Sakata la mchungaji kujiunganishia umeme;waumini wafunga kulaani waliomchongea

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,462
21,334
BAADA ya Mchungaji wa Kanisa la Uponyaji, Edward Kishimbo kukamatwa na polisi kwa kukutwa akijiunganishia na kutumia umeme wa Shirika la Umeme (Tanesco) katika kanisa lake isivyo halali, waumini wake juzi walitangaza kufunga kula na kunywa ili wale waliohusika kutoa taarifa kwa shirika hilo wadhurike.

Katika maombi hayo, Mchungaji Kishimbo na waumini wake walitumia ibada ya juzi kufanya maombi maalumu ya kulaani kitendo hicho na kuunda jopo la waumini watakaoongoza maombi hayo kwa siku saba kwa kutokula wala kunywa huku wakidai kitendo cha Tanesco kukata umeme kwao ni batili kwani uliunganishwa kihalali.

Katika ibada hiyo, waliitaka Tanesco irudishe umeme huo ndani ya siku tatu huku waandishi wa habari wakitakiwa kukanusha taarifa walizozitoa za kukamatwa kwa Mchungaji wao ndani ya siku tatu kabla maombi yao hayajajibiwa kwa kupata madhara kwa waandishi na wafanyakazi wa Tanesco.

Katika kanisa hilo lililopo Chama Tengeru, mamia ya waumini hao walikuwa wakitaja majina ya baadhi ya waandishi wa habari walioandika taarifa hiyo na kudai kuwa wasimalize siku saba kabla ya kujutia kitendo hicho.

“Baba sasa tunakwenda kuweka maombi haya mbele yako tunaomba hawa waandishi wasimalize siku saba… waandishi hawa wawe kaburini na kujutia walichokiandika,” aliomba Mchungaji Kishimbo.

Pia waumini hao walidai kuwa maombi hayo yanamuhusu meneja wa shirika hilo wilayani Arumeru na kwamba adhurike kwa nguvu za Mungu ndani ya siku hizo saba aungane na waandishi hao katika kujutia kitendo hicho.

Alidai hakuunganisha umeme huo kibatili kwa kuwa baadhi ya wafanyakazi wa Tanesco walifika kanisani hapo Januari 13, 2010 na kuunganisha umeme huo kwa gharama ya Sh 2,270,000. Alidai shirika hilo halimkutendea haki na limemdhalilisha yeye na waumini wake na kulitaka kuomba radhi kabla mambo hayajawa makubwa.

Akizungumza na gazeti hili, Meneja wa Tanesco Wilaya ya Arumeru, Kibiki Mohamed alisema Mchungaji huyo alishawahi kupeleka maombi ya kuunganishiwa umeme, lakini hakumuona tena na kukiri kuwepo kwa baadhi ya watu wanaojifanya ni waajiriwa wa shirika hilo, anaoamini huenda ndiyo waliofanya hivyo; kwani hakuna kumbukumbu zozote zinazoonesha kuwa Tanesco imewaunganishia umeme kanisa hilo.
 
Sasa wanacholaani ni nini hawa jamaa? au ndo maadili ya hilo dhehebu lao?
 
Wait and see! Kibwetere is here, tutakuja kia na kuaga meno wana wa tz kwa umbumbavu na ujinga wetu.
They r selling hope and we buy it. God gives hope, he neber sells it
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom