Sakata la Mchanga wa Madini: Utetezi wa ACACIA huu hapa

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,193
2,000
duu ngoja mie nikaangalie shilawadu haya ya Acacia siyawezi pasua kichwa, nishafurahia noah sasa imeyeyuka??
 

Magonjwa Mtambuka

JF-Expert Member
Aug 2, 2016
24,661
2,000
Nashukuru kwa kutafsiri hii taarifa kwa kiswahili. Tusiichangie kama ni habari mpya kwani kama inavyoonesha ni ya Tarehe 13/06/2017 na leo ni 21/06/2017 yaani siku nane zimepita tangu taarifa hiyo itolewe, na ilishakuwemo hapa katika Lugha ya Kiingereza.

Kwa mtazamo wangu Acacia wameamua kuitoa kwa Kiswahili ili kuwafikia watanzania wengi zaidi (Pamoja na wale wanaojua kusoma na kuandika tu) inawezakana baada ya kuona Watanzania wengi hawaelewi na hakieleweki ni nini kimeafikiwa mpaka sasa.

Kwa udadisi tu: Rais wa Acacia alipoona kwamba maslahi ya Kampuni yake yanatishiwa, alifanya hima kuja. Sisi tulioanzisha "Vita" hii mpaka sasa tumefanya nini. Kwa siku nane ni nini maendeleo ya ule mapango wetu wa Mazungumzo na "Acacia" na ni kwa nini hatupewi tena mrejesho wa nini kinaendelea kati yetu na "wezi" wa rasirimali zetu.

Acacia ni wanaume aisee!
Naona umeamua kuwa Lisurappa.
 

INGENJA

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
4,991
2,000
Bado ana dhana kuwa waTZ/watu weusi wana akili ya kucheza ngoma na kujamiiana tu!!!

Ni hivi, wametumia namba na wasomi kuficha ukweli, kulinganisha na makampuni mengine hakuwapi uhalali wa kuwa wao nj wakweli na kamati zetu ni waongo, kama mchezo ndio huo huo kwa kila kampuni???

Nani asiyemfahamu mzee Bakhresa kwa kushika dini na kutoa misaada, wangetumia kigezo hicho, bilioni nane zisingelipwa.

Muhimu ni Raisi na waTZ kwa ujumla, tusielewe wala kusikia la kwao, sisi ndo wenye kila kitu, hawataki, watuache.

Tukimalizana na hao, tuwageukie hawa wenzetu walioshikishwa chochote kitu, kama wezi wa mitaani tu, tuwatie tairi na moto wa petroli. Ni wezi tu kama wengine.

Hawa wageni sio wajinga, kama AIPITIELO imesababisha wamiliki wake kwa 50% kukamatwa na wamiliki waliobaki kulindwa, hatudhani kuwa na wao wanaona hiyo LOOPHOLE ndo maana wana cha kusema na mwisho kesi inaisha huku Raia namba moja akiaibika vibaya.

Nafikiri tu.
kwani mnaakali timamu sasa au makinikia yamejaa huko kichwani,kwani acacia alikuja kuchukua madini na mtutu au anachukua madini kimaandishi
 

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
10,982
2,000
JUZI; ACACIA hawa ni wezi, hawana leseni ya kuchimba madini nchini, hawana usajili, hatuwezi kuwalinda kwa askari wetu wezi wanaotuibia hawa.., hakuna mchanga kutoka nje.., ni wezi.

JANA; mimi kama mbunge wa eneo hilo, sasa natoa Rai kwa wananchi wangu, kuhakikisha tunazuia hawa wezi wa ACACIA wasituibie tena, tunakwenda kuzuia madini uetu yasisafirishwe.

LEO; HAPANA.., huyu mbunge ni mchochezi.., akamatwe na aunganishwe kwenye watu wenye vurugu, anahatarisha usalama wa nchi, anawasumbua wawekezaji.., akamatwe!!

#My_Take; Muombe Mungu kila siku.., usipewe ubongo na akili kama za ndugu zetu wa CCM.., ni laana, sasa ndugu zetu ndio wamebeba tafsiri sahihi ya neno "matumizi mabaya ya akili za binadamu", hawajui hata wanataka nini, kama bendera kavu tu, wanapepea!
 

kacheto2015

Senior Member
Oct 25, 2015
121
250
Tujiulize tu kwa maelezo Haya ya ACACIA neno la "on win win basis" inakuwaje kwa Tanzania. Hizi Noah si ndoto za mchana??
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom