Sakata la Mapesa yaliyofichwa Uswisi: Wamo vigogo wawili wastaafu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la Mapesa yaliyofichwa Uswisi: Wamo vigogo wawili wastaafu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by R.B, Jun 28, 2012.

 1. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 6,168
  Likes Received: 1,103
  Trophy Points: 280
  Toleo la 245 | 27 Jun 2012


  • Ni kati ya watoroshaji sita wakuu
  • Kikao cha Baraza ka Mawaziri kujadili
  • Membe asema mabilioni hayo yatarudi tu

  VIONGOZI wawili wastaafu waliopata kuitumikia nchi katika nafasi nyeti za dola ni miongoni mwa vigogo sita walioficha dola za Kimarekani takriban milioni 196.8 (Sh. Bilioni 315) katika mabenki ya Uswisi, RAIA MWEMA limeambiwa.

  Habari za uhakika ambazo gazeti hili limezipata zinasema kwamba vigogo hao walifanikiwa kukusanya mabilioni hayo kwa kuwashirikisha baadhi ya wafanyabiashara kupitia mfumo wa ununuzi serikalini (public procurement) kwa nyakati tofauti.

  Wakati hayo yakifahamika, Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, anatarajiwa kuwasilisha taarifa rasmi kuhusu uporaji huo kwenye Baraza la Mawaziri.

  Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari, baadhi ya wafanyabiashara walioficha pesa hizo kwenye mabenki ya Uswisi si wenye majina makubwa katika tasnia ya biashara hapa nchini, lakini ni wenye ufahamu wa kutosha katika mifumo ya kibiashara katika nchi mbalimbali duniani.

  "Taarifa za awali zinawahusisha viongozi sita. Serikali ya Uswisi iko tayari kutaja majina ya wahusika na pia wako tayari kutupatia mchanganuo wa kiasi cha fedha na taarifa nyingine muhimu. Rais ataitisha kikao cha Baraza la Mawaziri kujadili suala hili wakati wowote. Kwa sasa kinachoendelea ni ukusanyaji wa taarifa muhimu", kilieleza chanzo chetu cha habari serikalini.

  Mwandishi wetu alizungumza na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Dk. Edward Hosea, ambaye pia amekwisha kupata kuzungumzia suala hilo na vyombo mbalimbali vya habari nchini.

  Katika maelezo yake kwa mwandishi wetu, Dk. Hosea alisema: "Tumekwisha kuwaandikia Uswisi na tunatarajia taarifa kamili kutoka kwao. Tumewaandikia kuhusu maeneo ambayo tungependa kupata taarifa kuhusu suala hili, tunasubiri majibu yao. Tunaamini tutapata ushirikiano mzuri kwa sababu kwa sasa Uswisi imefanya mabadiliko ya sheria zake; tutafanikiwa."

  Lakini kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alipoulizwa kuhusu nafasi yake kama waziri katika kusaka taarifa za kadhia hii alijibu: "Ukizungumzia nafasi za mawaziri kuhusu suala hili...ni sahihi kusema kwamba kwa sasa lipo mikononi mwa Waziri wa Fedha. Sisi Wizara ya Mambo ya Nje tunazingatia taarifa zake (Waziri wa Fedha) ili kujua kwa namna gani tunashiriki."

  Membe aliongeza kusema: "Jambo moja la uhakika ni kwamba Serikali ipo tayari na imara kushughulikia suala hili. Kama kuna fedha zitarudishwa tu nchini. Jambo la msingi hapa ni kwamba sheria zote husika zitazingatiwa.

  Kama Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa itaingilia suala hilo, itakuwa ni mara ya pili katika utawala wa Rais Jakaya Kikwete kufanya hivyo. Tayari Waziri Membe alikuwa akiratibu namna ya urejeshaji wa fedha zilizozidi wakati wa ununuzi wa kitapeli wa rada ya kijeshi kutoka kampuni ya zana za kijeshi ya BAE-Systems ya Uingereza.

  Fedha hizo paundi za Uingereza milioni 29.5 (sawa na Sh bilioni 72.3 za Tanzania) zimekwisha kurejeshwa nchini na tayari zimepangiwa matumizi. Katika matumizi hayo, Sh. bilioni 54.2, sawa na asilimia 75) zimepangwa kutumika kununua vitabu vya kiada kwa shule za msingi na Sh. bilioni 18.1 zitatumika kutengeneza madawati kwa ajili ya shule za msingi.

  Pia katika sakata hilo la rada ilibainika kuwa aliyepata kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Andrew Chenge, alihifadhi takriban Sh. bilioni moja katika visiwa vya Jersey nchini Uingereza katika moja ya benki katika kisiwa hicho.

  Suala hili pia lilijitokeza jana, Jumanne, bungeni. Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto alimwomba Waziri Mkuu kuagiza mamlaka husika za kiserikali kufuatilia suala hilo na kutoa taarifa kwa umma.

  Zitto alisema hizo ni taarifa za kushtusha na kwamba hali hiyo inatia shaka zaidi kwa sababu inajitokeza katika wakati ambao nchi inakwenda kuvuna kiwango kikubwa cha gesi itakayoingiza fedha nyingi za kigeni na akasisitiza mianya ya utoroshaji fedha izibwe.

  Taarifa za kuporwa, kutoroshwa na kuhifadhiwa kwa takriban Sh bilioni 315 (dola za Marekani milioni 196.87) zimeanza kuandikwa na vyombo vya habari nchini kwa takriban wiki moja sasa.

  Taarifa kuhusu mabilioni hayo ziliwekwa hadharani kwenye ripoti ya Benki Kuu ya Uswisi, zikieleza kuwa si tu Tanzania, bali zipo nchi nyingine 10 ambazo watu mashuhuri katika nchi hizo wamehifadhi mabilioni ya fedha.

  Kwa mujibu wa taarifa hizo za Benki Kuu ya Uswisi, katika nchi za Afrika Mashariki Kenya ndio inayoongoza. Takwimu zinaonyesha kuwa kutoka Kenya, benki za Uswisi zimehifadhi dola milioni 857.

  Takwimu hizo za Uswisi zinaonyesha kuwa kutoka Uganda zimefichwa dola milioni 154, Misri dola milioni 798, Afrika Kusini dola milioni 795 na Rwanda dola milioni 29, Somalia dola milioni moja na Sudan dola milioni 179.

  Hivi karibuni Serikali ya Uswisi ilizielekeza benki zake mbalimbali nchini humo kufichua majina ya vigogo wa nchi mbalimbali walioweka kwa siri mabilioni ya fedha katika benki hizo.


  Chanzo: Raia Mwema
   
 2. Mfichua siri

  Mfichua siri Senior Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 19, 2012
  Messages: 135
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi namfikiria zaidi ndugu Edward Lowassa, waziri mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
   
 3. F

  Froida JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Hamtatutoa kwenye mada udhaifu wa serikali yenu na uuaji wao umefanya hospitali ya muhimbili kufungwa kwa asilimia 100 leo see for yourself
   
 4. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Wameficha au wameziweka?
   
 5. L

  Leodgard Member

  #5
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nalifikiria sana hili zee la vijisent change
   
 6. h

  handboy Senior Member

  #6
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 17, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yawezekana na wewe ni gamba unataka tuache kujadili uovu wa magamba unaolididiza taifa letu hilo litashugulikiwa
   
 7. D

  Don Draper Senior Member

  #7
  Jun 28, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kama mtu kafanya biashara au kazi na ana uwezo na kalipa kodi kihalali, kwa nini asifungue akaunti akutakako?
   
 8. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  billioni 315 ???, mbona hiyo ni pesa mbuzi tu mkuu.
   
 9. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,562
  Likes Received: 622
  Trophy Points: 280
  Kama ni mtihani wewe ume feli, huyo sio waziri mkuu mstaafu, wala si kiongozi mstaafu. Ni waziri mkuu aliyejiuzuru kwa Kashfa ya Richmond.
   
 10. Mfichua siri

  Mfichua siri Senior Member

  #10
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 19, 2012
  Messages: 135
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Basi hazina wenyewe
   
 11. The Fixer

  The Fixer JF-Expert Member

  #11
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 1,361
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Yaani unamfikiria mtu kama Lowassa maana unadhani yeye ndiye mwenye pesa peke yake hapa nchini ? Kwa taarifa yako Mh William Ngeleja yumo
   
 12. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Hapa lzamia BMW(Ben William Mkapa) atakuwa ndani ya listi.

  Mwingine ni kati ya hawa 3 : Basil Pesambili Mramba, Daniel Yonna au Tluwaye Sumaye.

  Tusubiri!
   
 13. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #13
  Jul 3, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Watajwe longolongo za kufichana zimepitwa na wakati
   
 14. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #14
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,960
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  yule muuaji wa baba wa taifa lazima atakuwepo. Anaitwa Mkwapa!
   
 15. K

  Kidogo chetu JF-Expert Member

  #15
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,386
  Likes Received: 774
  Trophy Points: 280
  leteni majina mengine haya ni majungu kama hayajatoka uswisi kaaeni kimya
   
 16. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #16
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Tatizo sio kurudishwa hela ,je kuna hatua ambazo zitachukuliwa dhidi ya wahusika ili iwe fundisho ??? Kuna kashfa kibao ikiwemo mambo ya rada ,tunasikia hela inarudishwa sasa hao wahusika inakuwaje wanapuyanga mitaani ??
   
 17. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #17
  Jul 3, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Hapa ndipo chama tawala kinapodhihirisha kuwa ni chama cha kipekee!

  Wahusika wengine nasikia wamechaguliwa kuwa waweka hazina wa chama. Eti wahusika wa EPA mpaka leo mashtaka na upelelezi haujakamilika.

  Ndiyo maana wapo wanaokipenda chama kwa kiburi sana! Mori huwapanda wanapoona kinabezwa, waweza kukuulimboka. Waweza kukutoa kwenye kiyoyozi wakakulaza mabwepande.

  Loh! Hili ni jinamizi letu watanzania au tusemeje sasa?
   
 18. O

  Original JF-Expert Member

  #18
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 326
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Msuya ndani ya list.
   
 19. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #19
  Jul 3, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,185
  Likes Received: 1,185
  Trophy Points: 280
  Kwa taarifa kama hizo kwa nini watumishi wasigome?
   
 20. Third Eye

  Third Eye JF-Expert Member

  #20
  Jul 3, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 332
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Sidhan kama hayo majina yatakuja,mana zilikofichwa kwenyewe ndo wanasifika kwa kusitiri wateja wao duniani,hilo ukijumlisha na kutokamatika kwao hapa nyumbani, ishu itaisha kimya kimya
   
Loading...