Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,172
Ni rahisi kumnyooshea waziri kidole pale wananchi wanapolalamika lakini mchango wa waziri katika matatizo unapimwaje?
Tunapima watendaji kwa kauli za wananchi au baada ya kutathmini mfumo unafanyaje kazi?
Hivi kama pembejeo hazijawafikia wakulima walengwa tatizo ni waziri mhusika au kuna matatizo yaliyopo nje ya uwezo wake?
a) Kama Hazina haijatoa pesa kwa wakati mwafaka yeye awajibike kwanini?
b) Kama Waziri wa fedha anatoa misamaha ya kodi na kuidhoofisha serikali hivi waziri mhusika anawajibishwa kwa makosa ya nani?
c) Kama watendaji ndani ya vyama vya ushirika wametafuna fedha hivi waziri mhusika afanyaje?
d) Kama ni sera ya serikali kuzuia mazao ya chakula ya wakulima yasiuzwe nchi za jirani hivi kweli waziri mhusika atawajibishwaje kwa mapungufu ya kisera ambayo yametafuna soko la wakulima husika?
e) Hivi kama Benki ya wakulima inaendeshwa visivyo kwani waziri mhusika ndiye aliyewateua?
f) Hivi kama fedha za bajeti na kasma halisi aliyopewa haitoshi kuyatatua matatizo yaliyopo waziri mhusika awajibishwe kwa kukosea wapi?
g) Hivi kama walioshiriki katika ziara ya Kinana mikoani nao wanaunyemelea uwaziri huohuo hivi haki ya watuhumiwa imekaa vipi?
Mawaziri bomu tunawajua lakini kamwe hatuwapigii ukelele. Wako ambao hupewa bajeti kubwa lakini utendaji wao ni wa kusuasua na hulitia taifa hasara ya kutisha kwa kutanguliza ukelele na kutishia wananchi badala ya kuchapa kazi……niwataje na mapungufu yao au mtawataja?