Sakata la Makinikia: Kuna aibu inatunyemelea

Mkuu tani moja ina kilo ngapi? kwa mahesabu yangu dola elfu kumi inanunua kilo 275 ya dhahabu
kwa gharama ya shilingi milioni themanini kwa kilo.Huenda nimekosea naomba nisahihishe.
Wakati unaninukuu nilikuwa narekebisha hesabu zangu kuna sehemu nilikosea kilo 250 niliita tani 25.

Lakini hesabu za mwisho za dola milioni 10 kujaza almost 20% ya cintainer la 40ft with pure gold yako sawa tangu awali kwa sababu nilifanya hesabu kwa density na bei ya dhahabu na ujazo wa container.
 
Isije ikawa ni hearsay stories ya watu wa vijiweni, need credible source. Sikatai post yako, hapana, tunataka uhakika wa source kama ni credible

Ona hii sasa ( ni uzi nimekopi JF for easy of reference, na uzi link nimeiweka chini.)
Nimeshangaa ile kamati ya pili iliyosheheni walimu wa chuo kikuu wameshindwa kutofautisha ACCACIA kama brand name iliyosajiliwa huko nje ikiwa na sub contract na Bulyanhulu Gold mine Tanzania.

Cha kusikitisha kwenye ile kamati alikuwepo mtu wa TRA tena afisa mwandamizi anayejua kodi hawakusanyi kwa jina la ACCACIA kama brand name bali wanakusanya kama Bulyanhulu Gold mine.

Kwa ufupi nina mashaka na uelewa wa huyu Profesa anayefundisha mambo ya Oligopolistic competition huko chuo kikuu,Kamati imemdanganya Raisi kweupe kuwa ACCACIA as brand name inafanya kazi kinyume cha sheria,

Profesa ameshindwa kuelewa ACCACIA sio kampuni bali wanafanya kazi na sub contractors kama Bulyanhulu Gold mine na zingine nyingi zilizopo huko mgodini
Kamati ya Profesa Osoro na uelewa wa Multinational Corporatios
Andiko langu labda umeogopa kulisoma ukakimbilia kutoa maoni,
ni tofauti kabisa na huu ulioweka. Mimi nimeweka uhalisia wa kinachofanyika
mgodini,na kama kuna unalolijua sahihisha kwa kuweka wewe uzalishaji wa
kiwanda kwa siku,na pia makinikia ni nini? ni udongo wote unaobaki
baada ya kutoa dhahabu au ni udongo maalum baada ya kutoa dhahabu?
 
Hawa jamaa kweli watakuwa wametuibia lakini findings za kamati hizi kuhusu viwango vya madini na hasara tuliyopata, mimi binafsi zinanipa mashaka sana na ninaona tunaweza kuja kuumbuka hapo baadae.

Ni hivi,kama mchanga tu unaweza kuwa na madini ya thamani ya trilioni mpaka 380.9 kwa kiwango cha juu kwa miaka hiyo 19,ni wazi nchi zenye rasilimali madini duniani na zenye mikataba mizuri zingekuwa ni nchi tajiri sana katika huu ulimwngu.

Cha kujiuliza, kama hiyo ni thamani ya makinikia tu,madini yenyewe(matofali ya dhahabu) yatakuwa na thamani kiasi gani kwa miaka yote hiyo?

Alafu kingine cha kujiuliza ni kwanini findings za kamati hizi mbili za sasa na ile ya Jaji Bomani zitofautiane katika data za viwango vya madini tu lakini zifanane katika matokeo mengine ikiwemo na mapendekezo?Tukumbuke hata hadidu za rejea zimeonekana kufanana kwa maelezo ya Lissu aliyoyatoa Bungeni jana huku akiwa na ripoti ya Jaji Bomani mkononi.

Kubiwa ni kweli tumeibiwa lakini hivyo viwango vya madini vilivyotajwa katika hizo ripoti inabidi tujiulize mara mbili mbili kama kweli vina uhalisia na hali ya nchi zingine zenye migodi tena kutuzidi.

Hizi ripoti hawa mabwana wanaweza kuzitafsiri kama ni defamatory kwao na hivyo tunaweza kuwa sued for defamation japo wametubia unless tuthibitishe usahihi wa hivyo viwango vya madini.
Huku ni kutapatapa kwa mfa maji. Hakuna kurudi nyuma. Mpaka kieleweke. Umaskini wetu ni wakujitakia, na unasababishwa na mawazo kama haya.
 
Wakati unaninukuu nilikuwa narekebisha hesabu zangu kuna sehemu nilikosea kilo 250 niliita tani 25.

Lakini hesabu za mwisho za dola milioni 10 kujaza almost 20% ya cintainer la 40ft with pure gold yako sawa tangu awali kwa sababu nilifanya hesabu kwa density na beibya dhahabu na ujazo wa container.
Ok asante.
 
Makontena yameshfunguliwa,kwa hiyo wameshacheza na ushahidi,ni sawa mtu kafa kijinai wewe ukambebe,akija mtu wa ku-collect DNA sample lazima atakuta salama zako,kontena ufungue wewe bila kuniita,ulifunge wewe, halafu uniambie nikuamini

Exactly. Kwanini wasinge tumia "indipendent body" tokea mwanzo kupima wakiwepo na reps wa ACACIA?
 
Takwimu zimepikwa

Sasa wewe umeangalia makontena mwaka 2017,

Unaweka majumuisho ya jumla eti kwa kuwa 2017 tumekuta hasara hii,basi tuweke assumption kwamba ulikuwa unafanya hivyo kila Siku

Yaani kama umeiba ngombe mmoja mwaka 2017,basi tunasema kila mwaka ulikuwa unaiba ngombe mmoja,

Ushahidi wa kwamba makinikia ya mwaka 2016,2015,2014,2013,2012,2011,2010 mpaka 1998 jamaa walikuwa wanafanya kosa lilelile na kwa kiwango kilekile bila kukosea wala kuzidi wala kupungua,je tuna evidence za makontena ya mwaka 1998,1999,2000,2001,2002......mpaka 2016?

Nani alichukua sample za mwaka 1998?1999?2000?

Unatumia sample ya 2017 kutoa hukumu kwa suala la 1998,2010.....

Exchange rate zilikwaje?thamani ya Dhahabu ilikuwaje?

Tunafanyiwa usanii
Hakuna sehem iliyosomwa bila kiwango cha juu na kiwango cha chini
 
Hawa jamaa kweli watakuwa wametuibia lakini findings za kamati hizi kuhusu viwango vya madini na hasara tuliyopata, mimi binafsi zinanipa mashaka sana na ninaona tunaweza kuja kuumbuka hapo baadae.

Ni hivi,kama mchanga tu unaweza kuwa na madini ya thamani ya trilioni mpaka 380.9 kwa kiwango cha juu kwa miaka hiyo 19,ni wazi nchi zenye rasilimali madini duniani na zenye mikataba mizuri zingekuwa ni nchi tajiri sana katika huu ulimwngu.

Cha kujiuliza, kama hiyo ni thamani ya makinikia tu,madini yenyewe(matofali ya dhahabu) yatakuwa na thamani kiasi gani kwa miaka yote hiyo?

Alafu kingine cha kujiuliza ni kwanini findings za kamati hizi mbili za sasa na ile ya Jaji Bomani zitofautiane katika data za viwango vya madini tu lakini zifanane katika matokeo mengine ikiwemo na mapendekezo?Tukumbuke hata hadidu za rejea zimeonekana kufanana kwa maelezo ya Lissu aliyoyatoa Bungeni jana huku akiwa na ripoti ya Jaji Bomani mkononi.

Kubiwa ni kweli tumeibiwa lakini hivyo viwango vya madini vilivyotajwa katika hizo ripoti inabidi tujiulize mara mbili mbili kama kweli vina uhalisia na hali ya nchi zingine zenye migodi tena kutuzidi.

Hizi ripoti hawa mabwana wanaweza kuzitafsiri kama ni defamatory kwao na hivyo tunaweza kuwa sued for defamation japo wametubia unless tuthibitishe usahihi wa hivyo viwango vya madini.
mkuu...am not bragging, lakini mimi ni mtaalamu wa eneo hili.

ninakuhakikishia kwa 110% kuwa findings za kamati # 1 (from technical perspective) siyo sahihi, labda kama walitumia sampuli walizozitengeneza wenyewe!

kama kamati # 2 ilitumia findings za # 1, nayo ni bomu lingine.

mkuu tukale mkao wa kuteswa tu kama hawa jamaa watatupeleka mahakamani. ila uzuri ni kwamba mengi ya makampuni haya makubwa huwaga hayapendi kwenda mahakamani ingawa yanajua yatashinda.
huwaga yana-prefer amicable but win-win conclusion, ingawa sisi ndiyo tutakaoliwa zaidi, but si kwa kiasi ambacho kinalingana na kushitakiwa mahakamani.
 
Ok asante.
Dhahabu bei yake leo ni takriban $40 per gram (rounding from $40.77).

That is $40,000 per kilo of pure gold in theory.

$10,000 unapata kilo 0.25 za pure gold.

$10,000,000 unapata kg 250 za pure gold.

Container la mchanga kutumia $ 10 mil kuliokoa inabidi liwe na kama 20% pure gold by volume.

*Nime round off bei kutoka $ 40.7 per gram to $ 40.

*Nimefanya hesabu za pure gold
 
Hakuna sehem iliyosomwa bila kiwango cha juu na kiwango cha chini
Sasa nenda mahakamani ukaseme kontena la mwaka 1998,lilikuwa na kiwango Fulani,tofauti na la mwaka 2011,na utwambie sampuli za 1999 ulimtuma nani akazichukue na akazipima katika maabara gani mbele ya nani
 
mkuu...am not bragging, lakini mimi ni mtaalamu wa eneo hili.

ninakuhakikishia kwa 110% kuwa findings za kamati # 1 (from technical perspective) siyo sahihi, labda kama walitumia sampuli walizozitengeneza wenyewe!

kama kamati # 2 ilitumia findings za # 1, nayo ni bomu lingine.

mkuu tukale mkao wa kuteswa tu kama hawa jamaa watatupeleka mahakamani. ila uzuri ni kwamba mengi ya makampuni haya makubwa huwaga hayapendi kwenda mahakamani ingawa yanajua yatashinda.
huwaga yana-prefer amicable but win-win conclusion, ingawa sisi ndiyo tutakaoliwa zaidi, but si kwa kiasi ambacho kinalingana na kushitakiwa mahakamani.
Mkuu tafuta copy ya UK-bribery act,utagundua kwamba makampuni yote
yaliyosajiriwa uingereza ni kosa kisheria kufanya udanganyifu
wa aina yoyote kwenye nchi hasa kama zetu kwa kuwatumia/kuwaonga maofisa wa
serikali.Sasa basi kama kiwango cha dhahabu kilichotajwa na kampuni
hii kuwepo kwenye makanikia ni tofauti na uhalisia wa kilichomo
hilo linatosha kuishushia hadhi kampuni husika na hata kupigwa faini
kama ilivyotokea kwa issue ya Rada.Ila tusubiri tuone.
Mtu anayeogopa kwenda mahakamani wakati amefanyiwa kosa
mara nyingi huwa ni mhalifu.
 
Ni hivi,kama mchanga tu unaweza kuwa na madini ya thamani ya trilioni mpaka 380.9 kwa kiwango cha juu kwa miaka hiyo 19,ni wazi nchi zenye rasilimali madini duniani na zenye mikataba mizuri zingekuwa ni nchi tajiri sana katika huu ulimwngu.
Mimi nasema hivi, matajiri wanaofanya biashara za kuchimba madini wangekuwa ndio matajiri wakubwa zaidi duniani na sio hawa akina Bill Gates!!!

Lakini cha ajabu, leo Bill Gates hata akiuza mali zake zoooooote bado hawezi kufikisha hizo Trillion 380!

Hata kama Bill Gates na Warren Buffet wanauza mali zao zote bado hawawezi kupata hizo Trillion 380. Bill Gates na Buffet ndio Top 2 Richest People duniani
 
Unalinganisha kamati ya Bomani iliochukua data kutoka kwenye makaratasi yaliyoandaliwa na GST halafu unalinganisha na kamati iliyofanya sampling katika Makontena yaliyodakwa?

Nadhani utakuwa ni muhitimu wa Chuo cha kata.

Pili unaongeleaje uwepo wa Bi kejo ndosi ndani ya kamati ile?

Tatu Kamati ya Bomani iliongelea madini nyeti kama Rhadium??

Wasaliti wakubwa mnaohangaika na simu usiku wa manane kwa kuhongwa na Acacia
well said. Hii ya sasa ina uhalisia
 
Kuna wakati kontena la makinikia lilizama bandarini, hao jamaa walitumia zaidi ya dollar milioni kumi kuliopoa.
Swali langu, kulikua na zahabu kiwango gani humo?

Hadithi za vijiweni hizo.
 
Mimi nasema hivi, matajiri wanaofanya biashara za kuchimba madini wangekuwa ndio matajiri wakubwa zaidi duniani na sio hawa akina Bill Gates!!!

Lakini cha ajabu, leo Bill Gates hata akiuza mali zake zoooooote bado hawezi kufikisha hizo Trillion 380!

Hata kama Bill Gates na Warren Buffet wanauza mali zao zote bado hawawezi kupata hizo Trillion 380. Bill Gates na Buffet ndio Top 2 Richest People duniani
Ndio maana nasema tusubiri kuumbuka.Huu utajiri ni wa kufikirika tu na wala haupo.

Yaani makinikia yawe na uwezo wa kutoa malori zaidi ya 300 ya pure gold kwa miaka 19 hapo hajugusa pure gold?Huu utajiri upo kweli?!
 
Hizi report zinawafaa zaidi watu wajinga, wasio na uelewa wa uchumi kwa ujumla. Kwa mwenye akili, hata kama hujui kuwa tumeibiwa au hatukuibiwa, au tumeibiwa kiasi gani, angalao utajua kuwa report hizi mbili hazina uhalisia hata kidogo. Suala hili la mchanga huenda ajenda yake kubwa ni manufaa ya kiasi kuliko manufaa ya kiuchumi.

Kama tuna nia ya kushinda, ilikuwa ni muhimu kutumia taarifa sahihi zenye uhalisia kuliko hizi zilizovuka kiwango cha uwongo. Report hizi kwa ujumla zinatudhalilisha kwa kiwango fulani. Na hii huenda ndiyo sababu kubwa kwa nini serikali haitaki kumpa mtuhumiwa nakala ya report, na kukimbilia kutaka kuzungumza.
 
Kwa hesabu za Acacia, ili tuwadai matrilioni hayo inabidi wao wamechuma mazilioni na kuwa wachimbaji wakubwa dunian
Hii nchi ina wasomi vi.laza hadi unaweza kujisikia aibu!!!

Hata kama tunawadai Trillion 200... ina maana kwa mwaka pesa ya kuja kwetu peke yako ni zaidi ya Trillion 5. Kama ya kwetu peke yake ni Trillion 5, tuta-assume kwa mwaka wanatengeneza Trillion 15 na wao wanabaki na Trillion 10 kwa mwaka! Hapo hazijaongezwa na zile zisizotokana na makinikia!

Ni mwendawazimu peke yake ndie anaweza kuamini kitu kama hicho kwa sababu, hata ukichukua kampuni ya Barrick Gold yooooooooote kwa ujumla wake, let alone Acacia; bado hawana ubavu wa kutengeneza trillion zote hizo kwa mwaka!!!

Lakini leo tunaambiwa makinikia tu kwa mwaka yanazalisha kiasi hicho cha pesa na watu wanashangilia!!!
 
Mimi naona mheshimiwa rais afanye kimya kimya tu maana anaweka mambo wazi ili wananchi wajue anaonekana muongo. Kwasababu tumeshazoea kuibiwa
 
Hizi report zinawafaa zaidi watu wajinga, wasio na uelewa wa uchumi kwa ujumla. Kwa mwenye akili, hata kama hujui kuwa tumeibiwa au hatukuibiwa, au tumeibiwa kiasi gani, angalao utajua kuwa report hizi mbili hazina uhalisia hata kidogo. Suala hili la mchanga huenda ajenda yake kubwa ni manufaa ya kiasi kuliko manufaa ya kiuchumi.

Kama tuna nia ya kushinda, ilikuwa ni muhimu kutumia taarifa sahihi zenye uhalisia kuliko hizi zilizovuka kiwango cha uwongo. Report hizi kwa ujumla zinatudhalilisha kwa kiwango fulani. Na hii huenda ndiyo sababu kubwa kwa nini serikali haitaki kumpa mtuhumiwa nakala ya report, na kukimbilia kutaka kuzungumza.
You're right!! Sote sisi tunaamini kabisa kwamba tunaibiwa! Lakini kwa viwango vinavyotajwa, wallah vinatia doa elimu yetu hasa ukizingatia hizi ripoti eti zimefanyiwa kazi na wahadhiri wa vyuo vikuu!!!

Na kama ulivyosema, it's purely for political benefit na wala sio kiuchumi!!!!
 
Ile ripoti mie niliiona ya uongo tokea msomaji alipokuwa akikosea maneno aliyoyaandika yeye na kuyapitia
 
Ndio maana nasema tusubiri kuumbuka.Huu utajiri ni wa kufikirika tu na wala haupo.

Yaani makinikia yawe na uwezo wa kutoa malori zaidi ya 300 ya pure gold kwa miaka 19 hapo hajugusa pure gold?Huu utajiri upo kweli?!
Mbona tushaumbuka tayari.
 
Back
Top Bottom