Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,682
- 149,886
Kwakuwa moja ya kazi ya Bunge ni kuishauri na kuisimamia serikali, nawashauri wabunge wote bila kujali vyama vyao wajadili jambo hili kama hoja ya dharura na waafikie maamuzi ya kuishauri serikali ikubali wazo wa kuunda Tume Huru ya uchunguzi kama ACACIA walivyopendekeza.
Iwapo kiti kitazuia hoja hiyo kujadiliwa, basi nawashauri katika mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kila mbunge atakayesimama aitake serikali ikubali swala la kuunda Tume Huru ili kumaliza huu mgogoro na hapo mtakuwa mmetimuza wajibu wenu kama wabunge.
Na ninashauri Tume hiyo itakayoundwa kwa kushirikiana na hao ACACIA, wajumbe wa iliyokuwa kamati ya Prof.Mruma washirikishwe na ikiwezekana Prof.Mruma mwenyewe ndio aingie kwenye hiyo Tume ili baadae nao wasije sema hawakubaliana na findings za hiyo Tume itakayoundwa..
Tena ikiwezekana kila hatua muhimu ya uchunguzi inapokamilika, kuwe na utaratibu wa kusaini makubaliano ya kukubali matokeo ya hatua muhimu ya uchunguzi iliokamilika kabla ya kuendelea na hatua nyingine ili baadae pasiwepo na visingizio vya kutokuikubali ripoti kamili itakapotolewa.
Na ili kufanikisha hili, nashauri wanasheria kutoka pande mbili hizi zenye mgogoro wawe wajumbe wa hii Tume na pia Tume hii isimamiwe na chombo huru kitakachokubalika na pande zote mbili au kama itakavyoamuliwa na mahakama (msuluhishi) iwapo tutamshirikisha na ni vizuri ashirikishwe
Binafsi naona swala kuunda Tume Huru lina adavantage sana kwetu kwasababu mpaka hapa huenda tayari tumeshafanya kosa la kuchukua maamuzi ya upande mmoja tu bila kuwashirikisha hawa jamaa na sidhani kama mkataba tuliosaini sisi na wao unaruhusu upande mmoja ku-act unilateraly pindi mgogoro unapotokea baina ya pande mbili na hii itatuepusha na adhabu za kuwalipa hawa jamaa fidia hata kama wametuibia.
Na vile vile kama kamati itakuwa imefanya kazi yake kwa usahihi na umakini,ni wazi hii itakuwa ni fursa ya kuwaumbua hawa watu na kumaliza huu mgogoro.
Hili jambo ni rahisi sana kulimaliza iwapo busara itatumika lakini tukitumia ubabe sisi ndio tutalipa gharama kubwa pamoja na kuwa wametunyonya vya kutosha na kwa muda mrefu.
Tulipaswa kuwa wababe wakati wa kusaini mikata na si baada ya kusaini mikataba.
CCM na Serikali msipotuelewa sasa, muda utawalazimisha kuelewa hapo baadae.