ya siasa ili ubishi uishe.

Ila Lowasa akamkumbusha ukweli unajulikana hadi kwa watanzania waliompigia kura wanajua muhusika mkuu wa Richmond ni nani.

Na Mnyika adai Kikwete nae ajiandae kuja kuijibia Richmond na aiomba serikali na bunge wapeleke mswada wa kumwondolea rais kinga.

Maoni:
Waziri mkuu najua hasaini mikataba ila ni msimamizi wa serikali bungeni na wala sio mwenyekiti wa baraza la mawaziri ila Rais ndo mwenyekiti. Hii issue la msingi ni kuipeleka mahakama ya mafisadi ilianzishwa kwa nini?
Mwakyembe hawazi kuwa serikali hiyo anayoitetea ndio hiyo hiyo iliyisabsbisha mwili wake mpaka leo uwe vile. Kimsingi ameshaiwa umaarufu baada ya kuwa M/kiti wa Kamati ya bunge kuchunguza sakata la Richmond.

Bahati mbaya anaemzunguzia kuwa ni Lowassa alibugi step maana mahakama imeshatoa hukumu juzi kati hapo kuwa Mhusika Mkuu wa Richmond ameshinda kesi, ameishinda serikali na sikusikia kama ni Lowassa.

Kuondoa ubishi, kwakuwa mahakama ya mafisadi IPO, wapeleke mahakamani hiyo kesi, Marais wastaafu waondolewe kinga, kazi ianze muone kama watu hawaishi Jela.

Aache Porojo Mwakyembe, umaarufu wake umeshakwisha, ukiwa PhD holder halafu unaanza kujipendekeza lazima upotee.
 
Tutaongea na kuandika yote lakini jibu ni mahakama kwani ugumu uko wapi wakati vyombo vyote vipo chini ya chama tawala. Kwanza Watanzania wameshazichoka hizi ngonjera ambazo watawala hawataki kueleza ukweli wake zaidi ya kumbambikia mtu tuhuma kwa vinywa vyao wakati mahakama zipo
 
Kwenye sakata hili lowasa amlaum nasari kwa kulianzisha tena. Lengo la nasari kuizungumza Richard Mond analijua yeye na baadhi ya wanacdm team Dr Slaa.
 
Acha upumbavu wewe.

Kumvumilia mtu mwizi kwa kuogopa impacts zake kisiasa siyo kuzidi kumjengea uwezo? Pumbaveu kweli wekli nyinyi majitu.

Pelekeni majizi mahakamani ili atakapohukumiwa na impact yake kisiasa inaisha.

Mnafanya mambo kipumbavue utafikiri taifa lote la majuha.

Wewe ni menzako wote wenye akili kama zako ni mapumbavue kweli. Hakuan mtu wenye kichwa chake atareason kama wewe hapa. Pumbavue kweliwlei.
Ni heri kuitwa Mpumbavu na wapumbavu kuliko kuwa Mpumbavu kwa upumbavu wa kutoona ufisadi wa Lowassa!!
 
Mitambo ya Richmond ni mradi wa mashirika ya kijasusi ya marekani ikiwamo CIA,mitambo hiyo baada "ilibadilishiwa jina" na kuitwa Symbion Power.

Marekani ana tabia ya kutojihusisha na miradi yenye harufu ya ufisadi,lakini mitambo ya Richmond(baadae symbion) ilitembelewa na Rais George Bush,Rais Obama,Condoleza Rice(nadhani) na pia mama Hillarly Rodham Clinton. Hii nadhani ilikuwa ni kuwapa ishara wapiga domo kwamba "kaeni mbali na hii kitu"

Obama alizindua mradi wa AfricaPower house wenye lengo la kusambaza umeme Afrika akiwa anaitazama mitambo ya Richmond(sasa symbion power)

Pia baada ya Lowasa kuondoka madarakani,bado serikali iliendelea na bado inaendelea kununua umeme wa symbion power na hakuna transaction wala kampuni inayoonyesha ilipokea au inapokea pesa kwa niaba ya Lowasa kutokana na umeme unaouzwa na symbion power.
Sisi Tanzania tunakuwa hatuijui dunia ya kitechnolojia, kisheria na kijasusi. Tunapaswa tukumbuke kwamba wenzetu wanaenda na mifumo inayopangiliwa kwa kipindi kirefu na huhusisha wataalamu ambapo si rahisi kugundulika .
Enzi za ukoloni, wamisionari walitumika sana, na bado wanaendelea.
Tehnolojia inatumika sana kuhakikisha wanafanya Yale ambayo sisi tukonayo gizani.
Siasa ni chambo, na Haya mataifa yaliyoendelea wanajua kwamba Afrika haina wanataaluma wa kugundua chochote. Hivyo wansiasa wanayumbishwa Kama matawi ya miti, na hakuna namna watajikwamua.
Mifumo ya utawala kwao walioendelea ni ya kupokezana vizuri. Sisi hatuwezi hata kupokezana madaraka kwani bado tunawaza "umimi, usisi, uwao, n.k.".
 
Serikali iache maneno. Buruza EL mahakamani tujuwe moja.... Ugumu uko wapi jamani?
Siyo rahisi, kuna tetemeko ambalo halijawahi kutokea Tanzania litabomoa nchi. Kuwepo kwa cheo kimoja siyo kwamba ndiyo utimilifu wa kukitumikia. Kuna kundi la watu wanaoambatana nacho. Mitambo bado inazalisha Umeme, mahamaka itabidi kwanza iombwe kwa dharura kusimamisha mitambo hiyo ili kesi ifanyike. Tutakuwa wendawazimu kufunguliana mashitaka wakati mitambo iko kazini. Je, hilo linawezekana? Kazi kwenu¡¡¡¡¡¡!!!!!!!
 
Serikali iache maneno. Buruza EL mahakamani tujuwe moja.... Ugumu uko wapi jamani?
Lowasa anastahili kuwa Rais wa Tanzania ili kukata mzizi wa fitina. Akiwa Rais kila kitu kitajulika. Lakini Ccm hivi walivyo madarakani, hakuna uwezekano wa wao kujibomoa
 
Hawa akina mwakyembe fafafafafa wote wananishangaza sana, wanasema hakuhitajika lowassa kuhojiwa maana ushahidi ulitosheleza. Kama ndivyo sasa mwalimu mzima wa sheria anataka kupeleka shauri bungeni badala ya ushahidi wake kuisaidia serikali kwenye mahakama ya mafisadi!!!?????
Hizo ni mbwembwe za watu waliofeli mambo yao. Nchi niko hoi, watu walio madarakani mbele giza.
Hukusikia juzi tunaambiwa serikali haikusema itatoa elimu bure Bali elimu bila malipo?
 
Kwani waliouanzisha huu mjadala tena ni kina nani?? Nassari ndo kaanzisha mjadala, yuko kambi gani? sasa mnataka Mwakyembe akae kimya?? Eboh!!
Acha awape dozi tu!
Hapa wanazuga ili kuvuruga mindset za watu bajeti ipite kiaina tuu
 
Hivi mwakiye hamna focus ya wapi mnaipeleka nchi unazungumzia ya Edo wakati hayo yeshapita na yeye alisema kama issue ni uqaziri mkuu basi anaachia ngazi. Wewe unarudisha mavi tumboni wakati yapo chhooni tayari. Edo aligombea uraisi na hakuna chombo kilicho muwekea pingamizi. Wacha ubashite ama nawe udocta wako ni wakale kabla ya kupata brain tumor. Unatuchosha kwa uzandiki wako kaa kimya.
 
Kuhusu kauli ya Mnyika namuunga mkono na ndio maana hata mimi nilileta huu uzi hapa chini:

Hoja ya kurudisha Bungeni sakata la Richmond iende sambamba na kuondoa kinga ya Rais

Ukweli ni kwamba ukipitia taarifa ya kamati ya Mwakyembe mwanzo mwisho huwezi kuamini kuwa yote yale yalifanyika bila bwana fulanj kujua.Ni mwendawazimu pekee ndio atakaeamini hivyo.

Mtu mwenye akili lazima ujiulize maswali haya 9 yafuatayo hapa chini:

1.Kwanini Lowassa hakuhojiwa?

2.Lowassa angehojiwa na katika kujittetea unadhani angemtaja nani?

3.Na kama angetaja mtu/watu katika kujitetea,unadhani angetaja wa chini yake tu bila kumtaja bwana fulani?

4.Je,unadhani Mwakyembe na kamati yake hawakujua hatari ya kumuhoji Lowassa?

5.Kama wangemuhoji Lowassa, unadhani Mwakyembe na timu yake walikuwa tayari kumtaja(kumu-implicate) mh.sana wa wakati huo katika taarifa yao walioiwasilisha Bungeni?

6.Wangemtaja mh.sana wa wakati huo katika ripoti yao,unadhani nini kingefuata?

7.Unadhani Lowassa nae angeweza kueleza kila kitu mbele ya Bunge kabla ya kujiuzulu?

8.Na yeye kama angeeleza ukweli wote anaoujua,unadhani nini kingefuata?

9.Unadhani angeondoka Lowassa peke yake bila fulani kuingia matatani?

Haya mambo yanawezekana tu katika nchi za wenzetu na sio huku kwetu tunakowaona kina fulani kama miungu watu.

Tuache kupotezeana muda na kudanganyana.

Namb 4 ndo umefunga mjadala wa mnafiki hharison.
 
Back
Top Bottom