Sakata la Makinikia:Kamati zinadanganya kwa maslahi ya nani?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
48,785
102,156
Hamjambo wanaJF
Niende kwenye hoja

Madini yenye mgogoro ni haya makinikia ya mchanga unaosafilishwa nje ya nchi na mgodi wa ACACIA ambapo kwa mujibu wa tume zilizoundwa na rais wametuambia kuwa mchanga huu wa makinikia una asilimia 5 ya madini na hizi asilimia 5% za madini tumepoteza trion 108 kwa miaka 18.

Kwamba migodi mingine kama ya Geita na maeneo mengine hayajabuguziwa kwa sababu dhahabu inasafishiwa mgodini hapahapa nchini na haidaiwi.

Kwa tafsiri ya haraka ni kwamba hii asilimia 95% ya dhahabu inayosafishiwa mgodini ACACIA hapahapa nchini haidaiwi na serikali,Yani imelipa kodi ndio maana haipigiwi kelele ...Sasa tupige hesabu hii asilimia 95% inayosafishiwa nchini hapahapa serikali inaiingiza shilingi ngapi kupitia dhahabu hii?

Kama mchanga wa makinikia unaosafilishwa nje ya nchi una asilimia 5% ya madini tu lakini tumepoteza trion 108 kwa miaka 18,Je hiyo aslimia 95% iliyosafishiwa hapahapa nchini serikali imeingiza shilingi ngapi kwa miaka 18?

Asilimi 5% kwa miaka 18 = trion 108
Asilimia 95% kwa miaka 18 = trion 2052 Yani serikali kwa miaka 18 imeingiza trion elfu mbili na hamsini na mbili kwa madini yanayosafishiwa mgodini kwa mgodi mmoja wa ACACIA.Pesa hizi anazo MUNGU tu hata marekani na utajiri mkubwa walionao hawajawahi kumiliki pesa hii .Swali la kujiuliza kama mlikuwa mnaingiza pesa zote hizo hili deni la taifa lilikuwa linaongezekaje?Kwa nini miradi ilikwama kwa kukosa fedha wakati mnaingiza fedha zote hizi?okay sio kesi hebu katika hizo trion 2052 lipeni deni la taifa trion 50 basi.

Trion 2052 ni sawa na bajeti ya tanzania miaka 51 kama bajeti itatengwa trion 40 kila mwaka.Yani miaka 51 tunatumia pesa za madini tu bila kulipa kodi za majengo,magari,maduka na kila kitu na maendeleo yanasonga.

Mfumo wetu wa elimu una matatizo makubwa sana.

Nnadiriki kusema siuamini hata chembe usomi wa waliondaa zile ripoti kama ni wa viwango.

Nnakuhakikishia ukizichunguza kwa makini hizo ripoti utakuta asilimia kubwa ni kopi na pesti na kuweka mahesabu kwenye Excel jibu linalotoka hata kama haliingii akilini ndiyo hilo hilo mradi Excel imefanya calculations.

Acacia hawana cha kulipa, sana sana tutakuja kuwaomba msamaha watusamehe wasitudai kwa kuwapotezea muda, faida na kuharibu jina lao.

Mtayakumbuka haya. Nilisema kama haya kwa Dowans na ndivyo ilivyokuwa.

Mara nyingi humu huwa nnautoa mfano wa msomi Nyerere na Tiny Rowlands lakini wengi hawanielewi.
 
Hamjambo wanaJF
Niende kwenye hoja

Madini yenye mgogoro ni haya makinikia ya mchanga unaosafilishwa nje ya nchi na mgodi wa ACACIA ambapo kwa mujibu wa tume zilizoundwa na rais wametuambia kuwa mchanga huu wa makinikia una asilimia 5 ya madini na hizi asilimia 5% za madini tumepoteza trion 108 kwa miaka 18.

Kwamba migodi mingine kama ya Geita na maeneo mengine hayajabuguziwa kwa sababu dhahabu inasafishiwa mgodini hapahapa nchini na haidaiwi.

Kwa tafsiri ya haraka ni kwamba hii asilimia 95% ya dhahabu inayosafishiwa mgodini ACACIA hapahapa nchini haidaiwi na serikali,Yani imelipa kodi ndio maana haipigiwi kelele ...Sasa tupige hesabu hii asilimia 95% inayosafishiwa nchini hapahapa serikali inaiingiza shilingi ngapi kupitia dhahabu hii?

Kama mchanga wa makinikia unaosafilishwa nje ya nchi una asilimia 5% ya madini tu lakini tumepoteza trion 108 kwa miaka 18,Je hiyo aslimia 95% iliyosafishiwa hapahapa nchini serikali imeingiza shilingi ngapi kwa miaka 18?

Asilimi 5% kwa miaka 18 = trion 108
Asilimia 95% kwa miaka 18 = trion 2052 Yani serikali kwa miaka 18 imeingiza trion elfu mbili na hamsini na mbili kwa madini yanayosafishiwa mgodini kwa mgodi mmoja wa ACACIA.Pesa hizi anazo MUNGU tu hata marekani na utajiri mkubwa walionao hawajawahi kumiliki pesa hii .Swali la kujiuliza kama mlikuwa mnaingiza pesa zote hizo hili deni la taifa lilikuwa linaongezekaje?Kwa nini miradi ilikwama kwa kukosa fedha wakati mnaingiza fedha zote hizi?okay sio kesi hebu katika hizo trion 2052 lipeni deni la taifa trion 50 basi.

Trion 2052 ni sawa na bajeti ya tanzania miaka 51 kama bajeti itatengwa trion 40 kila mwaka.Yani miaka 51 tunatumia pesa za madini tu bila kulipa kodi za majengo,magari,maduka na kila kitu na maendeleo yanasonga.
Chadema mmevurugwa kabisa!
 
Asante mkuu,watu wanaumbuka hapa,

Na hapo hujagusa migodi ile mingine ambayo haina makinikia

Aibu kwa maprofesa walioongoza hizo kamati
Ila kama mtu una hela peleka watoto wako vyuo vikuu ulaya,marekani na south afrika,

Sasa hao ma profesa si huwa wanafundisha uongo madarasani?

Kama kwa nchi nzima wanasema hivyo,madarasani je?
 
Mkuu, hata hii ni siasa ujue. Ni uwezo wa mtu kucheza na akili za watu.
Unacheza na akili za watu wakati unaiweka nchi katika hatari ya kudaiwa matrilioni?

Yaani hizo nafasi wameaminiwa na watanzania ili wakacheze na sio kufanya kazi?
 
Na

Nani adaiwe? Hivi unamuona jpm kilaza kama mashinji! au lisu. Jpm huko vizuri kila kitu anakielewa mwanzo na mwisho wake. Upinzani mashakani kufutika ndo mana mnaweweseka na jpm hawapi poo
 
Kama yuko vizuri,ile meli ya kigamboni iko wapi?

Mbona ndege moja haipai mpaka sasa?

Mbona wachina wa samaki walimpiga mahakamani na wanadai fidia?
 
bd8b4b270ed51152189dd5973fb88050.jpg
 
Nchi hii bana kila mtu ni mtaalam wa kila jambo! maana huyu anasema hili anakuja na data zake, atakuja mwingine atapinga kwa data zake!, sasa sijuwi tumuamini nani maana sisi wengine ni maamuma tu.
 
24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom