Sakata la nyara za Serikali: Kada wa Kikwete lawamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la nyara za Serikali: Kada wa Kikwete lawamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Sep 13, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,408
  Likes Received: 81,442
  Trophy Points: 280
  Na Mwandishi Wetu
  MwanaHALISI

  KAMPUNI ya uwakala iliyosafirisha kontena lililokuwa na meno ya tembo ambayo yalikamatwa nchini Vietnam, inamilikiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya CCM, Abdulrahman Kinana, imefahamika.
  Taarifa zinaonyesha kuwa Kinana anamiliki hisa 7,500 kati ya 10,000 za kampuni hiyo inayoitwa Sharaf Shipping Company iliyosajiliwa Dar es Salaam.
  Mshirika mwenzake katika kampuni hiyo, Rahma Hussen anamiliki hisa 2,500 zenye thamani ya shilingi 1,000 kila moja.
  Kwamujibu wa taarifa za usajili, wamiliki wote wawili, Kinana na Rahma wanapatikana kwa S.L.P 10910, Kiwanja Na. 403 Mtaa wa Tosamaganga, Msasani Peninsular, Dar es Salaam.
  Nyaraka zilizopo katika ofisi ya Wakala wa Usajili wa Makampuni na Biashara (BRELA), zinaonyesha kuwa kampuni ya Kinana ilisajiliwa Oktoba 2003 na kupewa hati Na. 47221.
  Sakata la kukamatwa kwa nyara hizo za serikali zilizosafirishwa na kampuni ya Sharaf Shipping Agency liliibuliwa bungeni kwa mara ya kwanza na mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela.
  Hati ya kusafirisha makontena hayo mawili yaliyokuwa yamesheheni pembe za ndovu ilisainiwa na mfanyakazi mwenye asili ya India wa kampuni hiyo Samir Hemani.
  Nyaraka zote zilionyesha kuwa kilichokuwa ndani ni plastiki zilizorudufiwa, wakati baada ya makontena kukamatwa, walikuta yamesheheni pembe za ndovu.
  Taarifa zinasema kibali cha kusafirishwa kontena hilo kilisainiwa 13 Novemba 2008 na Meneja wa Fedha na Utawala wa Kampuni hiyo.
  Wakati Hemani anasaini nyaraka hizo, kibali chake cha kuishi nchini tayari kilikuwa kimeshaisha. Kibali cha Hemani kiliisha 7 Mei 2008.
  Makontena yalikamtwa nchini China yakisafirishwa kwenda Hong Kong.
  Akichangia makadirio ya bajeti ya wizara ya Maliasili na Utalii ya mwaka 2009/2010, Kilango alisema utafiti wake umeonyesha kuwa makontena hayo yalipitia bandari ya Dar es Salaam na nyaraka zinaonyesha ndani kulikuwa na plastiki.
  Kilango alisema nchi zinazoongoza kwa kupokea nyara kutoka Tanzania ni Phillipines, China, Singapore na Hong Kong.

  Kutokana na kutopatikana kwa Kinana juzi kuzungumzia suala hilo, haikufahamika iwapo kampuni ya spika huyo wa zamani wa Afrika Mashariki au yeye mwenyewe, walijua kilichokuwamo katika makontena hayo. Lakini afisa mwandamizi katika wizara ya Viwanda na Biashara alisema kazi ya kukagua kilichomo kwenye kontena linalosafirishwa si ya wakala wa meli kwani wenye mamlaka na idhini ya kufanya hivyo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
  Alisema wanaowajibika kusitisha mzigo kusafirishwa pindi wanapoutilia mashaka ni TRA.
  "TRA ndio wanakagua na baada ya kujiridhisha kama kilichomo ndani ndicho kilichotamkwa kwenye nyaraka na ni halali, ndipo wanaweka muhuri (seal) wa mwisho," alisema afisa huyo.
  "Ukitamka kwa mfano, kuwa katika nyaraka ndani ya kontena kuna matairi 40 ya magari, lazima TRA wafungue na kukagua kuona kama kweli yako matairi 40 au kitu kingine. Baada ya hapo wanaweka seal; sasa kuna kila sababu ya kujenga mashaka," alieleza.
  Alisema, "Wakala wa meli kazi yake ni kusafirisha mzigo wa mteja wake. Hata mteja akija na kontena tupu na kusema anataka liende nchi fulani, kazi yake ni kulipeleka kunakohusika na si kuhoji kilichomo."
  Alifafanua kuwa watu muhimu wa kuhojiwa na ambao wanaweza kuwa wanajua mchezo wote, kama upo, ni wafanyakazi wa TRA.
  Hadi juzi Jumatatu hakukuwa na taarifa zozote za maofisa wa TRA kuhojiwa kuhusiana na sakata hilo.
   
  Last edited: Sep 14, 2009
 2. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Good job Mwanahalisi.
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hahahahahh JK ni mnafiki sawa na kabla jogoo hajawika ukweli huo . NO wonder kawekwa kamati ya kuwajua wambunge na moto wao bungeni .
   
 4. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hapa Mwanahalisi wamemkoma nyani kisawasawa...magazeti mengine uchwara wangezungusha kumtaja Kinana..Well done.
   
 5. Nkamu

  Nkamu JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 206
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ni jambo la kusikitisha kama sio kutia aibu kwa mtu ambaye anaonekana msafi na mwenye busara katika CCM kushiriki katika biashara hii haramu! Hii inathibitisha kuwa Mungu ameichoka CCM anataka kuitowesha kabisa katika ulimwengu wa Tanzania. Hongera sana Mwanahalisi kwa kuwapigania watanzania nasi watanzania tuache kulalama tufanye kweli kuuondoa uozo huu wa CCM! MUNGU IBARIKI TANZANIA
   
Loading...