Sakata la mifugo ya Jirani: Serikali kupiga mnada Ng'ombe zaidi ya 10,000 toka Uganda na Rwanda

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,927
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ametangaza kupiga mnada ng'ombe zaidi ya 10,000 wa nchi za Uganda na Rwanda waliokamatwa katika operesheni inayoendelea nchini.

Mpina alitangaza hayo leo Jumatatu bungeni mjini Dodoma wakati akichangia Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa 2018/2019.

Waziri huyo ambaye alikuwa akijibu hoja zilizoibuliwa na baadhi ya wabunge amesema ng'ombe hao watapigwa mnada wakati wowote kama ilivyofanya kwa ng'ombe 1,325 wa Kenya.

Amesema uhusiano wa Tanzania nchi nyingine washirika wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ni mzuri na akisisitiza hakuna ushirikano wa kihalifu.

Mpina amesema walioingiza ng'ombe hao ni wahalifu na wamevunja sheria za nchi na kutahadharisha wafugaji wa nchi jirani kufuata sheria wanapotaka kuingiza mifugo nchini.
 
Hili swala sidhani kama litatuacha salama Kidiplomasia na Nchi marafiki kutokana na taswira hasi inayojengeka!!
 
Hawa wasukuma sijui wanatupeleka wapi...well, wauze kweli ng'ombe wa Kagame tuone!
 
Hili swala sidhani kama litatuacha salama Kidiplomasia na Nchi marafiki kutokana na taswira hasi inayojengeka!!
Ni tatizo kubwa sana mbeleni, watu wanaoshughulika na sera zetu kwa nchi za nje na utengamano wawe makini sana! Intelijensia pia when it comes to covert ops.

Inaweza kuonekana ni jambo jema kwetu kwa sasa... Ila ikajakuwa ni jambo bora zaidi kwa "wengine" hapo baadae!
 
Wauze tu maana hakuna namna tena, hata kama machadema yatapinga maana tumeshayazoea.....pinga pinga
 
Nilisikiaga kuna watanzania waliuwawa kwa kupigwa risasi mto kagera na wauaji wakadai tunavua samaki kwny nchi yao hivyo sioni ubaya wa sisi kupiga mnada mifugo yao bila kuua yeyote kama walivyofanya wao
 
Wauze tu maana hakuna namna tena, hata kama machadema yatapinga maana tumeshayazoea.....pinga pinga

Wewe hakika ni mwendawazimu na hujitambui.
Hivi unajua hawa ng'ombe wanaokamatwa hovyohovyo bila maafikiano kuna siku watasababisha VITA ya watu na siyo NG'OMBE tena. Ng'ombe wote 10,000 wanaweza kufa mra moja na kusiwe na tatizo lakini sio binadamu...!!Kifo cha binadamu 1 kwa wenzetu ulaya ni jambo la kushughulikiwa kitaifa siyo kama hapa tunapoongozwa na malimbukeni fulani ambao hata mtu 1 akifa who cares? Watu wanaokotwa kwenye viroba, watu wanapotezwa lakini hakuna anayejali...!!!

Wewe na CCM yako endeleeni tu na huu uzezeta wa kucheza na AMANI lakini ipo siku kikiwaka ndipo mtajua CHADEMA wanasema nini kwa sasa..! Nduli Idd Amin alianza kama hivi kupuuza mambo madogo na kudai kateka na kutaifa eneo fulani lakini mwisho wake ilikuwa ni kufurushwa na kwenda kufia ughaibuni...!!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom