SAKATA LA MAWAZIRI MZIGO: KWANINI Kinana anapaswa kupuuziliwa mbali?

Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,611
Likes
705,305
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,611 705,305 280
Ni rahisi kumnyooshea waziri kidole pale wananchi wanapolalamika lakini mchango wa waziri katika matatizo unapimwaje?

Tunapima watendaji kwa kauli za wananchi au baada ya kutathmini mfumo unafanyaje kazi?

Hivi kama pembejeo hazijawafikia wakulima walengwa tatizo ni waziri mhusika au kuna matatizo yaliyopo nje ya uwezo wake?

a) Kama Hazina haijatoa pesa kwa wakati mwafaka yeye awajibike kwanini?

b) Kama Waziri wa fedha anatoa misamaha ya kodi na kuidhoofisha serikali hivi waziri mhusika anawajibishwa kwa makosa ya nani?

c) Kama watendaji ndani ya vyama vya ushirika wametafuna fedha hivi waziri mhusika afanyaje?

d) Kama ni sera ya serikali kuzuia mazao ya chakula ya wakulima yasiuzwe nchi za jirani hivi kweli waziri mhusika atawajibishwaje kwa mapungufu ya kisera ambayo yametafuna soko la wakulima husika?

e) Hivi kama Benki ya wakulima inaendeshwa visivyo kwani waziri mhusika ndiye aliyewateua?

f) Hivi kama fedha za bajeti na kasma halisi aliyopewa haitoshi kuyatatua matatizo yaliyopo waziri mhusika awajibishwe kwa kukosea wapi?

g) Hivi kama walioshiriki katika ziara ya Kinana mikoani nao wanaunyemelea uwaziri huohuo hivi haki ya watuhumiwa imekaa vipi?

Mawaziri bomu tunawajua lakini kamwe hatuwapigii ukelele. Wako ambao hupewa bajeti kubwa lakini utendaji wao ni wa kusuasua na hulitia taifa hasara ya kutisha kwa kutanguliza ukelele na kutishia wananchi badala ya kuchapa kazi……niwataje na mapungufu yao au mtawataja?

Mwalimu

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
1,492
Likes
285
Points
180
Mwalimu

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
1,492 285 180
Kazi za Waziri ni zipi?

Nafikiri hapa ndio kuna shida kubwa....
 
Kichuguu

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Messages
7,438
Likes
1,326
Points
280
Kichuguu

Kichuguu

Platinum Member
Joined Oct 11, 2006
7,438 1,326 280
Kinana na timu yake wanataka kuwaaminisha wananchi kuwa serikali ya CCM inafanya mambo yote sawasawa isipokuwa kuna mawaziri wachache tu ambao ndiyo "mizigo." Kwa bahati mbaya watanzania tunaweza kuamini hivyo kutokana na ujinga wetu, lakini ukweli ni kuwa (a) Waziri mmoja hana nguvu ya kuleta mabadiliko ya maana unless amevuka mipaka ya wajibu na madaraka yake, yaani akaingilia mambo yaliyoko nje ya madaraka yake. (b) Utendaji wa wizara za serikali uko intertwinned kiasi kuwa huwezi kutenganisha wizara moja ukaicha nyingine; kwa mfano kusafisha rushwa airport kutokomeza usafirishaji wa madawa ya kulevya siyo kazi ya waziri wa uchukuzi bali ni kazi ya wizara ya mambo ya ndani, pamoja na ofisi ya rais na ofisi ya waziri mkuu kwa pamoja kabla wizara ya uchukuzi haijachukua nafasi ya kuwafukuza kazi wahusika.

Mwisho wa yote ni kuwa kinana anajaribu kuisha CCM kama mchora katuni alivyoainisha
 
J

jnuswe

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Messages
1,270
Likes
6
Points
135
J

jnuswe

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2010
1,270 6 135
Kamati kuu ya CCM imefanya jambo zuri kwa kutambua kuwa serikali ya chama chao kina mawaziri mizigo lakini wanapaswa waliangalie tena upya baraza la Mawaziri linaloongwazawa na serikali ya CCM , kwa yale watanzania tunayoyashuhudia yakiutendaji katika serikali hii ya awamu ya nne karibu mawaziri wote ni mizigo

Hivi kweli inaingia akilini kutomuingiza Philipo Mulugo kwenye orodha ya Mawaziri Mizingo ?

Nawasilisha
 
D

duchi

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Messages
1,766
Likes
3
Points
0
D

duchi

JF-Expert Member
Joined Oct 22, 2012
1,766 3 0
Ndo maana Kinana alisema waitwe kwenye kamati kuu ili wajieleze. Hakusema wafukuzwe kazi.
 
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,611
Likes
705,305
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,611 705,305 280
Kamati kuu ya CCM imefanya jambo zuri kwa kutambua kuwa serikali ya chama chao kina mawaziri mizigo lakini wanapaswa waliangalie tena upya baraza la Mawaziri linaloongwazawa na serikali ya CCM , kwa yale watanzania tunayoyashuhudia yakiutendaji katika serikali hii ya awamu ya nne karibu mawaziri wote ni mizigo

Hivi kweli inaingia akilini kutomuingiza Philipo Mulugo kwenye orodha ya Mawaziri Mizingo ?

Nawasilisha
Tatizo la kujiuliza tangia tumebadilisha mawaziri tija iko wapi? Jibu ni kuwa hakuna.
 
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,611
Likes
705,305
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,611 705,305 280
Ndo maana Kinana alisema waitwe kwenye kamati kuu ili wajieleze. Hakusema wafukuzwe kazi.
wajieleze nini tayari kawaita mzigo? Huku na baraza jipya wamelisuka?
 
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,611
Likes
705,305
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,611 705,305 280
Mlishawahi sikia watu wakisema..."CHANGA LA MACHO"?.......basi hiyo ndio mbinu ya akina Kinana.......
Hata mimi naona hivyo.
 
bona

bona

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2009
Messages
3,794
Likes
183
Points
160
bona

bona

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2009
3,794 183 160
Ni rahisi kumnyooshea waziri kidole pale wananchi wanapolalamika lakini mchango wa waziri katika matatizo unapimwaje?

unapimwa kwa kuleta unafuu kwa wananchi ktk mambo ambayo wizara yake anaiongeza pamoja na kuongeza pato la taifa!!!
Tunapima watendaji kwa kauli za wananchi au baada ya kutathmini mfumo unafanyaje kazi?

nshakujibu apo juu

Hivi kama pembejeo hazijawafikia wakulima walengwa tatizo ni waziri mhusika au kuna matatizo yaliyopo nje ya uwezo wake?

kama pembejeo hazijawafikia wakulima yeye alichukua hatua gani? kukaa tu ofcn ndo zingefika? wizara yake ina kitengo cha kufuatilia kwamba wakulima wanapata pembejeo kwa wakati so no excuse

a) Kama Hazina haijatoa pesa kwa wakati mwafaka yeye awajibike kwanini?

kuna tatizo ktk wizara yake mbona wizara zingine zinapata pesa kama miundombinu nk ingefikia hatua achukue collective responsibility ya kumwandikia barua rais ya kujiuzulu kwa sababu amekwamishwa kukaa tu ofcn kusubiri mshahara wake haitoshi

b) Kama Waziri wa fedha anatoa misamaha ya kodi na kuidhoofisha serikali hivi waziri mhusika anawajibishwa kwa makosa ya nani?

serikali kwa taarifa yako inatoa subsidies kwenye wiara ya kilimo kusupport mazao mbali mbali kwa mfano pamba serikali nna uhakika inatoa ruzuku, pili suala la misamaha ya kodi umelihusishaje na hili na mwisho wizara yake ndio inapeleka muswada wa sheria bungen kuhusu mambo ya kilimo kwa nn hawakuyaona mapungufu haya

c) Kama watendaji ndani ya vyama vya ushirika wametafuna fedha hivi waziri mhusika afanyaje?

alichukua hatua gani?? alipeleka vielelezo vya wizi uo kwa vyombo vya dola ili watu wachukuliwe hatua au alikaa kimya tu?

d) Kama ni sera ya serikali kuzuia mazao ya chakula ya wakulima yasiuzwe nchi za jirani hivi kweli waziri mhusika atawajibishwaje kwa mapungufu ya kisera ambayo yametafuna soko la wakulima husika?

sera kuhusu mambo ya kilimo inatungwa na nani kama c wizara husika? na nani ni mkuu wa hiyo wizara zaidi ya waziri? dont shoot yourself on the foot!!!

e) Hivi kama Benki ya wakulima inaendeshwa visivyo kwani waziri mhusika ndiye aliyewateua?
f) Hivi kama fedha za bajeti na kasma halisi aliyopewa haitoshi kuyatatua matatizo yaliyopo waziri mhusika awajibishwe kwa kukosea wapi?

g) Hivi kama walioshiriki katika ziara ya Kinana mikoani nao wanaunyemelea uwaziri huohuo hivi haki ya watuhumiwa imekaa vipi?

usiliete propaganda lete hoja zinazoendana kuzungumzia kuna watu wanautaka uwaziri ni hoja dhaifu, uanzishwaj wa benki ya wakulima wizara nk ni muendelezo wa sera za wizara so isipofanya kazi wizara haiwez kujitoa kwamba hawahusiki

Mawaziri bomu tunawajua lakini kamwe hatuwapigii ukelele. Wako ambao hupewa bajeti kubwa lakini utendaji wao ni wa kusuasua na hulitia taifa hasara ya kutisha kwa kutanguliza ukelele na kutishia wananchi badala ya kuchapa kazi……
niwataje na mapungufu yao au mtawataja?

uko free kuanzisha mada ya mawaziri unaowaona bomu na data zao ila usilete hapa kama njia ya kuficha huyu aliyetajwa, kila mada itashuhulikiwa kivyake si kwa kuleta kitu kipya kuficha madudu yaliyopo!!
 
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,611
Likes
705,305
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,611 705,305 280
Wakajieleze kuwa siyo mizigo.
kwa kuwaita mizigo tayari kesha wahu7kumu kuwa ni mizigo sasa kuwahoji na kujieleza ni changa la macho tu. Kama waliwahukumu hata kabla ya kuwapa nafasi ya kujiele haki zao za asili zilikiukwa na kamwe hawawezi kutendewa haki.
 
bona

bona

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2009
Messages
3,794
Likes
183
Points
160
bona

bona

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2009
3,794 183 160
Kamati kuu ya CCM imefanya jambo zuri kwa kutambua kuwa serikali ya chama chao kina mawaziri mizigo lakini wanapaswa waliangalie tena upya baraza la Mawaziri linaloongwazawa na serikali ya CCM , kwa yale watanzania tunayoyashuhudia yakiutendaji katika serikali hii ya awamu ya nne karibu mawaziri wote ni mizigo

Hivi kweli inaingia akilini kutomuingiza Philipo Mulugo kwenye orodha ya Mawaziri Mizingo ?

Nawasilisha
mulugo ni naibu waziri ila waziri wake kawambwa ndio katajwa!!
 
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,611
Likes
705,305
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,611 705,305 280
uko free kuanzisha mada ya mawaziri unaowaona bomu na data zao ila usilete hapa kama njia ya kuficha huyu aliyetajwa, kila mada itashuhulikiwa kivyake si kwa kuleta kitu kipya kuficha madudu yaliyopo!!
Hujajibu khoja. Nionacho unatiririkwa na mapovu...................
 
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,611
Likes
705,305
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,611 705,305 280
sera kuhusu mambo ya kilimo inatungwa na nani kama c wizara husika? na nani ni mkuu wa hiyo wizara zaidi ya waziri? dont shoot yourself on the foot!!!
sera mbovu ni maamuzi ya baraza la mawaziri walioipitisha siyo waziri mmoja au wizara yake na ndiyo maana mkapa alienda kutoa ushahidi mahakaman kutetea maamuzi ya baraza la mawaziri. Chunga unachoandika!
 
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,611
Likes
705,305
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,611 705,305 280
alichukua hatua gani?? alipeleka vielelezo vya wizi uo kwa vyombo vya dola ili watu wachukuliwe hatua au alikaa kimya tu?
wa kumpa taarifa si ni CAG, DPP na Takukuru. Kama hawajekeleza majukumu yao yeye afanye nini?
 
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,611
Likes
705,305
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,611 705,305 280
serikali kwa taarifa yako inatoa subsidies kwenye wiara ya kilimo kusupport mazao mbali mbali kwa mfano pamba serikali nna uhakika inatoa ruzuku, pili suala la misamaha ya kodi umelihusishaje na hili na mwisho wizara yake ndio inapeleka muswada wa sheria bungen kuhusu mambo ya kilimo kwa nn hawakuyaona mapungufu haya
sehemu kubwa ya bajeti haitekelezwi kisa ni kuwa fedha zimepangiwa safari a masurufu ya wakubwa ikiwemo tiba nje ya nchi zisizo za lazima. yeye anahusika vipi kama Hazina haimpi hela kwa kuruhusu misamaha ya kodi isiyowajibika bungeni?
 
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,611
Likes
705,305
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,611 705,305 280
kuna tatizo ktk wizara yake mbona wizara zingine zinapata pesa kama miundombinu nk ingefikia hatua achukue collective responsibility ya kumwandikia barua rais ya kujiuzulu kwa sababu amekwamishwa kukaa tu ofcn kusubiri mshahara wake haitoshi
katika wizara zinazoongoza kuvuja pesa ni Miundo mbinu na nashangaa Magufuli halalamikiwi. Kila kukicha wanabomoa madaraja ambayo waliyajenga wenyewe swali linakuja hawakujua vipimo sahihi au ni mbinu ya kutafuna pesa tu? Kila kukicha kilometa ya lami kuitengeneza bei inapanda lakini hakuna anayewajibika na matokeo yake barabara chache sana zinatengenezwa wa kumlaumu ni nani kama si Magufuli ambaye ni bingwa kwa ukelele lakini tija hakuna. Tukilalamikia hakuna barabara za maana tunaambiwa tuone vichochoro vinavyojengwa kuwa nazo ni barabra wakati ni vichochoro hatarishi na ajali zimetosonga kutokana na msongamano barabarani.....................uko dunia ipi walakini?
 
Forum statistics

Threads 1,250,679
Members 481,436
Posts 29,741,508