Sakata la Makinikia: Balozi Juma Mwapachu anajiondoaje ktk "lawama za kuingamiza" Tz kwa wawekezaji?

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,676
2,000
image.jpeg


Juu ya meza ya mazungumzo kati ya wataalamu wa Tanzania na ACACIA katika kuelekea makubaliano ya namna ya kulipana kilichopotea,bila shaka yupo Mtanzania mmoja tu kwa upande wa ACACIA.Huyu ni mwana wa Tanzania, mwanamajumuhi na mwanadiplomasia mbobezi, ni JUMA V. MWAPACHU.Balozi wetu wa zamani wa Ufaransa,Katibu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na mwanafasihi/mshairi kindakindaki.

Haya ya "Meza ya mazungumzo" siyo yanatokea wakati uzalishaji na usafirishaji wa dhahabu umesimama!La hasha!!Kila kitu kipo sawa isipokuwa "mchanga wa dhahabu" uliopo kwenye makasha pale bandarini ndio umesitishiwa safari zake kwenda nje ya nchi

Katika migodi yao yote usafirishaji wa dhahabu unaendelea,ukusanyaji wa dhahabu toka katika migodi yao yote ya Tanganyika unaendelea,na dhahabu zote kukusanywa katika jiji la Mwanza kabla ya kuchukuliwa Mwanza kwa pamoja na kupelekwa Dsm tayari kwa kupelekwa sokoni nje ya nchi.Kuna sababu za kiusalama zilizofanya ACACIA kukusanya madini yote Mwanza toka migodini kabla ya kuisafirisha na ndege kwenda nje kupitia uwanja wa Dsm.

Mkufunzi wangu wa "mbinu za uandishi" na mtaalamu wa picha za ndege(birds) Chuo Kikuu Dsm,Ndugu Kayoka aliandika kuwa "Robert Greene katika kitabu chake cha "33 Strategies of War." amaeelezea mbinu za mapambano katika "vita",katika mbinu zote 33,kuna mbinu ya 21,bila shaka hawa ACACIA ndiyo wanaitumia mbinu hiyo"

Inaitwa "The Diplomatic-War Strategy." Falsafa yake ni "Negotiate while advancing." Do they still advance? Bado wanachimba dhahabu? Kila kitu bado wanaendelea nacho isipokuwa tu ule mchanga?Jibu ni NDIYOOOO...Hawa jamaa bado wanaendelea na kila kitu cha uzalishaji,usafirishaji na uuzaji wa dhahabu huku duniani,isipokuwa tu ule "mchanga" pale bandarini.THEY ARE NEGOTIATING WHILE ADVANCING....

Tupelekeni watu wetu shule,mambo ya Negotiation siyo siasa za kina Lusinde Kibajaji na Msukuma wa Geita.Hapa tukiingiza siasa tunaliwa mchana kweupe,itakuwa ni mambo ya jazwa ujazwe.Tatizo tunawekeza sana katika siasa,ndiyo maana hata kule kwenye kuwajadili hawa Accacia na mikataba yao,tunapeleka watu wanaojua kusoma na kuandika tu.

Katikati ya jopo la majadiliano kama haya,Tanzania tupeleke wasomi wa mambo yafuatayo kwa umuhimu wake,kwanza ni "Interantional Trade Law,Foreign Trade Administration,International Commercial Contract,International Marketing,World Commercial Law,International Bussiness English,International Trade Payments,Overseas Marketing Studies,Interantional Politics,Bussines Negotiation Skills pamoja na International Diplomatics"

Balozi Juma Mwapachu alichaguliwa kama "INDEPENDENT NON EXECUTIVE DIRECTOR" na kampuni ya Barrick Gold Corporation kwa miaka kadhaa,huyu amekuwa "sehemu fulani" ya uendeshaji wa kampuni ya Barrick Gold Corporation hapa Tanzania kwa namna ya "kimvuli".Sasa nimeona Balozi Mwapachu ni mjumbe wa board ya Accacia.

Haya makampuni makubwa ya "kibeberu" yana mbinu nyingi sana za kupenyeza ushawishi na kukatiza katika kuta ngumu za ofisi za serikali,ambazo kwa kawaida inakuwa ngumu kupita na kufika mpaka ndani,hizi "Multilateral Companies" hutengeneza vyeo kama hivi vya "NED au NXD" kama hicho cha Juma Mwapachu ili kuweza kupata mtu watakayemtumia kutangulia mbele wakati wa kupenyeza ushawishi wao katika mikataba na fursa mbalimbali ya nchi wanayotaka kuwekeza.

Sifa kubwa ya "INED" ni lazima awe na ushawishi wa kisiasa,kijamii na kiitifaki ndani ya nchi wanayowekeza,wanapenda kumpata mtu yule ambaye katika sekta ya umma ana ushawishi na katika sekta binafsi ana ushawishi,sifa hizi zote,mwanadiplomasia Juma Mwapachu anazo.Juma amekuwa Founding Secretary General wa Chamber of Commerce,Industry and Agriculture,pia alikuwa Chairman of the Confideration of Tanzania Industries 1996-2000.Sifa hizi ni wazi zinamuonyesha Balozi Mwapachu kuwa mtu sahihi mwenye uzoefu uliotukuka katika sekta ya umma na ile ya binafsi.

Balozi Juma Mwapachu amefanya kazi na Mwalimu Nyerere,Juma Mwapachu amekaa meza moja na Ally Hassani Mwinyi,Juma Mwapachu ni mshirika wa kiungozi wa Ben Mkapa,huyu Juma Mwapachu ni mteuliwa toka 2002-2006 kama balozi wetu kule Ufaransa,na baadae wakati wa Jakaya Kikwete alikuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,unaachaje kumpa hiyo nafasi ili apite katika "kuta ngumu" za ofisi za serikali kukupitishia ushawishi wako kiuwekezaji?

Kwa uelewa zaidi,moja ya kazi kubwa ya "Independent Non-Executive Director" ni kusimamia kazi yake kama "External Communicator" wa kampuni na wadau wa nje(Third parties),ambayo kwa nchi za kiafrika huwa ni serikali zilizopo madarakani.Kuhakikisha kuwa vile vizingiti ambavyo wazungu wameshindwa kupita sababu ya uelewa mdogo wa siasa za ndani ya nchi,uelewa mdogo wa "bussiness behaviour" ya ndani ya nchi na hata kukosa "connection" ya kujua nani wa kumtuma kuonana na Waziri wa viwanda au waziri wa Nishati na Madini,basi INED hutumika kukatiza katika vizingiti hivi kwa niaba ya kampuni.

Mtaalamu mmoja wa ushawishi wa siasa za makampuni ya kibeberu anasema,moja ya kazi kubwa ya "Independent Non Executive Director" ni kuhakikisha yafuatayo:

"The company’s and board’s effectiveness can benefit from outside contacts and opinions. Therefore it can be an important function of a Non-Executive Director to help ‘connect’ business and board with networks of potentially useful people and organisations within a country.In some cases, the non-executive director will be called upon to represent the company externally."

Kwa tafsiri ya haraka,utaona kuwa kazi kubwa ya huyu INED,ni kuhakikisha kuwa ile kampuni aliyopewa "kazi" inavuka vihunzi vyote vya ndani ya nchi,iwe ni vya kisiasa au kijamii.Hapa ndio ni pamoja na uwakilishi wa kampuni katika vikao kadhaa vya "nje" vinavyoweza kuwa vinahusisha wizara na kampuni au shirika la serikali na kampuni ya uwekezaji.

Hii ndio kusema,INED anakuwa na uwezo wa kujua wapi apite na wapi pa kutokea,nani wa kumuingia na nani wa kumpeleka jambo gani ili liweze kupitishwa kwa maslahi ya kampuni.

INED anajua wapi pa kumpata Mwansheria Mkuu wa serikali na kuongea naye jinsi ya kupunguza asilimia ya mrahaba toka 5% mpaka 0%,INED ndiyo mwenye kujua wapi pa kumpata Waziri wa Nishati na madini na kumpandisha ndege kwenda London ili kutia saini uwekezaji wa mgodi wa Bulyanhulu.

INED ndiyo mwenye kujua wapi pa "kumtuliza" mbunge machachari kama Zitto Kabwe anayeisakama kampuni ya madini kwa kuisema "hovyo" bungeni.INED anaishauri kampuni kuwa ili huyu asiwaseme sana bungeni,mpelekeeni madawati 2000 kwa ajili ya shule za jimboni kwake,mradi wa maji na mjengeeni shule za msingi mbili kwenye moja ya kata mbili za jimbo lake,haswa zile kata alizopata kura chache uchaguzi uliopita.

INED,ndiyo anafanya kazi ya kumuunganisha Waziri wa Nishati na Madini na "Shirika la Misaada la Watu wa Canada",kwa pesa zinazotoka katika kampuni ya madini kwa mlango wa nyuma,ili kuja kufadhili ujenzi wa daraja,shule,visima vya maji na hata kununua nguzo za umeme ili kupeleka maendeleo jimboni kwake ili uchaguzi ujao arudi tena madarakani.

Kampuni inapotaka ushawishi wake uingie mpaka ndani ya bunge,sheria ya msamaha wa kodi ipitishwe,INED anajua ni wabunge gani wa kukutana nao ili wahakikishe mswaada huo unakuwa sheria,ili kutoa "tax holiday" kwa makampuni yote ya madini Tanganyika.

Unapomsikia Mbunge wa Tanganyika tena kutoka jimbo la Mchinga wanakovuna nazi na korosho tu,anasimama na kutoa hoja ya kuhakikisha mbunge wa Kigoma Kaskazini anatolewa bungeni kwa kufichua namna mkataba wa kuuza mgodi wetu ulivyofanyikia hoteleni,yule mbunge anakuwa siyo yeye na akili zake za kuzaliwa,ni "ushawishi" wa rupia za madini.

Gazeti la Citizen katika ukurasa wake wa mbele,liliandika kuwa mazungumzo kati ya serikali ya Tanzania na Accacia,hayatakuwa kama "Walk in the park".Yaani haiwezi kuwa rahisi hivyo,yaani tu kama matembezi ya mtu na familia yake kwenda mbuga za wanyama kufurahia uoto wa asili na uzuri wa wanyama.Itakuwa ni "maongezi magumu" ambayo tusipoangalia tunaweza kutoka kapa na tukapoteza pakubwa kuliko tulivyotegemea.

Katikati ya meza ya majadiliano,upande wa suti za watu wa Accacia,suti moja itakuwa juu ya mwili wa Mtanzania mmoja,mshairi,mwanadiplomasia na Mtanganyika halisi mkazi wa Tanga,nyika iliyozaa jina la Tanga-Nyika.Je huyu Mtanga-Nyika Juma Mwapachu atasimama upande upi siku ya majadiliano!!?Kule kwa "muajili" wake au "kwa Mama Tanzania?".. Nafikiri hata yeye...Kuna jambo analiwaza.Tungoje na tutaona,haya makinikia yamekuja na mengi,tunayoyajua tutayafukua na kuyatazama.

barafu Toronto-Canada
 

Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
6,681
2,000
Hili suala ni nyeti sana,sikudhani kama litafikia katika hatua hii.Mwapachu ni mwanadiplomasia mbobezi sana ila sidhani kama atakuwa anahusika kiundani zaidi na suala hili
 

Mkwawe

JF-Expert Member
Jun 10, 2016
1,767
2,000
Hili suala si la mtu mmoja, mwapachu ndiye aliyeonekana kuonesha ukulukumbi wa dhahiri
je wale ambao hawakujionesha hadharani wako wangapi
Mwapachu ni "Malaya" na aliwakilisha malaya wenzake wengi tu ambao hawakujifichua
ushahidi wa umalaya wake ni kipindi cha uchaguzi 2015, kabla na baada hakueleweka aende wapi na asimamie nini.
 

Daby

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
32,353
2,000
Ndiyo uzalishaji unaendelea kilio chetu kikubwa ni makenikia na sio dhahabu... wanaendelea.

Mwapachu tusimlaumu lazima afuate matakwa ya mwajiri wake wa sasa. Hayo ya Mama Tanzania ni baadae saana na hata Barrick lazima wawe wamemfuatilia kwa kina hadi kufikia kumweka hapo kama kiungo Chao kwetu.
 

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,676
2,000
Hili suala ni nyeti sana,sikudhani kama litafikia katika hatua hii.Mwapachu ni mwanadiplomasia mbobezi sana ila sidhani kama atakuwa anahusika kiundani zaidi na suala hili
Mkuu zingatia alama za funga na fungua semi kwenye "heading"
Simpi lawama Balozi moja kwa moja,wala yeye si wa kualamiwa,mimi nataka kutoa tu picha ya ujumla ya safari ya kuelekea katika majadiliano na wapi tulipotoka na jinsi hawa jamaa walivyotumia mbinu za kintelijensia kuingiza uwekezaji katka nchi yetu.

Simlaumu Balozi kwa lolote!!naeleezea tu majukumu ya Independent Non Executive Director na nafasi ya balozi katika majadiliano yanayokuja
 

Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
6,681
2,000
Mkuu zingatia alama za funga na fungua semi kwenye "heading"
Simpi lawama Balozi moja kwa moja,wala yeye si wa kualamiwa,mimi nataka kutoa tu picha ya ujumla ya safari ya kuelekea katika majadiliano na wapi tulipotoka na jinsi hawa jamaa walivyotumia mbinu za kintelijensia kuingiza uwekezaji katka nchi yetu.

Simlaumu Balozi kwa lolote!!naeleezea tu majukumu ya Independent Non Executive Director na nafasi ya balozi katika majadiliano yanayokuja
Pamoja nimekupata.Ila kama na yeye alihusika atawajibishwa pia.Tatizo linaanzia pale WAHUSIKA wengine wana kinga ya kutokuhojiwa,kushitakiwa na hata kuandikwa gazetini
 

residentura

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
2,336
2,000
Another well - written analysis from one of few well - known JF GT & "mzalendo" barafu. Kongole barafu.
Niliwahi msikia mzee P Rutabanzibwa akiongelea kuhusu "makuwadi" wakubwa watatu wa uchumi wetu. Mmoja ni huyu J,wa pili ni J pia na wa tatu naye ana J. Kwa hili nimeanza kuelewa.
 

Poise

JF-Expert Member
May 31, 2016
7,544
2,000
Hili suala ni nyeti sana,sikudhani kama litafikia katika hatua hii.Mwapachu ni mwanadiplomasia mbobezi sana ila sidhani kama atakuwa anahusika kiundani zaidi na suala hili
Jisahihishe.

Yeye kama msomi, mwanadiplomasia na kiongozi.

Tatizo ni uzalendo umepotea hapo Tanzania.

Mwapachu hawezi kuwa salama ama hahusiki yaani huwezi ukawa jikoni kisha usitambue Kama Chakula ki tayari kuliwa.
 

jobless tycoon

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
674
500
Lawama zako ni bora hata ungezipeleka kwa babake chenge kwa kutuzalia joka la makengeza kuliko huko ulikozipeleka. Hayo madai yako sio part of Mwapachu's job description. Hizo Lawama pelekea wabunge na wanasheria wetu. Huyu Mwapachu umemuonea
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
12,133
2,000
Hivi ukiwa kama mtanzania na ukaajiriwa na external agent anayefanya shughuli zake Tanzania na anakulipa vizuri mno - pengine mshahara na marupurupu ambayo hayapatikani popote nchini. At some point, ukagundua au hata kuhisi (kutokana na mienendo yenye shaka, n.k.) kwamba huyo agent anaifanyia nchi hujuma; utasimama upande wa nani? Mwajiri/agent au taifa lako?
 

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,676
2,000
Lawama zako ni bora hata ungezipeleka kwa babake chenge kwa kutuzalia joka la makengeza kuliko huko ulikozipeleka. Hayo madai yako sio part of Mwapachu's job description. Hizo Lawama pelekea wabunge na wanasheria wetu. Huyu Mwapachu umemuonea
Mkuu kuna mahali umenona nimemlaumu?Hebu paonyeshe...Halafu rudia kusoma sehemu niliyo-bold kuonyesha moja ya majukumu ya "Independent Non Executive Director"
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom