Sakata la pandora papers liifundishe serikali kuwa na uwazi na matumizi mazuri ya fedha za umma

chase amante

JF-Expert Member
Feb 24, 2018
5,540
2,069
Habarini,

Jumapili kuliibuka sakata la pandora papers report ambayo iliibua akaunti za fedha za nje za viongozi na watu matajiri duniani akiwepo Tony blair,rais uhuru kenyatta n.k

Kua na akaunti nje ya nchi sio kosa ,ila kosa ni kua kodi inashindwa kulipwa kwa nchi zile walizopo wamiliki kutokana na akaunti hizo.pia uwazi wa hizo fedha na jinsi zilivyopatikana unakua ni mdogo kwa umma japo ni fedha za watu binafsi.

Tanzania kuna viongozi wamenza kutumia fedha za umma vibaya,mfano ni waziri mkuu kukodi ndege binafsi wakati za serikali zipo.haya mambo yakiendelea yatapelekea kupungua uaminifu kwa wananchi dhidi yao,na pengine na wao wanaweza pia kuanza rushwa na kufungua akaunti za fedha nje ya nchi bila uwazi wa mali zao kufahamika na watu.

Ni tahadhari tu na naamini tanzania tutakwenda vizuri mbeleni.
 
Sijui kwanini sisi 1 % tunaandamwa sana siyo kwa wamatumbi ama wazungu. Kwani kuwa tajiri ni dhambi? Mtuache bana tule hela zetu kwa amani.
 
Crypto currencies zikiwa rasmi, wizi utashamiri sana maana hakuna wa kuzidhibiti - itakuwa another pandora papers.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom