Mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri aliyofanya Rais jana hayakuwa na uharaka wowote, badala ya kuonekana ni mabadiliko ya kawaida yameonekana kama yamefanywa kuonyesha yeye ni nani. Zaidi yamemchora rais kama ni mtu wa aina gani, mtu wa jazba, asiye na ustahimilivu, mtu mwenye pupa, anayelipiza kisasi na mwenye upendeleo fulani.
Baada ya Nape kupokea ripoti ya tume aliyounda hata kama Rais hakufurahishwa alitakiwa kwanza kutulia, kwa vile ripoti ilikuwa ipelekwe kwake alikuwa na uwezo wa kuonyesha hisia zake kwa kuitupilia mbali kuliko kuonyesha hisia zake kwa kumtumbua Nape ndani ya masaa 12 baada ya ripoti kukabidhiwa.
Kitu kingine ambacho rais angefanya bila kuonyesha chuki kwa mtu mmoja, angesubiri muda aliopanga kufanya mabadiliko ya jumla kwenye baadhi ya wizara kama tulivyokuwa tunatarajia na kumtoa mtu asiyemtaka, lakini kubadili baraza ghafula kwa ajili ya mtu mmoja na wengine kuteuliwa pengine kabla ya kuapishwa kuwa wabunge kamili kinachukuliwa kama kitendo cha ku panic, na kiongozi mkubwa namna hii hatakiwi kutenda mambo wakati akiwa na ghadhabu.