Sakata la Mawaziri Mizigo na Uwajibikaji; Nape kutua ITV kesho asubuhi

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,645
2,000
Katibu wa halmashauri kuu ya Taifa idara ya Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kesho ataunguruma katika kituo cha televizion cha ITV katika kipindi cha asubuhi saa moja.

Katibu huyo wa Uenezi wa CCM anatarajia kuelezea juu ya kikao na maamuzi ama maazimio ya kikao cha kamati kuu ya taifa kuhusu mawaziri wa serikali ambao wameshindwa kutekeleza majukumu yao ndani ya wizara husika na kwamba kamati kuu imefikia maamuzi hayo baada ya kuwasilikiza mawaziri hao walioalikwa kwenye kikao hicho ili kujieleza.

Pamoja na kuelezea maamuzi ya kamati kuu kwa kina pia anatarajia kuzungumza sakata la uwajibikaji wa mawaziri na kujiuzulu pamoja na kuvuliwa nafasi hizo kwa baadhi ya mawaziri, ambao kutokana na makosa na utendaji ulio na mapungufu Rais wa Jamhuri ameamua kuwavua nafasi zao hizo.

wote mnakaribishwa.
 
mapinduzi daima

JF-Expert Member
Sep 30, 2013
1,582
2,000
Are you nape?
Hivi CC ni appointing authority ya mawaziri?

Waungwana...natamani hii nchi ipate RAIS mpya 2015 ambaye anajua EXACTLY WHY TUMEKWAMA HAPA NA ana weza kufuta mfumo huu MBOVU wa kiutawala hata ikibidi kukosana na NDUGU ZAKE na CHAMA CHAKE kwa ajili ya watanzania.
 
Froida

JF-Expert Member
May 25, 2009
8,758
2,000
Acha ujinga Nape munajivua nguo mawaziri wawe mizigo ila Raisi awe bora na chama kiwe salama propaganda za kijinga hizo sasa hivi tumeshajua mbinu zenu tutaanza kuwakaushia mapema na kuanika ujinga wenu mtu anaongoza serikali miaka kumi na kubadili baraza la mawaziri mara nne ni upuuzi kumuacha aendelee kuwa Raisi fanyeni yale yaliyofanywa na ANC kumuondoa mwenyekiti wenu na kuweka mwingine na uchaguzi kuittishwa
 
Honolulu

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
5,648
1,225
Hii yote ni homa kuelekea uchaguzi mkuu 2015. CCM wanataka kuhadaa wananchi kwamba na wao maamuzi magumu wanayaweza. Kama kweli wanayaweza maamuzi magumu hebu washughulikie ile orodha ya mafisadi papa waliyokabidhiwa na Dr Slaa tuone.
 
DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
8,619
2,000
Unataka kuhubirh mizigo inayokimbia while ni tofauti ya wale 7,watanzania wamewashtukia kuwa mnawahadaa.
 
peace2007

JF-Expert Member
Oct 9, 2007
213
195
Kwa staili hii ya Uongozi wa CC na mfumo uliopo hata wakiniteua mimi kuwa Waziri NITAJIUZULU HAPOHAPO KWA KWELI!
 
Roga Roga

JF-Expert Member
Dec 20, 2013
645
500
Katibu wa halmashauri kuu ya Taifa idara ya Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kesho ataunguruma katika kituo cha televizion cha ITV katika kipindi cha asubuhi saa moja.

Katibu huyo wa Uenezi wa CCM anatarajia kuelezea juu ya kikao na maamuzi ama maazimio ya kikao cha kamati kuu ya taifa kuhusu mawaziri wa serikali ambao wameshindwa kutekeleza majukumu yao ndani ya wizara husika na kwamba kamati kuu imefikia maamuzi hayo baada ya kuwasilikiza mawaziri hao walioalikwa kwenye kikao hicho ili kujieleza.

Pamoja na kuelezea maamuzi ya kamati kuu kwa kina pia anatarajia kuzungumza sakata la uwajibikaji wa mawaziri na kujiuzulu pamoja na kuvuliwa nafasi hizo kwa baadhi ya mawaziri, ambao kutokana na makosa na utendaji ulio na mapungufu Rais wa Jamhuri ameamua kuwavua nafasi zao hizo.

wote mnakaribishwa.

Sasa hapo ITV ndipo anakwenda kutoa maamuzi ya CC au lengo lake nikupiga domo kama kawaida yake
 
samaki2011

JF-Expert Member
Dec 17, 2013
1,775
0
siku zote hizo walikuwa wapi? It is too late jamani wananchi tusikubali hizi harufu za vinyesi tuchukue hatua za kuwatoa hawa makaburu. Washaona mambo yameanza kuwa magumu wanakumbuka shuka asubuhi kushakucha.

Kifo cha jani kikifika miti yote huteleza. kifo cha ccm kimlangoni
 
Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,065
2,000
Waungwana...natamani hii nchi ipate RAIS mpya 2015 ambaye anajua EXACTLY WHY TUMEKWAMA HAPA NA ana weza kufuta mfumo huu MBOVU wa kiutawala hata ikibidi kukosana na NDUGU ZAKE na CHAMA CHAKE kwa ajili ya watanzania.

Dr.W.Slaa ndio jibu lako
 
Last edited by a moderator:

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,181
2,000
Nape ajiandae ikifika 2015 naye atavyotupwa nje kwa kigezo naye ni mzigo!

Kabla hujahukumiwa na Mungu duniani hapa hapa ni lazima uonje joto ya jiwe. Mshikaji wako Nchimbi sijui atakuonaje kwa kumharibia kitumbua na yeye kuingia katika mzozo wa mawaziri mizigo.
 
juve2012

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
3,339
2,000
Mimi bado nakula sahani moja na wewe Nape.

Hivi Chiza na Malima una ugomvi nao gani? Si utueleze tu watz ukweli halisi kwamba Chiza na naibu wake Malima ni "mzigo" kwenu mafisadi baada ya kuwakatalieni dili zenu chafu pale kilimo?

Kuwa muwazi waeleze watu ukweli usifikiri watu ni wajinga,wengine ni insiders!Mmemaliza Kagasheki sasa mnahamia kwa Chiza na Malima. Mnaendelea kuharibu system nzima kwa maslahi ya vigogo wa chama chenu?

Mawaziri hawa mnawaonea, wanashindwa kufanya kazi zao kwa sababu ya mgongano wa maslahi kati ya uwaziri na ubunge(ambao ni ukada wa chama). Ndio maana mnatumia nguvu zenu zote kukwamisha katiba mpya ili mawaziri waendelee kunyenyekea bunge na chama, sivyo?

Tunasema hivi, hamtafanikiwa! Wananchi tumestuka. CCM ni kansa ya taifa. Hata wakiwemo watu wazuri humo mnawapiga vita ili kutetea "uchafu" wenu. Tumewastukia.

Endeleeni kuwatimua lakini kumbukeni mnatengeneza jeshi la watu nje ya chama ambalo litawatikiseni na kuwamaliza na sie wananchi tunawasubiri 2015.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom