Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Si pingi kwa ubaya Ila kwa kuepusha mabaya..

Enyi watanzania.. kweli mimi naunga mkono wachache ambao wanapinga uchangiaji wa rambirambi kwaajili ya ajari mbaya iliyotufika watanzania wote kwa ujumla wetu .

Sababu mpaka sasa hakuna taarifa zilizo weza kuthibitisha ni watu wangapi walio kuemo katika meli(kivuko) #hivyo familia zinazo passwa kuhaniwa ni unknown

Pili imekua kamchezo wananchi kutoa rambirambi Na rambirambi kupelekwa kusiko julikana
#yalinihuzunisha yaliyotokea kwenye maombolezo ya wadogo zetu *wa kwa mgambo the don. Wa A. Town*

Tatu.. still hakuna muongozo wowote ulioafikiwa wa kuweza kuzitambua familia zilizo patwa Na misiba


It's too early for that watanzania msije pigwa mkaambiwa pesa hazijulikami zilikoenda

Nawasilisha ..
Labda nikutane na mfiwa nitampa ,Lakini kwenye bakuli La Magufuli sitoi hat a senti
 
We ndugu

Mbowe alimtaka Rais aongee na sio Msigwa Kutoa Twite kwamba Rais amesikitishwa hatimaye Rais kazungumza, je ndio kuvuliwa nguo huko?

Pili lawama kwa serikali haiepukiki kwa sababu zilizo wazi. Moja ndio yenye jeshi la uokozi sio vyama vya siasa. Pili serikali ndio mmiliki wa kivuko, tatu serikali kupitia Sumatra ndio mkaguzi maswala ya usalama wa vyombo vya usafiri na mwisho ndio operator wa kivuko hicho sasa lawama apewe nani?

Tumeona wavuvi ndio wamefanya kazi ya uokozi na uopoaji wa maiti je jeshi letu la uokozi lipo wapi inafika usiku wanasimamisha kazi ilihali watu bado wamenasa ndani ya meli.

Kwa muktadha huo huoni aibu kwa uliyoyaandika. Tusifie pale panapostahili na tukosoe pale inapohitajika. Sio kila kitu kusifia natamani upate janga kama hilo ndio akili ikukae vizuri.

Roho za marehemu wote waliokufa kwenye ajali Mungu azipe pumziko la milele
Ulikuwepo eneo la tukio?
 
Ndugu zangu mimi nilikuwepo ndani ya kivuko kile cha MV NYERERE,tumepona tu kwa sababu tulikuwa nje,waliokaa ndani ni ngumu sana kupona kwakuwa kivuko kiligeuka gafla chini juu na kina uzito,
mtu ukifunikwa vile ata waokozi wakifika ndani ya robo saa kukuta bado mzima ni ngumu sana.
Kama hauamini na unazani masihara jaribu kuzama ndani ya pipa la maji kwa dakika 10 bila kupumua uone.
Mimi naomba wale waliozidisha abiria na uzito wakamatwe kama Mhe Rais alivyosema
na sisi abiria tujiongeze
Tukifika standi kwenye basi ama bandarini tuwe tunauliza, je hiki kivuko kina beba watu wangapi ?
na huo uzito ubandikwe kwenye mbao za matangazo,ukiona watu wamezidi usipande ila wa afrika sisi tunalazimisha na wengine tunatoa rushwa ili turuhusiwe kupanda madhara ndio haya,
ni ngumu sana kupona ukifunikwa vile ata kama baada ya dakika 10 kivuko kinge ondolewa majini lazima maiti zingekuwa nyingi sana,
watu waangalie ata Marekani boat ili wahi kuzama kwa kugeuka tu watu 17 wakaaga dunia,,waokozi wanafika wakakuta tayari na wenzetu wameendelea sana lakini kifo cha maji kinaua haraka hasa kama mtu unakuwa umefunikwa kama hawa walikuwa ndani.

Hiki kivuko kime karabatiwa mwaka jana na kote huko kimeenda vizuri tu tunakaribia kupaki watu wa ndani wanagombea kutoka nje

kwa kuwa watu walizidishwa uzito ukaenda sehemu moja kikageuka wajuu tukarushwa kwenye maji ndio pona yetu, wavuvi jirani wakaja kutuokoa,,walipoingia ndani ya kivuko kwa chini mda ule ule wakakuta watu washakufa kwa kukosa hewa sasa watu wasilaumu tu bila kujua.
nawaambia usiombe kufunikwa na kivuko, Sikia tu kwenye mitandao.......

mimi John Kisekwa..."
pole sana mkuu kuanzia leo usikose kanisani maana umepata nafasi ya pili
 
Kazi ya Mungu Wakuu huwa haina makosa wale ndugu zetu waliofariki ni kwasababu ya mda wao wakuishi hapa duniani ulifikia mwisho
 
Wewe ni zaidi ya kilaza mkubwa unabishana kama zuzu au kichaa wakati hiyo hotuba ya mbunge wa ukerewe bungeni ipo na clip yake ipo,wacheni masihara kwenye msiba mkubwa kiasi hiki
Mbwiga anachosema mbunge ni kwamba hoja take ilifanyiwa kazi na kivuko kilitengenezwa......KUB Mbowe anasema hoja ya mbunge haikusikilizwa. Use unaelewa mkuu machale
 
Vifo vya kujitakia kwa uzembe wa serikali..

Gharama ya kivuko kama cha Magogoni maximumly ni 10Bil..

Tumeshafanya chaguzi za marudio za KIJINGA kabisa ambazo wabunge wameamua wenyewe kujiuzulu then hao hao wakagombea tena na wakashinda na zimeshagharimu 60Bil mpaka sasa..

Hii pesa ingetosha kununua vivuko 6 vipya na kusambazwa kwenye sehemu mbalimbali na kuondokana hata na hii ajali ya juzi.

Acha pesa mabilioni ambazo zimeshatumika kuwanunua wabunge na madiwani wa upinzani halafu mtu anakwambia yeye yupo kwa ajili ya wanyonge wa nchi hii..

Serikali ya ovyo kabisa isiyojali wananchi wake.
ungefiwa na ndgu au rafiki ingekuuma sana na usingeliweka kisiasa
 
Hii Habari Moderate Ifatilieni Haraka Tujue Ukweli Wake
Mungu Ni Mwema Wakati Wote
 
HAPO WA KULAUMIWA NI @SUMATRA..Hao polisi TRA,hayo sio mamlaka yao,,kama polisi,kitengo cha Marine wao wanasubiri order tu kutoka Sumatra.
 
Back
Top Bottom