Sakata la Msondo Ngoma: BASATA yawashukia WCB wasema ukitumia kazi ya mtu bila utaratibu hiyo moja kwa moja ni kosa

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Baada ya Band ya Msondo Ngoma kutaka ilipwe shilingi milioni 300 na kundi la WCB kwa kutumia bila ruhusa vionjo vya wimbo wake kwenye wimbo wa “Zilipendwa” Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Mngereza ameongea yafuatayo.

“Unaweza kuitazama katika mitizamo mbalimbali lakini unapoangalia kwamba wanaanza kushtakiana kimsingi ni taratibu ambayo inagusa sana mambo ya haki miliki, kabla ya kuitumia kazi ya mtu ni vizuri ukamuona mwenye kazi mkubaliane” AMEONGEZA NA KUSEMA

“Ukitumia kazi ya mtu bila utaratibu hiyo moja kwa moja ni kosa, cha msingi hata kabla ya kumuweka Mwanasheria ili kudai haki yako ni vizuri ukawafata au ukawasiliana na alietumia kazi yako bila ruhusa…. katika hili linalojitokeza sasa hivi ni swala la kuamshana kwamba kazi ya sanaa ya mtu flani haina tofauti na mali ya mtu ya aina nyingine, huwezi kutumia gari la mtu bila ridhaa yake” – Mngereza
 
Ametoa mtizamo wa jumla...ila hajaingia ndani zaidi katika kuchambua mtizamo wa sheria katika Haki Miliki...yaani ni wakati gani tutasema hapa hakimiliki ya mtu imevunjwa?!

huyo jamaa inaonekana mweupe kidogo linapokuja suala la copyright laws au lbd alikuwa anaona uvivu tu kuchambua kiundani hiyo ishu ya Msondo na WCB ambapo kimsingi kwa jicho la Sheria hakuna uvunjifu wa hakimiliki uliofanywa na WCB kwa hicho kionjo walichokitumia.

Watu inabidi wajipe muda wa kusoma kabla ya kuconclude hasa kama jambo husika linahusu sheria.
 
Swali wametumia au hawajatumia?
 
Unajua buana, ukila hata kama hukushiba ni umekula tu.

Kama ulikuwa kwenye swaumu inakuwa umeshafungulia teali.

Aiyaaaaaaaa...!
 
Ametoa mtizamo wa jumla...ila hajaingia ndani zaidi katika kuchambua mtizamo wa sheria katika Haki Miliki...yaani ni wakati gani tutasema hapa hakimiliki ya mtu imevunjwa?!

huyo jamaa inaonekana mweupe kidogo linapokuja suala la copyright laws au lbd alikuwa anaona uvivu tu kuchambua kiundani hiyo ishu ya Msondo na WCB ambapo kimsingi kwa jicho la Sheria hakuna uvunjifu wa hakimiliki uliofanywa na WCB kwa hicho kionjo walichokitumia.

Watu inabidi wajipe muda wa kusoma kabla ya kuconclude hasa kama jambo husika linahusu sheria.
Kwa hiyo na wewe umeona uvivu au? Mbona mimi ndio sijakuelewa kabisa
 
Ametoa mtizamo wa jumla...ila hajaingia ndani zaidi katika kuchambua mtizamo wa sheria katika Haki Miliki...yaani ni wakati gani tutasema hapa hakimiliki ya mtu imevunjwa?!

huyo jamaa inaonekana mweupe kidogo linapokuja suala la copyright laws au lbd alikuwa anaona uvivu tu kuchambua kiundani hiyo ishu ya Msondo na WCB ambapo kimsingi kwa jicho la Sheria hakuna uvunjifu wa hakimiliki uliofanywa na WCB kwa hicho kionjo walichokitumia.

Watu inabidi wajipe muda wa kusoma kabla ya kuconclude hasa kama jambo husika linahusu sheria.
Timu wcb nakuona haukubali ukweli hata kidogo
 
Mkuu upo sahihi!
Niliwahi kuelezea Sheria inavyosema juu ya jambo hili, walikuja wale wa team nyingine, ilikua hatari!
 
Tatizo watu wanapenda kuhitimisha mambo kwa kufuata mihemko na matamanio ya nafsi zao,kuliko kutafuta uhalisia wa jambo fulani kwanza...hili ndo tatizo la watz.
 
Back
Top Bottom