Sakata la Mbowe kuwa na tuhuma za ugaidi isiwe sababu ya kutaka Watanzania tuamini anaonewa. Tuache mahakama iamue.

Pole ndugu,
duniani kuna wengi wenye uwezo wa kawaida wa kuelewa vizuri mambo yanayo wazunguka katika maisha yao, na penye hitaji, hawa huweza kusaidiwa wakabadilika na kuwa wazuri, wema na wenye utu na hamu ya maendeleo ya kweli kwao.
Lakini pia, kuna ambao wanazidi kupoteza uwezo wa hata kusoma mazingira na zaidi umuhimu wa mabadilikojami chanya kwao, wewe u mmoja wao. Nyie ndio zao kuu la awamu ya kipindi cha giza cha Nabii Walwa Njozi wa Burigi. Kwa kurithi takataka zote za ukatili na udhalimu mmekuwa ni hasara kubwa kwa TAIFA.
Kipindi cha kuyaong'oa haya magugumaji sasa kimeshafika. AMEN
Umemjibu vizuri sana tena kwa hekima kuu.

Cc Idugunde
 
Kila mwanaChadema anataka kuwaaminisha watanzania kuwa Mbowe amebambikizwa shitaka la ugaidi. Mbowe anaonewa maana sasa amewekwa kwenye sero ya wafungwa wa kunyongwa. Sawa, mnaweza kuwa sawa lakini suala lipo mahakamani.

Ibara ya 13 ya JMT ipo wazi kabisa kuwa hakuna mtu atakuwa na hatia mpaka mahakama imtie hatiani.

Sasa kama mahakama ndio chombo cha kumtia mtu hatiani mbona mnataka watanzania waingilie suala amabalo lipo mahakamani? Kama hana kosa basi acheni mahakama iamue,sio kutaka watanzania waingilie suala ambalo lipo ndani ya mahakama.

My take; Kulazimisha wananchi waamini kuwa Mbowe kaonewa is wastage of time.
Utambue kuwa kuna watu wengi magerezani wame fungwa kwa kubambikwa kesi. Mfano mh. Sugu alifungwa baadae makama ya rufaa ikamuona hakuwa n hatia (wakati huo alisha maliza kifungo) Mbowe naviongozi wa Chadema walipigwa faini ya ml 350 au kifungo mahakama ya rufaa iliwaona hawana hatia.
 
Bahati mbaya Tanzania hatuna mahakama inayoweza kuitwa mahakama kwa maana ya mahakama.

Marehemu aliua mahakama, akaigeuza kuwa taasisi yake kwa nia ya kuwatesa wasiomshangilia. Aliwateua wasiojulikana kuwa majaji, akawajaza mahakamani. Msajili wa mahakama ni afisa wa wasiojulikana. Ndiye anayeamua kesi gani ipelwkwe kwa jaji, na ipi apewe asiyejulikana ili kumkomoa mtuhumiwa, kama walivyofanya kwa Mbowe. Baada ya njama kugundulika, amejitoa mapema.
lakini muwe mnaweka na kumbukumbu kidogo mbona hakuna hakimu aliyejitoa mwenyewe kwenye hii kesi nani alijitoa mwenyewe?
 
Utambue kuwa kuna watu wengi magerezani wame fungwa kwa kubambikwa kesi. Mfano mh. Sugu alifungwa baadae makama ya rufaa ikamuona hakuwa n hatia (wakati huo alisha maliza kifungo) Mbowe naviongozi wa Chadema walipigwa faini ya ml 350 au kifungo mahakama ya rufaa iliwaona hawana hatia.
kwahiyo hata hii kesi akifungwa watakata rufaa akionekana hana hatia ataachiwa hata mwaka 2030 atakuwa huru maisha yanaenda byeeeeeee
 
kwahiyo hata hii kesi akifungwa watakata rufaa akionekana hana hatia ataachiwa hata mwaka 2030 atakuwa huru maisha yanaenda byeeeeeee
Wewe Gwanda linakutesa livue usingoje kuvuliwa
Amini amini nakuambia Watanganyika watawageuka kijani msiamini
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom