Sakata la Nyamongo Radio Free Afrika(RFA) kuomba radhi !

Rutunga M

JF-Expert Member
Mar 16, 2009
1,769
1,382
Taarifa za hivi Punde kutoka News room ya RFA ni kuwa kituo cha redio Free Afrika kilichoko Mwanza,Tanzania kitaomba radhi kwa kutangaza habari ya uongo dhidi ya waandishi wa Habari na Mbunge wa CHADEMA kwamba walikamatwa na Polisi kwa kuingia katika eneo la mgogoro baada ya polisi kuwapiga risasi wananchi 4 huko Tarime.
Habari hiyo waliirusha katika taarifa ya Habari na kuwekwa katika mtandao wa internet lakini imegundulika kuwa ni uongo mtupu,kuwa mwandishi aliyeandika alikuwa na visa na wahusika.
HABARI YENEWE NI HII Au chini
WAANDISHI wa habari wanne, wabunge wawili na watu wengine kadhaa wamekamatwa na Jeshi la Polisi wakituhumiwa kuzuia uchukuaji na mazishi ya miili ya watu wanne waliouawa kwa kupigwa risasi na askari polisi katika Wilaya ya Tarime, mkoani Mara.

Kwa mujibu wa habari zilizothibitishwa na Jeshi la Polisi, waandishi wa habari waliokamatwa ni Anthony Mayunga wa Mwananchi, Beldina Nyakeke wa The Citizen, Anna Moroso wa Nipashe na Mabere Makubi wa Channel ten.

Wabunge waliokamatwa ni Bw. Tundu Lissu (Chadema) wa Singida na Bi. Ester Matiko (Chaema) wa Viti Maalumu Mkoa wa Mara.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Constantine Massawe amesema wanahabari hao, Mbunge Ester Matiko na watu wengine kadhaa wakiwamo wanaodaiwa kuwa ndugu wa marehemu wamekamatwa leo asubuhi katika kijiji cha Nyakunguru wilayani Tarime.

Kamanda Massawe amesema wamekamatwa kwa tuhuma za kushawishi ndugu wasizike miili ya ndugu zao na kuchochea uvunjifu wa amani.

Aidha, amesema kuwa Mbunge Lissu na watu wengine saba wamekamatwa na polisi jana saa tatu usiku mjini Tarime kwa tuhuma za kuzuia ndugu wa marehemu kuchukua miili ya watu wanne iliyokuwa imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime kwa muda wa siku 13.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, Mbunge Lissu na watu wengine saba walikuwa wanasubiri maandalizi ya kufikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime leo kujibu tuhuma zinazowakabili.

Akizungumza na Radio Free Africa kwa njia ya simu kutoka kituo cha polisi cha Nyamwaga ambako yeye na wenzake walishikiliwa kwa ajili ya kuhojiwa, mwandishi Mayunga amesema wamekamatwa wakiwa kwenye gari ambalo waliomba lifti kwenda katika mji mdogo wa Nyamongo, Tarime na baadaye mjini Mugumu, wilayani Serengeti.


Jeshi la Polisi limethibitisha kuchukua na kusindikiza miili ya marehemu hao jana usiku kwenda katika miji ya ndugu husika kwa ajili ya mazishi.
Lakini habari ambazo hazijathibitishwa zinadai kuwa jeshi hilo limechukua miili ya marehemu hao kwa siri kutoka chumba cha maiti na kwenda kuitelekeza jirani na miji ya ndugu husika jana usiku.

Tukio la kukamatwa kwa wanahabari hao limekuja siku moja baada ya Jeshi la Polisi kupiga marufuku mkusanyiko wa watu uliokuwa imeitishwa na baadhi ya viongozi wa Chadema kwa ajili ya kuendesha ibada na kutoa heshima za mwisho kwa miili ya marehemu hao.

Mkusanyiko huo ulipangwa kufanyika jana kati ya saa tatu na saa nne asubuhi kwenye uwanjwa wa mpira wa miguu mjini Tarime, na kwamba baada ya hapo miili ya marehemu hao ingesafirishwa kwenda katika vijiji husika kwa ajili ya mazishi.

Jeshi la Polisi lilitoa sababu ya kuzuia mkusanyiko huo kuwa ni kuepusha kuchochea hasira na uvunjifu wa amani miongoni mwa wananchi wilayani Tarime.

Marehemu hao ni Chacha Ngoka mkazi wa kijiji cha Kewanja, Emmanuel Magige mkazi wa kijiji cha Nyakunguru, Chacha Gwasi (ameshazikwa) mkazi wa kijiji cha Bisarwi, wilayani Tarime, Chawali Bhoke na Mwikwabe Marwa wakazi wa Mugumu, wilayani Serengeti. Mwili wa Gwasi ulichukuliwa na ndugu na kuzikwa Mei 18, mwaka huu.

Waliuawa kwa kupigwa risasi na askari polisi alfajiri ya Mei 16, mwaka huu, wakituhumiwa kuvamia na kujaribu kupora mawe yenye dhahabu katika Mgodi wa Dhahabu wa North Mara (NMGM) unaomilikiwa na kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick Gold (ABG).

Mazishi ya miili ya marehemu hao yalicheleweshwa baada ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutaka miili hiyo ifanyiwe uchunguzi wa kina mbele ya usimamizi wa wanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu na Mabere Marando.

Uchunguzi huo umefanyika Mei 23, mwaka huu na kuamriwa kuwa miili hiyo isafirishwe kwenda vijiji husika Mei 24, mwaka huu, kwa ajili ya mazishi.
 
Back
Top Bottom