Crashwise
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 22,227
- 8,739
Jamani oneni tunavyo aibika
Kama taarifa nilizoziona kwenye moja ya majukwaa ya kijamii kuhusu wana habari Arusha na RC ni kweli kwamba RC Gambo kamuombea radhi DC wa Arumeru kwa kuamuru kuswekwa rumande kwa Mwandishi wa ITV na Radio One, Halfan Liundi na kutoa pikipiki mbili kwa chama cha waandishi wa habari Arusha (APC), basi tuna safari ndefu katika harakati za kukataa ukandamizaji na matumizi mabaya ya waliokabidhiwa dhamana ya uongozi dhidi ya wananchi wanyonge wasio na uwezo wa kujitetea.
Kama ni kweli najiuliza maswali kadhaa:-
1. kwanini ambaye hajatenda kosa aombe radhi wakati mhusika yupo.
2. Najiuliza wakati RC anaomba radhi DC mhusika naye alikuwepo?
3. Kama hakuwepo hiyo radhi ni ya RC au DC?
4. Je, DC mwenyewe ameona na kujutia kosa linaloombewa radhi?
5. Papo hapo najiuliza pikipiki ni za nini kwenye kikao cha kuombana radhi?
6. Ni faini kwa kosa lililotendeka au ilikuwa kwenye ratiba na mpango wa RC kuwasaidia wana habari na bahati mbaya au nzuri imeangukia kwenye kikao cha kuombana radhi.?
7. Hivi kwanini RC hakuona busara ya kupanga siku nyingine kwa shughuli hiyo kupisha vumbi la mkwaruzano kati ya kada tawala na want habari litulie?
8. Najiuliza iwapo hii siyo kishawishi (sisemi rushwa), kwa waandishi?.
Mwenyekiti wa APC na baadhi ya wanachama wamo humu, wajitokeze watusaidie kujibu baadhi ya maswali kuondoa ukungu ulioanza kutanda.
***Kilichofata ni watu kuanza kuondolewa kwenye kundi la APC