Sakata la Mengi na Rostam: Kumbe na TBC nao wamewekwa kiti moto!

ByaseL

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
2,225
247
Kama tulivyosikia wiki jana kwamba ITV waliitwa na Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) kujieleza kwa nini wasichukuliwe hatua kwa kurusha kipindi maalum 23 April 09 na kurudiwa tarehe 27 April 09. Katika kipindi hiki Bwana Mengi anatuhumiwa kuwakashifu watu watano akiwemo Mbunge wa Igunga Mhe. Rostam Aziz kuwa ni “Mafisadi Papa” kitendo ambacho TCRA inasema ni kwenda kinyume na kanuni za utangazaji. Katika Tangazo la kulipiwa (advertisement) kwenye ukurasa wa 7 wa Gazeti la The Citizen la leo tarehe 4 Juni 09 TCRA wamebainisha kwamba vile vile TBC nao waiitwa (kama ITV) kwenda TCRA kutoa maelezo kwa nini wasichukuliwe hatua kwa kurusha hotuba ya Mhe. Rostam Aziz (kama kipindi maalum) iliyomtuhumu Bwana Riginald Mengi kuwa ni “Fisadi Nyangumi”.

Vituo hivi viwili yaani ITV na TBC kwa kurusha vipindi hivi vilikiuka kanuni ya 5(f) na 5(h) za TCRA zinazokataza kutangaza mambo yanayoweza kuleta uchochezi, chuki .nk. Vile vile vituo hivi vilikiuka kanuni ya 22 ya TCRA inayoagiza vituo ya television kutangaza ratiba ya vipindi vyao kwenye magazeti kila siku na kuzingatia ratiba hivyo labda kama kuna jambo la dharula na lenye umuhimu kitaifa. Tangazo linasema ITV na TBC wote wametoa maelezo yao kwa TCRA tarehe 18 Mei 2009 na hatua zitachukuliwa kulingana na kanuni za TCRA.

Tangazo hili sasa linaonyesha kwamba TBC nayo huenda haikufuata maadili ya utangazaji tofauti na kauli ya Mtendaji Mkuu wa TBC, Bwana Tido Mhando ambaye alisema yeye kama mtangazaji wa siku nyingi wa BBC anaona kurushwa kwa kipindi maalum cha kulipiwa na Rostam Aziz ilikuwa ni sawa. Tusubiri uamuzi wa TCRA.
 
Mimi nahisi kuiweka TBC1 ni kuzugia tu, lengo ni ITV....wanapenda sana kutupiga sanaa hawa!
 
Hapo ni mchezo wa hide and seek tu. Anatafutwa Mengi hapo. Subiri tuone.
 
Nimeamini Mengi ananguvu maana kila anaemgusa basi yeye atashinda tu hata kama ukweli hauko anavyotaka yeye uwe. Sasa hebu fikiri mtu anaenda kanisani kujadili masuala ya kidunia wapi na wapi lakini bado ataonekana hana makosa. Haya bwana najua mko wengi na wengine hodari wa kujenga hoja sijui ni wanasheria? Anyway waswahili husema hakuna marefu yasiyo na ncha. Tuende tuone, alikataa Dk salim alipoulizwa kama anampango wa kugombea Urais.
 
Back
Top Bottom