Sakata la maziwa ya china linatufundisha nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la maziwa ya china linatufundisha nini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Sep 21, 2008.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Katika siku hizi za karibuni kabisa kumekuwa na sakata la maziwa kutoka China.Sijashanga sana, kwa vile Wachina ni jamii ya watu ambao kwao si ajabu kukuuzia karatasi huku wakisema ni noti.Ndio maana mimi sio mpenzi kabisa wa bidhaa za China.Tatizo la msingi hasa katika sakata hilo ni nini.Ni kwamba, katika mazima ya aina ya Sanlu yanayotengenezwa huko China, imegundulika kwamba kuna kemikali iitwayo 'melanime'.Kemikali hii ina matumizi mengi.Chache katika hizo ni kwamba, huweza kutumika katika kutengenezea vyombo na viezekeo.La ajabu ni kwamba kemikali hii imeongezwa katika maziwa ya watoto.Kwa nini hasa imewekwa?Inasemekana kwamba wakulima wanaozalisha maziwa hayo huko China, ndio walio ongeza kemikali hii,ili maziwa waliyoweka maji yaonekane yana protini zaidi.Vituko hivyo.Kemikali hiyo inaweza ikaletelea 'kidney stones' na hatimaye figo kushindwa kufanya kazi na kusababisha vifo.Mpaka sasa watoto wanne wamekufa,na wengine 1,253 ni wagonjwa.Lakini sisi Tanzania tunajifunza nini katika sakata hili?Tunayo TBS na TFDA,sina hakika ni chombo kipi kinahusika hasa katika suala kama hili, maana majukumu yao hayajawekwa wazi sana,lakini kwa vile haya ni mambo ya vyakula, basi nadhani TFDA ndiyo inayo husika.Ni vema vyombo hivi hata hivyo vikawa 'alert' muda wote kuzuia uingizwaji wa bidhaa zisizo faa.Si vema tatizo limeshatokea, halafu hawana uhakika kama bidhaa hiyo imeshaingia nchini au laa,kama TFDA ilivyo-onekana kufanya.Nilitegemea TFDA inyanyuke kifua mbele na kuwaambia wananchi kwamba wasiwe na wasiwasi, maziwa hayo hayako nchini.Katika hali ya namna hii, sisi walaji tunakuwa na wasiwasi sana,kwa vile inavyo onekana ni kwamba, bidhaa inaweza kuingia nchini bila vyombo hivyo kuwa na habari,na mpaka wanapopata habari wananchi wanakuwa wamesha athirika sana.Ninaiomba serikali isimamie inavyopaswa utendaji wa TBS na TFDA,ili kuepuka athari mbaya zinazoweza kuwapata wananchi wetu kutokana na matumizi ya bidhaa zisizofaa.Leo watoto waliokufa ni wa Kichina,lakini tusipokuwa waangalifu,watoto watakao kufa kesho watakuwa ni wa watanzania wenzetu. Mungu ibariki Tanzania.
   
 2. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2008
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Chakufanya hapa ni kupiga marufuku chochote kiingiacho kinywani au kutumika kwenye mwili wa binadamu kutoka china,kama wanafanya hivi kwa watoto wao kwetu tutegemee nini?
   
Loading...