Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Wadau hii imekaaje?

Nilikuwa nangalia vipindi vya maombolezo kupitia tivi ya taifa.

Sasa mbona maombolezo haya yamekaa kikristu kristu zaidi?

Wanyarwanda na nyimbo zao wanafunika.


Najua wapo watakaokuja kuniponda kwa ukweli niliouona.

Nipo tayari kukosolewa.
 
Hiki kivuko kikiibuliwa na kukarabatiwa kisitumiwe tena na raia kikabidhiwe jeshini ili kiwe kifaa cha kijeshi, wananchi tusikijadili tena chenyewe na huu mkasa
 
"Ndugu zangu mimi nilikuwepo ndani ya kivuko kile cha MV NYERERE,tumepona tu kwa sababu tulikuwa nje,waliokaa ndani ni ngumu sana kupona kwakuwa kivuko kiligeuka gafla chini juu na kina uzito,
mtu ukifunikwa vile ata waokozi wakifika ndani ya robo saa kukuta bado mzima ni ngumu sana.
Kama hauamini na unazani masihara jaribu kuzama ndani ya pipa la maji kwa dakika 10 bila kupumua uone.
Mimi naomba wale waliozidisha abiria na uzito wakamatwe kama Mhe Rais alivyosema
na sisi abiria tujiongeze
Tukifika standi kwenye basi ama bandarini tuwe tunauliza, je hiki kivuko kina beba watu wangapi ?
na huo uzito ubandikwe kwenye mbao za matangazo,ukiona watu wamezidi usipande ila wa afrika sisi tunalazimisha na wengine tunatoa rushwa ili turuhusiwe kupanda madhara ndio haya,
ni ngumu sana kupona ukifunikwa vile ata kama baada ya dakika 10 kivuko kinge ondolewa majini lazima maiti zingekuwa nyingi sana,
watu waangalie ata Marekani boat ili wahi kuzama kwa kugeuka tu watu 17 wakaaga dunia,,waokozi wanafika wakakuta tayari na wenzetu wameendelea sana lakini kifo cha maji kinaua haraka hasa kama mtu unakuwa umefunikwa kama hawa walikuwa ndani.

Hiki kivuko kime karabatiwa mwaka jana na kote huko kimeenda vizuri tu tunakaribia kupaki watu wa ndani wanagombea kutoka nje

kwa kuwa watu walizidishwa uzito ukaenda sehemu moja kikageuka wajuu tukarushwa kwenye maji ndio pona yetu, wavuvi jirani wakaja kutuokoa,,walipoingia ndani ya kivuko kwa chini mda ule ule wakakuta watu washakufa kwa kukosa hewa sasa watu wasilaumu tu bila kujua.
nawaambia usiombe kufunikwa na kivuko, Sikia tu kwenye mitandao...fikisha salam mimi

John Kisekwa.
Pole sana mkuu. Nayahisi maumivu muliyoyapitia.
 
duu inasikitisha sana ndio naamin kuwa kuna watu wengi wangepewa msaada mwanzo wa tukio wangeweza kuokolewa yan uzembemkubwa sana ulitumika kwenye tukio hili.
 
meli kupinduka ilikuwa mipango ya Mungu, ila vifo vingi vilikuwa kwa mapenzi ya serikali yetu.
Ni akili finyu na mbovu za mwenye jukumu la ulinzi na usalama wa mkoa husika, ndiye wa kunyooshea kidole kuhusu idadi ndogo ya waliookolewa wakiwa hai.
 
Ila mm hii nimeshindwa kuimeza asee maana kuna sehemu alikuwepo kulikua na hewa ya oxygen aliweza kupumua kwa izo siku3 jmn
 
Mongela you need to be proactive.
Ungeanza kujipanga mapema na mahema. Majenereta. Bulbu.fedha kidogo na chakula kwa waokoaji. Huyu aliyeokolewa hai leo angetoka na wengine wengi wasio na hatia.
Mongela alifika eneo na tukio na smart phone minus washauri wake na hakua na mkakati wowote zaidi ya kupigwa picha.
 
Back
Top Bottom