Sakata la mali za sharo milionea, polisi mnahusika

Isango

R I P
Jul 23, 2008
295
450
Jeshi la Polisi mtabadilika lini?-Mmekula Hela ya Marehemu Sharo Milionea

Jeshi la polisi, tungependa mjue kuwa ninyi mnaishi katika jamii. Sio vizuri sana kuiona jamii ni ya watu wajinga sana kwa kiasi kwamba mnabeza hata uwezo wa jamii kuelewa vitu kwa akili ya kawaida bila kusoma sana. Jeshi la Polisi jifunzeni kwetu tunapoandika makala. Tunapoandika na kuitoa, tunajua inasomwa na watu wengi, wenye maarifa mbalimbali, hivyo inatuwia vigumu kuandika kwa kukurupuka. Unapoandika kitu kwa jamii, ujue jamii inayosoma suala hilo ina wasomi, ina wakulima, ina madaktari, ina polisi wenye akili, ina wana jeshi nk.
Ukiandika tamko la polisi likawa la kipuuzi, unadhalilisha jeshi. Tunafikiri na wengine hawana akili, lakini kumbe pengine sio. Sasa kwanini wewe uliyepewa jukumu la kukaa mezani kuandika kwa niaba ya Polisi uchafue jeshi zima kwa sababu za fikra ndogo?. Watu wanatilia shaka kuwa uteuzi wa majaji hauzingatii sifa, je na polisi uteuzi hauangalii hayo? Ni hatari sana kuongozwa na watu wenye maono madogo.
Pengine hata tunaposema, mauaji, vitendo vya kikatili, na vitendo vya watu kujichukulia sheria mikononi vinazidi. Vitendo hivi vinazidishwa pamoja na utendaji na matamko ya polisi ya kizembe kama hili ninalotaka watu waelewe uwezo wa polisi ulivyo.
Hivi majuzi tunatambua kuwa msanii mahiri wa filamu na muziki wa kizazi kipya nchini, Hussein Mkieti ‘Sharo Milionea’ alipata ajali, ajali hiyo ilipelelekea kifo chake, na watuw asio waungwana wakamwibia kabisa na kila mtu mwenye maadili mema akasitikishwa na kitendo hicho.
Tarehe 30/12/2012, jeshi la polisi lilitoa taarifa kuwa vitu vilivyoporwa na watu wasiojuliana katika ajali ya msanii mahiri wa filamu na muziki wa kizazi kipya nchini, Marehemu Hussein Mkieti ‘Sharo Milionea’ eneo la Songa Kibaoni wilayani Muheza mkoani Tanga, vimesalimishwa na wananchi wanaosadikiwa ni wezi. Hivi kweli wananchi ni wezi?, tunazumgumzia wananchi wenye hasira kali, kumbe ahta siku hizi tunaweza kusema wananchi wezi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, alithibitisha kupatikana vitu hivyo, ambako alisema upatikanaji wake ulitokana na msako mkali uliofanywa na uongozi wa serikali Muheza wakishirikiana na Jeshi la Polisi wilayani humo. Mpaka hapo hakuna shida, tunawapongeza kwa msako. Hii ni kazi nzuri
Kamanda alisema, baada ya kutokea kwa tukio hilo, Jeshi la Polisi mkoani Tanga, liliweka mtego na kutangaza kuinunua simu ya mkononi ya msanii huyo aina ya ‘blackberry’ ndipo moja kati ya wanaodaiwa vibaka waliohusika kwenye tukio hilo, alipojitokeza na kuipeleka kwa ajili ya kuiuza. Hii ni intelijensia nzuri, mliweka mtego, mwizi akaleta simu nako ni sawa. Tunamshukukru kachero aliyeweka mtego simu ikaletwea.
Kamanda alisema, wakati wezi walipofika eneo ambalo walikubaliana, walikabidhi simu hiyo kwa ajili ya kuikagua, lakini baadaye wezi hao walishtukia mtego huo na kukimbia huku wakiiacha simu hiyo. Hapo ndo huwa nakasirishwa na polisi. Walijua anayekuja ni mwizi, alipokimbia kwanini hawakumkamata? Kwanini hawakumfukuza? Hawakuwa na bunduki kumtishia? Kwanini mwizi amekimbia, na amekimbilia wapi? Polisi semeni vizuri kuondoa dhana kuwa mmehongwa kuwaachia watu wasio waungwana. Eti Mwizi amekimbilia kusikojulikana, kwanini wakati anakimbia askari hakukimbizana naye kwenda huko kusikujulikana ili kujulikane ni wapi? Kifalsafa nakataa
Kamanda hakuishia hapo ametaja vitu ambavyo vimesalimishwa kwa jeshi hilo kuwa ni simu ya mkononi aina ya blackberry, Betri la gari, tairi la akiba, radio ya gari, begi ambalo lilikuwa na nguo za marehemu, saa ya mkononi na nguo ambazo alikuwa amevuliwa na vibaka wa eneo hilo mara baada ya kutokea ajali hiyo. Mmesema Mwizi wa simu alikimbia, wa tairi la fari, na Yule wa betri, na Yule wa redio ya gari, na Yule wa begi la nguo. Wote hawa walikimbia, au polisi kweli mtaaminika lini kwa utendaji wa aina hii? Inasononesha sana lakini matamko kama haya yanazidisha hasira za wananchi, na kuongeza vitendo vya watu kujichukulia sheria mikononi. Badilikeni. Polisi kuvaa magwanda kuja kukaa kwa waandishi kuzungumza “hewa”. Iwe mwisho.

Naskia kulikua na mill 6 kwenye gari anampelekea mama yake ili aanzishe biashara,zi wapi hizi mpaka sasa?!.:A S cry:
 
Binafsi nakuona kama una jazba. Walioitwa wezi ni wale waliokutwa na mali hizo, sasa ulitaka waitweje. Kwa nini waliondoka na mali za marehemu. Hivi ajali inapotokea, ukafika na ukaondoka na baadhi ya mali za marehemu, wewe uitweje. Nililivyomwelewa Kamanda huyo alitangaza hao waliokutwa na mali hizo kama wezi na siyo wananchi wote wa Tanga.....
 
mwandishi anaamini polisi hawezi kuweka mtego wa kukamata mwizi na mtego huo ukashindwa kufanya kazi, anasema iweje polisi akimbiwe ,kwanini hakumfukuza , kwanini ,asimtishie kwa bunduki ili aweze kumkamata, mwandishi anaamini polisi anambio kuliko mwizi, mwandishi anaamini mwizi akikimbia polisi akitishia kwa bunduki mwizi atasimama mwenyewe na kurudi kwa askari ili ampeleke kituoni, mwandishi anasema eti ametorokea kusikojulikana , kwanini hawakumfuata na kujua huko kusiko julikana , binafsi labda kama mwandishi anao ushahidi mwingine alioamua kuuficha kwa sababu zake lkini kama ndo haya tunawaonea na kuwapandikizia chuki polisi zisizo na maana , dunia nzima polisi wanatorokwa licha ya kuwa na mavifaa kibao.
 
Polisi moro walimuhua marehemu jb (juma banatozi) na jamaa zake kisha wakawasachi wakakomba hela zote baadae wakatangaza vitu walivyokutwa navyo marehemu eti ni dola moja na shilingi mia ya kenya. Simu na hela zao wakagawana hao jamaa awahaniki kabisa kwenye maslai
 
pole sana japo kwa hii lugha uliyoandika hapa utadhani c mtanzania vile.
 
Jeshi la Polisi mtabadilika lini?-Mmekula Hela ya Marehemu Sharo Milionea

Jeshi la polisi, tungependa mjue kuwa ninyi mnaishi katika jamii. Sio vizuri sana kuiona jamii ni ya watu wajinga sana kwa kiasi kwamba mnabeza hata uwezo wa jamii kuelewa vitu kwa akili ya kawaida bila kusoma sana. Jeshi la Polisi jifunzeni kwetu tunapoandika makala. Tunapoandika na kuitoa, tunajua inasomwa na watu wengi, wenye maarifa mbalimbali, hivyo inatuwia vigumu kuandika kwa kukurupuka. Unapoandika kitu kwa jamii, ujue jamii inayosoma suala hilo ina wasomi, ina wakulima, ina madaktari, ina polisi wenye akili, ina wana jeshi nk.
Ukiandika tamko la polisi likawa la kipuuzi, unadhalilisha jeshi. Tunafikiri na wengine hawana akili, lakini kumbe pengine sio. Sasa kwanini wewe uliyepewa jukumu la kukaa mezani kuandika kwa niaba ya Polisi uchafue jeshi zima kwa sababu za fikra ndogo?. Watu wanatilia shaka kuwa uteuzi wa majaji hauzingatii sifa, je na polisi uteuzi hauangalii hayo? Ni hatari sana kuongozwa na watu wenye maono madogo.
Pengine hata tunaposema, mauaji, vitendo vya kikatili, na vitendo vya watu kujichukulia sheria mikononi vinazidi. Vitendo hivi vinazidishwa pamoja na utendaji na matamko ya polisi ya kizembe kama hili ninalotaka watu waelewe uwezo wa polisi ulivyo.
Hivi majuzi tunatambua kuwa msanii mahiri wa filamu na muziki wa kizazi kipya nchini, Hussein Mkieti ‘Sharo Milionea’ alipata ajali, ajali hiyo ilipelelekea kifo chake, na watuw asio waungwana wakamwibia kabisa na kila mtu mwenye maadili mema akasitikishwa na kitendo hicho.
Tarehe 30/12/2012, jeshi la polisi lilitoa taarifa kuwa vitu vilivyoporwa na watu wasiojuliana katika ajali ya msanii mahiri wa filamu na muziki wa kizazi kipya nchini, Marehemu Hussein Mkieti ‘Sharo Milionea’ eneo la Songa Kibaoni wilayani Muheza mkoani Tanga, vimesalimishwa na wananchi wanaosadikiwa ni wezi. Hivi kweli wananchi ni wezi?, tunazumgumzia wananchi wenye hasira kali, kumbe ahta siku hizi tunaweza kusema wananchi wezi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, alithibitisha kupatikana vitu hivyo, ambako alisema upatikanaji wake ulitokana na msako mkali uliofanywa na uongozi wa serikali Muheza wakishirikiana na Jeshi la Polisi wilayani humo. Mpaka hapo hakuna shida, tunawapongeza kwa msako. Hii ni kazi nzuri
Kamanda alisema, baada ya kutokea kwa tukio hilo, Jeshi la Polisi mkoani Tanga, liliweka mtego na kutangaza kuinunua simu ya mkononi ya msanii huyo aina ya ‘blackberry’ ndipo moja kati ya wanaodaiwa vibaka waliohusika kwenye tukio hilo, alipojitokeza na kuipeleka kwa ajili ya kuiuza. Hii ni intelijensia nzuri, mliweka mtego, mwizi akaleta simu nako ni sawa. Tunamshukukru kachero aliyeweka mtego simu ikaletwea.
Kamanda alisema, wakati wezi walipofika eneo ambalo walikubaliana, walikabidhi simu hiyo kwa ajili ya kuikagua, lakini baadaye wezi hao walishtukia mtego huo na kukimbia huku wakiiacha simu hiyo. Hapo ndo huwa nakasirishwa na polisi. Walijua anayekuja ni mwizi, alipokimbia kwanini hawakumkamata? Kwanini hawakumfukuza? Hawakuwa na bunduki kumtishia? Kwanini mwizi amekimbia, na amekimbilia wapi? Polisi semeni vizuri kuondoa dhana kuwa mmehongwa kuwaachia watu wasio waungwana. Eti Mwizi amekimbilia kusikojulikana, kwanini wakati anakimbia askari hakukimbizana naye kwenda huko kusikujulikana ili kujulikane ni wapi? Kifalsafa nakataa
Kamanda hakuishia hapo ametaja vitu ambavyo vimesalimishwa kwa jeshi hilo kuwa ni simu ya mkononi aina ya blackberry, Betri la gari, tairi la akiba, radio ya gari, begi ambalo lilikuwa na nguo za marehemu, saa ya mkononi na nguo ambazo alikuwa amevuliwa na vibaka wa eneo hilo mara baada ya kutokea ajali hiyo. Mmesema Mwizi wa simu alikimbia, wa tairi la fari, na Yule wa betri, na Yule wa redio ya gari, na Yule wa begi la nguo. Wote hawa walikimbia, au polisi kweli mtaaminika lini kwa utendaji wa aina hii? Inasononesha sana lakini matamko kama haya yanazidisha hasira za wananchi, na kuongeza vitendo vya watu kujichukulia sheria mikononi. Badilikeni. Polisi kuvaa magwanda kuja kukaa kwa waandishi kuzungumza “hewa”. Iwe mwisho.

ndugu mwandishi mgao ulikupita nini?ucjali mwisho wa mwaka huu dili kibao utatoka tu.
 
Unachofanya hapa ni kuhalalisha Uzembe wa Polisi, ni kuhalalisha kwamba Polisi wako sahihi kutuhadaa na kutufanya wajinga! Mtoa Mada ana hoja!
kinachonifurahisha ni kwamba polisi wa kiTanzania wan uwezo wa kuamua Kutorokwa na Wahalifu wote au Kuwanasa na kuwauwa wote hata kama niwengi kiasi gani... hapa hapako sawa!

mwandishi anaamini polisi hawezi kuweka mtego wa kukamata mwizi na mtego huo ukashindwa kufanya kazi, anasema iweje polisi akimbiwe ,kwanini hakumfukuza , kwanini ,asimtishie kwa bunduki ili aweze kumkamata, mwandishi anaamini polisi anambio kuliko mwizi, mwandishi anaamini mwizi akikimbia polisi akitishia kwa bunduki mwizi atasimama mwenyewe na kurudi kwa askari ili ampeleke kituoni, mwandishi anasema eti ametorokea kusikojulikana , kwanini hawakumfuata na kujua huko kusiko julikana , binafsi labda kama mwandishi anao ushahidi mwingine alioamua kuuficha kwa sababu zake lkini kama ndo haya tunawaonea na kuwapandikizia chuki polisi zisizo na maana , dunia nzima polisi wanatorokwa licha ya kuwa na mavifaa kibao.
 
Unachofanya hapa ni kuhalalisha Uzembe wa Polisi, ni kuhalalisha kwamba Polisi wako sahihi kutuhadaa na kutufanya wajinga! Mtoa Mada ana hoja!
kinachonifurahisha ni kwamba polisi wa kiTanzania wan uwezo wa kuamua Kutorokwa na Wahalifu wote au Kuwanasa na kuwauwa wote hata kama niwengi kiasi gani... hapa hapako sawa!
yawezekana mtoa mada yuko sahihi, ywezekana ww ukawa sahihi na yawezekana pia mimi nikawa sahihi, lkn ili nimuunge mkono mtoa mada basi labda aniongezee uthibitisho mwingine wenye ushahidi kwa kile anachoamini kimetendeka, vinginevyo aepuke uandishi wa kuhisi, afanye uandishi wa uchunguzi wenye hitimisho. naamini kuna kutorokewa mtuhumiwa kwa uzembe, kuzidiwa maarifa na kupangwa sasa mwandishi aje na hoja ya mashaka yake, nawe nadhani unanihukumu kukumbatia ufanyaji kazi wa uzembe sababu ya mwandishi kutotekeleza kazi yake ipasavyo, dunia nzima hayo ya uzembe, kuzidiwa maarifa na kupangwa hutokea kwenye vyombo vya ulinzi kabla ya kutoa lawama tujilizishe kwanza kipi kimefanyika kwa walinda usalama.
 
Mkuu pengine uko sahihi! mara nyingi mtoa mada kama hajaja nahoja zinazokidhi, tunamwambia kuwa hapa umepotosha (hili linawezekana tu kama tutakuja na hoja inayo nullify hoja za mwanzo). Unapaswa nawe kutuletea uchunguzi wako ili uweze kutuconvince kuwa mtoa uzi amepotosha na siyo kutumia nguvu na kudemanda yeye (mtoa mada) alete taarifa za ziada! Tupe uliyonayo ili tuweze kuamini kuwa tumepotoshwa. Tusifike sehemu tukahalalisha matatizo (udhaifu) wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kuwa ni vya kidunia (Global issues)!

Polisssm dhaifu kama ...............................Shameful!!
 
Mwandishi yuko sahihi na uzoefu unaonyesha hivyo. Na isitoshe, ni kweli haiwezekani polisi aliejiandaa kimtego akimbiwe na kibaka asiejiandaa kwa mtego. Hapo ni kwamba wamewabana wakachukua cash na kuwaambia wapotee. Kwani wale wauza madini wa Morogoro ilikuwaje? Mshasahau mara hii? Wabongo bana.
 
polis ana mazoezi, mwizi hana mazoezi, so polis lazima awe na mbio kuliko mwizi.

je mwizi wa nguo nae alitoroka?

wa spare tair je?
wa radio ya gar?
nk, nk

Je mill 6 alizokuwa nazo!!!
 
Mkuu pengine uko sahihi! mara nyingi mtoa mada kama hajaja nahoja zinazokidhi, tunamwambia kuwa hapa umepotosha (hili linawezekana tu kama tutakuja na hoja inayo nullify hoja za mwanzo). Unapaswa nawe kutuletea uchunguzi wako ili uweze kutuconvince kuwa mtoa uzi amepotosha na siyo kutumia nguvu na kudemanda yeye (mtoa mada) alete taarifa za ziada! Tupe uliyonayo ili tuweze kuamini kuwa tumepotoshwa. Tusifike sehemu tukahalalisha matatizo (udhaifu) wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kuwa ni vya kidunia (Global issues)!
mkuu data zaidi hakika sina,ila mtoa mada alikuwa pale, ambapo wlipokea taarifa ,lilikuwa ni jukumu lake kuuliza maswali yale ambayo aliona wazi kuwa yanautata ili atufikishie ujumbe ulio na ushahidi, nakubaliana nawe kuwa ktk khali ya kawaida [mtizamo wa sisi raia] hawezi kuzidiwa ujanja na muhalifu, mf; ktk maelezo ya mwandishi ametoa changamoto kwanini, hawakumtishia kwa kupiga risasi ni ushauri mzuri lkn bila kuuliza swali hilo kwa aliyewapa taarifa, huwezi kujua ni kwanini? hawakufanya hivyo, yote kwa yote uzembe kazini haukubaliki .
 
ndugu mwandishi mgao ulikupita nini?ucjali mwisho wa mwaka huu dili kibao utatoka tu.

wakazi wa manzese utawajua tuh..!!

Hapo usikute ni tayari keshamwagiza mkewake amwandalie ugali nayeye anarudi na vichwa + miguu ya kuku,,,

thinking capacity inatia shaka sana
 
Kwani kukaa manzese tatizo, wewe unayekaa huko uliko mwisho wa siku wote ni mavumbini

wakazi wa manzese utawajua tuh..!!

Hapo usikute ni tayari keshamwagiza mkewake amwandalie ugali nayeye anarudi na vichwa + miguu ya kuku,,,

thinking capacity inatia shaka sana[/QUOTE]
 
Ilishatangazwa toka awali kwamba waliohusika na wizi ule wasalimishe zile mali na hawatachukuliwa hatua lakini kama hawakujisalimisha msako mkali ungefanyika na kuwakamata wahusika na kuwashitaki. Sasa hapa watu wamesalimisha na hawakusakwa ni kama vile ilani inavyotolewa ya kusalimisha silaha zinazomolikiwa kiholela. ukisalimisha hushitakiwi.
Mimi bunafsi hapa sioni tatizo kwa Polisi kwa sababu kauli ya Mkuu wa Wilaya ndiyo ilivyosema.
 
kwani kukaa manzese tatizo, wewe unayekaa huko uliko mwisho wa siku wote ni mavumbini

wakazi wa manzese utawajua tuh..!!

Hapo usikute ni tayari keshamwagiza mkewake amwandalie ugali nayeye anarudi na vichwa + miguu ya kuku,,,

thinking capacity inatia shaka sana
[/quote]

sijakataa ya kwamba wote ni wa mavumbini

ila waache basi tabia ya kula miguu + vichwa vya kuku,,ile athari wanayoipata si unaiona??
 
Back
Top Bottom