Sakata la makato elimu ya juu latua Bungeni

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
SAKATA LA MAKATO ELIMU YA JUU LATUA BUNGENI

Mbunge wa Viti Maalum Ng'wasi Kamani amesema malipo ya asilimia 15 ya mkopo kwa wanufaika wa elimu ya juu ni uvunjaji wa sheria kwa kuwa hakuna uchunguzi uliofanyika kabla ya kuanza utaratibu huo.

"Nani alifanya uchunguzi wa kuona vijana wa Tanzania wanaweza kumudu kiasi hicho kwa makato ya asilimia 15 ukijumlisha na makato mengine, je kijana huyu anabaki na kiasi gani," amesema Kamani.

Mbunge huyu ameeleza hayo Jumatano Aprili 28, 2021 bungeni mjini Dodoma akibainisha kuwa awali kulikuwa na makato ya asilimia nane ambayo licha ya ugumu wake bado ilikuwa na unafuu kiasi.

Hivi karibuni wadaiwa walilalamika ongezeko la makato ya mkopo kutoka asilimia 8 hadi asilimia 15 kwa mwezi kutoka katika mshahara ghafi wa mdaiwa/mnufaika.

Makato mengine ni tozo ya kutunza thamani ya mkopo ya asilimia 6 (Value retention fee -VRF), tozo ya asilimia moja ya shughuli za kiutalawa (Loan Administration Fee) na adhabu ya asilimia 10 ya deni linalodaiwa kwa anayechelewa kulipa deni baada ya miaka 2 tangu kuhitimu chuo.

Katika maelezo yake Kamani ameita Serikali kupeleka bungeni muswada wa sheria ili kulinusuru kundi hilo ikiwemo kufanya uchunguzi iwapo inafaa kweli mtu kuanza kulipa ndani ya miaka miwili baada ya kuhitimu masomo.
 
Back
Top Bottom