Sakata la mali za sharo milionea, polisi mnahusika

Binafsi nakuona kama una jazba. Walioitwa wezi ni wale waliokutwa na mali hizo, sasa ulitaka waitweje. Kwa nini waliondoka na mali za marehemu. Hivi ajali inapotokea, ukafika na ukaondoka na baadhi ya mali za marehemu, wewe uitweje. Nililivyomwelewa Kamanda huyo alitangaza hao waliokutwa na mali hizo kama wezi na siyo wananchi wote wa Tanga.....


Katalina kidogo naona hujampata Mtoaji mada!
Mimi navyomuelewa ni kwamba yeye anakelwa sana hata mimi pia,kwa police kusema eti walivyouweka mtego na wezi walivyorudisha mali za marehem sharo gafla wakasitukia kuwa ni mtego wakatokomea kusikojulikana.
Kitu ambacho mtoaji maada analalamikia hata mimi,hainiingii akilini kuwa police walishindwa kumkamata.
Police wanafanya tufikiri ni kusudi tu kuwa wao walipanga tu vitu vipatikane na kazi ya kuwatia mbaroni wezi kwa lengo la kukomesha vitendo vya unyama wa aina hiyo halikuwahusu.
 
Mwandishi yuko sahihi na uzoefu unaonyesha hivyo. Na isitoshe, ni kweli haiwezekani polisi aliejiandaa kimtego akimbiwe na kibaka asiejiandaa kwa mtego. Hapo ni kwamba wamewabana wakachukua cash na kuwaambia wapotee. Kwani wale wauza madini wa Morogoro ilikuwaje? Mshasahau mara hii? Wabongo bana.

Uzoefu unaonyesha kwamba ukiibiwa vitu lets say laptop na kulikuwa na document za muhimu, uchunguzi unaonyesha ukiwatumia polisi utapata hizo document zako ila laptop hutopata kwani vijiwe vyote vinavyouza vitu vya wizi wanavijua, sema tu kwa issue ya Sharo hapo wameonysha tu kwamba wapo sambamba na marehemu kuheshimu mchango wake lakini mara nyingi watakutoa hela na kukushauri kama umepata vitu vyako no need ya kufungua kesi na vitu kama hivyo. (ni kitu ambacho kinafanyika), polisi ninawaaminia sana kama wakiamua kufuatilia kitu lazima wafanikiwe tatizo lao hawawezi kufanya kazi bila kuhamasishwa na lazima wale hela kotekote kwa muahalifu na kwako ulieibiwa unless issue iwe sensitive sana hapo hakuna jinsi lazima waifikishe
 
Back
Top Bottom